JamiiForums
βœ”
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAREKANI: Mkurugenzi Mtendaji wa #Tesla, Elon Musk amenunua 9.2% ya hisa za Twitter na kuwa mbia mkubwa akimiliki karibu mara 4 zaidi ya hisa za Mwanzilishi wake #JackDorsey mwenye 2.25%

> Taarifa hii imefanya hisa za Twitter kupanda kwa 22%

Soma https://jamii.app/AnunuaHisaTwitter
WABUNGE WAIKATAA RIPOTI YA MTO MARA

Prof. Muhongo "Ripoti kuhusu Uchafuzi wa Mto Mara ina upotoshaji. Isiwekwe hata kwenye Tovuti ya Wizara. Hakuna Mafuta Ziwa Victoria. Ikiwekwa kwenye tovuti, UNESCO watanishangaa mimi mtaalamu wa eneo hili"

> Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku (Musukuma) amesema: "Ripoti hii hatuitaki. Ni uchafu. Mimi kuanzia leo ninatangaza kujiuzulu Ubalozi wa Mazingira nilioteuliwa na Waziri Jafo kwa sababu ya mwenendo huu.”

Soma - https://jamii.app/RipotiMtoMara
DODOMA: Bunge la Tanzania limetengua Kanuni kwa ajili ya kuruhusu Mfungo wa Mwezi wa Ramadhan na mabadiliko hayo yataendelea hadi mwisho wa mfungo

> Mwisho wa shughuli za Bunge itakuwa saa 12:00 Jioni badala ya saa 1:45 Usiku

Soma - https://jamii.app/BungeTenguaKanuni
#RamadanKareem
ROBO FAINALI - CAFCC: SIMBA KUIVAA ORLANDO PIRATES

- Simba SC itavaana na Orlando Pirates katika Robo Fainali ya michuano ya Shirikisho Barani Afrika

- Simba ilimaliza ya 2 katika Kundi D ikiwa na alama 10 huku Orlando Pirates ikiwa kinara wa kundi B na alama 13

#JFSports
EWURA: BEI ZA MAFUTA ZAPANDA

Dar itakuwa, Petroli ni TSh. 2,861, Dizeli bei ni Tsh. 2,692 na Mafuta ya Taa ni Tsh. 2,682

> Tanga itakuwa Petroli ni Tsh. 2,848, Dizeli ni Tsh. 2,779 na Mtwara itakuwa Petroli ni Tsh. 2,678 na Dizeli Tsh. 2,811

Soma - https://jamii.app/MafutaYapanda
Tanzania na Uingereza zimekubaliana kuweka mikakati ya kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu wakiwemo Watoto

> Pia, Uingereza imetoa jengo kwa ajili ya kutoa Ushauri wa Kisaikolojia na Kisheria kwa Waathirika wa Ukatili wa Kijinsia

Soma > https://jamii.app/UKTZUshirikiano
RAIS PUTIN: VIKWAZO VIMEPELEKEA JANGA LA CHAKULA DUNIANI

Amesema Urusi inalazimika kuangalia kwa karibu mauzo yake ya Chakula kwa Nchi zisizo rafiki kwani vikwazo vya Magharibi vimechochea janga la chakula duniani na kuongezeka kwa bei za Nishati

Soma - https://jamii.app/PutinFoodCrisis
Umoja wa Ulaya umependekeza vikwazo vipya kwa Urusi ikiwemo marufuku ya ununuzi wa Makaa ya Mawe, Kompyuta na uingizaji Meli za Urusi kwny Bandari za EU

Ni kutokana na kuuawa raia ktk Mji wa #Ukraine uliokuwa umekamatwa na Warusi

Soma - https://jamii.app/RussiaVikwazoEU
#RussiaUkraineWar
#SRILANKA: UHABA WA DAWA WAPELEKEA MADAKTARI KUITISHA MAANDAMANO

Hospitali zimeishiwa Dawa muhimu kwasababu ya mgogoro wa kiuchumi na hali hiyo inaweza kusababisha Mfumo wa Afya kuporomoka

> Raia wanakabiliwa na upungufu wa Mafuta na Chakula

Soma - https://jamii.app/SriLankaProtests
KENYA: BIMA YA RESOLUTION YAWEKWA CHINI YA USIMAMIZI WA SERIKALI

Hatua hiyo imefikiwa kutokana na matatizo ya uendeshaji na ya kifedha

#ResolutionInsurance haitaweza kushiriki #Biashara yoyote ya Bima na Sera zake zote zimekoma kufanya kazi

Soma - https://jamii.app/ResolutionKE

#JFLeo
BUNGENI: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Jenista Mhagama amesema Serikali inatambua tatizo la Uhaba wa Watumishi hususani katika Miradi ya Sekta ya #Afya na Elimu, na Ajira zipatazo 32,000 zinatarajiwa kutolewa

Soma - https://jamii.app/SerikaliAjira

#JFLeo
DODOMA: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni amesema Vituo vya Polisi vya Daraja B vilivyopo Nchini ni 93 tu badala ya 563, hivyo kuna upungufu wa Vituo 470

> Waziri amesema hayo akiwa Bungeni Aprili 5, 2022

Soma - https://jamii.app/VituoVyaPolisi

#HumanRights
THE HAGUE: Kesi ya Ali Muhammad Ali Abd–Al-Rahman (72) anayedaiwa kuwa Kiongozi wa Janjaweed imeanza kusikilizwa ktk Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu

> Ali amekana mashtaka yote 31 ya Uhalifu wa Kivita dhidi ya Binadamu ktk mzozo wa #Darfur

Soma: https://jamii.app/KesiWanamgambo
MAREKANI: Kampuni ya Kutengeneza 'Chip' za Kompyuta ya Intel Corp imesitisha uuzaji wa 'Chip' hizo kwa Nchi za #Urusi na #Belarus

> Intel imesema inaungana na Jumuiya za Kimataifa kulaani uvamizi wa Urusi kwa #Ukraine

Soma: https://jamii.app/IntelKusitisha

#RussiaUkraineConflict
BUNGENI: Serikali imeagiza Wazalishaji na Wasambazaji wa bidhaa muhimu kushusha bei za bidhaa zinazopandishwa pasipo kuendana na uhalisia wa Soko

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa asema hivi karibuni kumekuwepo na taarifa za uhaba na upandaji wa bei usioendana na uhalisia wa Soko ktk bidhaa za Ujenzi, Vyakula, Nishati na pembejeo za Kilimo

Soma - https://jamii.app/BeiBidhaaMuhimu
JANUARY MAKAMBA: Tunayo mafuta ya kutosha kutumika kwa takriban siku 27. Pia, Serikali imeshaagiza mafuta yatayotumika Mwezi wa Tano na wa Sita ambayo yapo kwenye Mchakato

> Amesema hayo ktk Mkutano na Waagizaji na Wasambazaji wa Mafuta Nchini

Soma - https://jamii.app/MafutaYapoTZ
RAIS SAMIA: SHERIA YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI IKAMILISHWE

Ameelekeza Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuhakikisha inakamilisha uandaaji wa Sheria ya Kulinda Taarifa Binafsi za Watu

JamiiForums imekuwa mstari wa mbele kuitetea Haki hii ya Faragha ambayo ipo Kikatiba

Soma - https://jamii.app/RaisSheriaTaarifa

#DataProtection
Zaidi ya Watu milioni 346 Barani Afrika wanakabiliwa na Baa la Njaa huku baadhi ya Familia zikipata Mlo 1 kwa Siku

Hali ni mbaya Burkina Faso, Mauritania, #Somalia, Ethiopia, #Kenya, Sudan Kusini, DRC, Sudan, Nigeria, Chad, #Cameroon, Niger na Mali

Soma https://jamii.app/BaaNjaaAfrika
MARA: MBARONI KWA KUFUNGISHA NDOA WATOTO

Waliokamatwa siku ya tukio Aprili 2, 2022 ni Nyang'ombe Magere (50) na Ghati Masero (38) wazazi wa mtoto wa kiume, Msimamizi wa Ndoa (10), Bwana Harusi (12), Bibi Harusi (16) na Kibaki Rioba (23)

Soma - https://jamii.app/NdoaZaUtotoni
EAC: MWISHO WA MATUMIZI YA 'PASSPORT' ZA ZAMANI NI NOVEMBA

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imetangaza Novemba 2022 kuwa ndio mwisho wa matumizi ya Pasi za Kusafiria (Passport) za zamani tofauti na ilivyotangazwa awali kuwa ni Aprili 4, 2022

Soma: https://jamii.app/PassportEA