JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
URUSI KUKABILIWA NA VIKWAZO KUTOKANA NA MZOZO NA UKRAINE

Urusi iko hatarini kukabiliwa na vikwazo kutoka EU kuhusiana na mgogoro unaoendelea kati yake na #Ukraine

Vikwazo hivyo vitahitaji ridhaa ya Nchi Wanachama zote 27

Soma - https://jamii.app/VikwazoUrusi

#RussiaUkraineConflict
TCRA: KASI YA INTANETI INASABABISHA BANDO KUISHA HARAKA

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Jabiri Bakari amesema wameelekeza watoa huduma kuunda 'App' ya kusaidia watumiaji kufuatilia matumizi

Asema kuwa na 'Apps' nyingi kwenye simu humaliza bando haraka

Soma - https://jamii.app/InternetKuisha
KISUTU, DAR: Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), Sylvester Mwakitalu leo Februari 23, 2022 amemfutia mashtaka ya Uchochezi M/kiti wa Baraza la Wazee la CHADEMA, Hashimu Issa Juma

Alikuwa akituhumiwa kutoa tuhuma za chuki dhidi ya Viongozi

Soma - https://jamii.app/HashimuFreed
#Siasa
UMOJA WA ULAYA KULEGEZA MASHARTI YA COVID-19 KWA WATALII

Baraza la Umoja huo limependekeza kuanzia Machi 2022 masharti ya Karantini yaondolewe kwa waliochanjwa

Pia, Watoto chini ya Miaka 6 wasilazimike kupimwa wanaposafiri na Watu wazima.

Soma - https://jamii.app/TourismEUMarch
#UVIKO3
MDAU: NAMNA UNAVYOWEZA KUMSAIDIA MTOTO KUKABILIANA NA MSIBA WA MPENDWA WAKE

1. Kuwa muwazi na mweleze kilichotokea kwa njia rahisi anayoweza kuelewa. Tumia maneno yenye Uhalisia (amefariki), usimfiche kwa kumwambia amelala

2. Jaribu kurudisha Mazingira katika hali ya kawaida kwa haraka iwezekanavyo kutegemea na nani anaishi na Mtoto kwa wakati huo. Mtoto atajisikia kuwa yuko salama kama ratiba za kila Siku hazitabadilika.

Soma - https://jamii.app/MtotoMsiba
#Malezi
NIGER: WANAMGAMBO WAWILI WAUA WATU 18

Wanamgambo hao waliokuwa kwenye pikipiki walishambulia lori lililokuwa likisafirisha watu

Eneo la Magharibi Nchini humo limekuwa likikabiliwa na uasi kwa miaka mingi licha ya jitihada mbalimbali

Soma - https://jamii.app/NigerWatu18
#JFLeo
TANZANIA KUPOKEA NDEGE TANO HIVI KARIBUNI

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi Dkt. Ally Possi amesema ili kukabiliana na hasara za ATCL wataboresha Viwanja vya Ndege Nchini

> Amesema ndege 5 zimenunuliwa ili kuongeza Mapato ya Serikali

Soma https://jamii.app/NdegeATCL
#JFLeo
Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) limetoa Onyo kwa wanaotumia Nembo ya Baraza hilo kupotosha Misamiati ya #Kiswahili na kusambaza Mtandaoni

Atakayebainika atalipa faini isiyopungua Milioni 5 au kifungo Miaka 3 jela ama vyote kwa pamoja

Soma - https://jamii.app/UpotoshajiBAKITA
#Lugha
IRAN YAREJESHA CHANJO 820,000 ZILIZOTENGENEZWA NA MAREKANI

Chanjo hizo zilitolewa kama Msaada na #Poland

Mwaka 2020, Kiongozi Mkuu wa #Iran, Ali Hosseini Khamenei alisema Chanjo kutoka Uingereza na Marekani ni haramu, na hawatazipokea

Soma - https://jamii.app/IranMarekani

#UVIKO3
MOSHI: ANAYETUHUMIWA KUMUUA MAMA YAKE AFIKISHWA MAHAKAMANI

Washtakiwa 3 akiwemo Wendy Mrema (Mtoto wa Marehemu) wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, kwa tuhuma za kumuua Patricia Ibreack Paul (66) na kumzika kwenye shimo nje ya Makazi yake

Soma - https://jamii.app/WendyMahakamani
MSUMBIJI: TOVUTI ZA SERIKALI ZADUKULIWA

Wadukuzi wa 'Yemen Hackers' wamedai kudhibiti tovuti 34 za Serikali ya Msumbiji na wanataka wapewe takriban Tsh. Milioni 46

Wametaka Fedha ndani ya saa 24 au watavujisha taarifa za siri

Soma - https://jamii.app/WadukuziMsumbiji

#DigitalSecurity
HOJA: UNATUMIA MBINU GANI KUTATUA CHANGAMOTO ZA KIMALEZI?

Mdau ametolea Mfano changamoto za Mtoto kutokupenda kula, kwenda Shuleni, kuchanganyika na wenzake, Uwezo mdogo Kimasomo, Utundu kupita kiasi na mengineyo

Anauliza umewahi kukumbana na tatizo gani la kimalezi na ulitatua vipi na kufanikiwa?

Mjadala - https://jamii.app/ChangamotoMalezi

#Malezi
UKRAINE YATANGAZA HALI YA HATARI

Bunge limethibitisha hali ya hatari kwa siku 30. Mamlaka zinaweza kuzuia raia kutembea na mikutano kwa maslahi ya Taifa

> Pia Serikali imetangaza huduma ya lazima ya kijeshi kwa wanaume waliofikia umri wa kupigana

Soma https://jamii.app/StateOfEmergency
UN YAITAKA URUSI KUONDOA WANAJESHI #UKRAINE

Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres amesema wengi wameshapoteza maisha, na ni wakati wa kuipa nafasi Amani

Rais wa Marekani, Joe Biden asema Urusi itabeba lawama kwa yatakayotokea

Soma https://jamii.app/UrusiUN

#RussiaUkraineConflict
PAPA FRANCIS ATANGAZA MACHI 2 KUWA SIKU YA KUFUNGA NA KUIOMBEA #UKRAINE

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani ametoa wito kwa watu kutumia Siku ya Jumatano ya Majivu kuiombea Ukraine baada ya ripoti za Urusi kuanza mashambulizi

Soma https://jamii.app/PapaUkraine

#RussiaUkraineConflict
MDAU: MAKOSA YA KIFEDHA YANAYOFANYWA NA VIJANA WENGI

1. Kutumia Fedha uliyoipata kabla ya kuweka Akiba: Msemo wa 'Ponda Mali kufa kwaja' hupelekea Vijana wengi kufanya Matumizi yasiyo na ulazima na kukosa Akiba

2. Kutupa Risiti (Stakabadhi za Malipo): Unaweza kudhani risiti za vitu unavyonunua hazina umuhimu kwako lakini hukusaidia kutambua tabia/mwenendo wa Matumizi yako

Soma - https://jamii.app/MoneyMistakes

#Maisha
PUTIN: ATAKAYEINGILIA MZOZO WA UKRAINE ATAPATA PIGO LA KIHISTORIA

Baada ya milipuko kuripotiwa Mji wa #Kyiv, Rais wa Urusi asema, "Yeyote atakayeingilia kutoka Mataifa ya Magharibi, atakutana na matokeo ambayo hajakutana nayo"

Soma - https://jamii.app/OnyoPutin

#RussiaUkraineCrisis
#UPDATES: Takriban Watu 6 wameripotiwa kupoteza Maisha katika shambulio la Bomu llililofanywa na vikosi vya Urusi Nchini #Ukraine

Maafisa wanasema shambulio dhidi ya kambi ya Jeshi ya #Podilsk, nje ya Mji wa #Odessa limesababisha Watu wengine saba kujeruhiwa, na 19 hawajulikani walipo.

#RussiaUkraineConflict #JamiiForums
MALEZI: MTENGENEZEE MTOTO MAZINGIRA YA KUJISOMEA NYUMBANI

1. Kama inawezekana ni vema kuwe na chumba/sehemu maalumu isiyokuwa na usumbufu kwaajili ya Mwanafunzi kujisomea

2. Hakikisha una ratiba ya Masomo kwa Siku, Wiki na kwa Mwezi. Kwenye ratiba kuwe na muda wa kujisomea vitabu vya ziada

3. Tunza Mitihani yote ya Mtoto iliyopita ili kutathmini Maendeleo yake. Mwanafunzi awe na ratiba maalumu ya kuangalia TV au kutumia Vifaa vya Kieletroniki.

Soma - https://jamii.app/MasomoNyumbani
#Malezi
SHINYANGA: WATUMISHI 6 WAFUKUZWA KAZI KWA UTORO, KUGHUSHI NYARAKA

Baraza la Madiwani Wilaya ya Shinyanga limewafukuza kazi Watumishi hao kutoka Idara ya Afya na Idara ya Utawala

Watumishi wengine 2 watakatwa 15% ya Mishahara yao kwa Miaka mitatu

Soma - https://jamii.app/WafukuzwaUtoro