JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KISUTU, DAR: MADABIDA NA WENZAKE WAACHIWA HURU

Aliyekuwa M/kiti wa CCM - Dar, Ramadhani Madabida na wenzake 5 walikuwa wakikabiliwa na mashtaka matano likiwemo la kusambaza makopo 7,776 ya Dawa Bandia za kufubaza VVU (ARV) aina ya Antiretroviral.

Soma - https://jamii.app/MadabidaFree
MTWARA: MWANAFUNZI AANDIKA BARUA KWA MWALIMU MKUU KUKATAA SHULE

Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza Shule ya Sekondari Madimba ameandika barua kwa Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo kukataa kuendelea kusoma, akisema Masomo yamemshinda

Soma - https://jamii.app/ShuleBasiUvuvi

#JFLeo
NAIROBI, KENYA: MUSWADA WA KUDHIBITI KAMARI WAANDALIWA

Muswada huo utafanya Michezo ya kubeti na kamari Jijini #Nairobi iwe inachezwa kwenye Hoteli zenye hadhi ya Nyota Tano na Casino tu, huku muda wa kucheza ukiwa saa 2 usiku hadi 12 alfajiri

Soma - https://jamii.app/BettingGambling
UKRAINE: RAIS KUMPATIA SILAHA KILA RAIA ANAYETAKA KUIPIGA URUSI

Rais Volodymyr Zelensky amewahamasisha Raia kupigania Nchi yao, na kusema silaha zitatolewa

Kufuatia Urusi kuivamia, #Ukraine imesitisha uhusiano wake wa Kidiplomasia na Taifa hilo

Soma - https://jamii.app/SilahaUkraine
WANAOVUJISHA MIAMALA YA WATEJA KUCHUKULIWA HATUA

Waziri wa Sheria, George Simbachawene ameagiza Kampuni za Mawasiliano kuchunguzwa na hatua kuwachukuliwa dhidi ya Watumishi ambao wanavujisha Taarifa za Miamala ya Wateja kwa wahalifu wa Mitandaoni

Soma - https://jamii.app/WatejaTaarifa
SCHALKE O4 KUONDOA NEMBO YA KAMPUNI YA URUSI KWENYE JEZI

- Klabu hiyo ya Ujerumani imethibitisha kuondoa kwenye jezi zake nembo ya mdhamini mkuu wa Klabu, Kampuni ya Gazprom inayomilikiwa na Urusi

- Imesema sehemu ilipokuwa inakaa nembo yatawekwa maneno β€˜Schalke 04’

#JFSports
TANESCO: KUANZIA JULAI, UMEME UTAINGIA BILA KUANDIKA TOKEN KWENYE MITA

Kuanzia Julai, Smart Meters zitaanza kutumika. Umeme utawaka moja kwa moja kama ilivyo huduma za king'amuzi

Suala la Token liliwahi kulalamikiwa kupitia #StoriesOfChange ya JF

Soma - https://jamii.app/SmartMeters
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#UPDATES: Takriban Raia 10 na Wanajeshi 40 wa #Ukraine wameripotiwa kuuawa katika mashambulizi ya Anga yaliyofanywa na Urusi leo Februari 24, 2022 katika Mji wa #Odessa

Taarifa ya Vifo hivyo imetolewa na Msaidizi wa Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine alipozungumza na Waandishi.

#RussianInvasion #RussiaUkraine
MDAU: VITU VYA KUZINGATIA KABLA YA KUHAMIA DAR

Anashauri wanaotaka kuhamia Dar wahakikishe wana Ujuzi na Nidhamu ya Fedha

Asema si tatizo Kijana wa Mkoani kuja Dar, lakini ni muhimu kujiuliza; Mambo yakienda tofauti utafanyaje?

Soma - https://jamii.app/DarKuhamia

#StoriesOfChange
UKRAINE: Rais Volodymyr Zelensky ameagiza wanaume nchini humo wenye umri wa miaka 18-60 kuilinda nchi yao

> Taarifa zinasema Majeshi ya Urusi yameshauteka Uwanja wa Ndege wa Jeshi la Ukraine pamoja na Kinu cha Nyuklia cha Chernobil

Soma https://jamii.app/WanaumeUkraine
Ukraine: Watu zaidi ya 137 wahofiwa kufariki baada ya mlipuko uliosikika katika Mji Mkuu wa Nchi hiyo, Kyiv

Majeshi ya Urusi yameonekana kuendelea na mashambulizi mbali na kuwekewa vikwazo na Marekani na Ulaya

#JamiiForums #RussiaUkraineConflict
GEITA: AUAWA KWA TUHUMA ZA KUJARIBU KUMBAKA MWANAFUNZI

Kijana mwenye umri kati ya miaka 18 - 22 ameuawa na kuchomwa moto akidaiwa kujaribu kubaka Mwanafunzi aliyekuwa akielekea Shuleni

M/kiti wa Mtaa anashikiliwa na Polisi kusaidia kubaini wahusika

Soma https://jamii.app/GeitaAuawa
❀1
#UPDATES: Mashirika ya Ndege ya Uingereza yamepigwa marufuku kutua katika Viwanja vya Ndege vya Urusi pamoja na kupita kwenye Anga lake

Uamuzi huo unafuatia uamuzi wa Uingereza kupiga marufuku Shirika la Ndege la Urusi, #Aeroflot kutua Nchini Uingereza.

#RussiaUkraineConflict
πŸ‘1
UEFA: FAINALI YA KLABU BINGWA ULAYA HAITAFANYIKA URUSI

- UEFA imehamisha fainali ya Klabu Bingwa Ulaya kutoka St. Petersburg, Urusi kwenda Paris, Ufaransa

- Fainali hiyo itakayochezwa Mei 28, 2022 itachezwa katika uwanja wa Stade de France badala ya Gazprom Arena

#JFSports
πŸ‘1
SERIKALI: WATANZANIA WALIO UKRAINE WAWE WATULIVU

Wizara ya Mambo ya Nje imesema hakuna Mtanzania aliyepata madhara hadi sasa

Serikali imewashauri Watanzania wafuate maelekezo ya #Ukraine, na kuwasiliana na Ubalozi

Soma - https://jamii.app/UkraineWatanzania

#RussiaUkraineConflict
UKRAINE YAOMBA MSAADA WA MAJESHI YENYE NGUVU

Rais wa #Ukraine, Volodymyr Zelensky amelalamika Mataifa yenye nguvu kuwaacha wajipambanie huku wakitazama kwa mbali

> Amesema vikwazo vilivyowekwa havijamshawishi Rais Vladimir Putin kuacha mashambulizi

Soma https://jamii.app/UkraineYaombaMsaada
KIGOMA: MGANGA ATUHUMIWA KUMUUA MTEJA ALIYETAKA KUZIKA FEDHA ZA BIASHARA

Dereva wa Pikipiki na Mganga wa Kienyeji wanatuhumiwa kumuua na kisha kumfukia Mwanamke aliyekuwa ameenda kuzindika Fedha za Biashara kiasi cha Tsh. Milioni 9

Soma - https://jamii.app/MtejaKifoZindiko
#HumanRights
MAREKANI: ASKARI 3 WANAOTUHUMIWA KUMUUA GEORGE FLOYD WAKUTWA NA HATIA

Maafisa hao wa zamani wa #Minneapolis walishtakiwa kwa kumnyima Floyd Haki yake ya matibabu wakati Afisa Derek Chauvin alipomkandamiza kwa goti shingoni mnamo Mei 25, 2020

Soma - https://jamii.app/FloydCaseGuilt
#UKRAINE YATAKA MAZUNGUMZO NA URUSI

Rais Volodymyr Zelensky ametaka mazungumzo na Rais Vladimir Putin ili kunusuru Raia wasio na hatia

China imesema Urusi ipo tayari kwa mazungumzo baada ya Rais Putin kuongea na Rais Xi Jinping

Soma https://jamii.app/Mazungumzo

#RussiaUkraineConflict