JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
NINI MAANA YA DHANA YA HAKI ZA KIJAMII?

Humaanisha uwepo wa Haki sawa kwa watu wote na uwezekano wa kila mtu, bila ubaguzi, kufaidika na Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii

Baadhi ya Haki za Kijamii ni pamoja na Usawa mbele ya #Sheria na Haki ya kupata Huduma za Afya

Soma - https://jamii.app/SJD2022

#SocialJusticeDay #SocialJustice
NIGER: Watoto saba (7) wameuawa na wengine watano (5) kujeruhiwa vibaya nchini humo baada ya shambulizi la anga la Jeshi la #Nigeria lililolenga wapiganaji walioko mpakani

> Mamlaka zinaendelea kufuatilia tukio hilo

Soma https://jamii.app/NigeriaNiger

#JFMatukio
HISTORIA: Chips za Viazi (Crisps) zilianza kutengenezwa Mwaka 1853 baada ya Mmarekani mweusi, George Speck (Mpishi) kupokea malalamiko ya Mteja akimlaumu kuwekewa Viazi vyenye mapande makubwa sana

Inadaiwa ili kuwakomoa Wateja, Speck alianza kukata vipande vidogovidogo mfano wa Karatasi lakini Wateja wakatokea kuvipenda sana.

Soma zaidi - https://jamii.app/SaratogaChips

#JFHistoria
40% YA WATU HAWATUMII LUGHA MAMA KWENYE ELIMU

Shirika la UN linalohusika na Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limesema Jamii hizo zimelazimika kufahamu Lugha zaidi ya moja

Februari 21 ni Siku ya Kimataifa ya Lugha Mama

Soma - https://jamii.app/LughaMama

#MotherLanguageDay #JFLugha
MALEZI: TUNZA AFYA YA MTOTO KWA KUMFUNDISHA USAFI

Usafi wa Kinywa: Mpigishe Mtoto Mswaki kila siku Asubuhi na ikiwezekana kila baada ya kula. Mfundishe namna ya kuswaki vizuri ili kuzuia kuoza kwa Meno na Magonjwa ya Fizi

Usafi wa Mikono: Wafundishe Watoto kunawa Mikono kwa Maji safi na sabuni kila wanapotoka Kucheza, kabla ya Kula, baada ya Kula na baada ya kutoka Maliwato

Soma - https://jamii.app/UsafiWatotoAfya

#JFMalezi #Parenthood
Uwajibikaji unapima kiwango ambacho Serikali inatekeleza majukumu yake katika kueleza na kuhalalisha Maamuzi yake kwa Umma

Ufanisi mkubwa wa #Uwajibikaji unaainishwa kwa namna ambavyo Wadai Haki/Wananchi wanaelezea mahitaji yao, lakini pia unahusiana na Nafasi, Uwezo na Utayari wa Watendaji kuwajibika kwa Matendo

Soma - https://jamii.app/UwajibikajiUfanisi
#Accountability #Democracy
MAGU: WAVUNJA MAKABURI NA KUIBA MISALABA, NONDO

Wananchi wamedai baadhi ya Makaburi yameharibiwa na kuachwa wazi au na mianya mikubwa huku vitu vikiibwa

Mkuu wa Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza, Salum Kalli ameagiza wahusika wasakwe na kutiwa nguvuni

Soma - https://jamii.app/MakaburiMagu

#JFUwajibikaji
LINDI: Wanachama Wanne wa CHADEMA wamehukumiwa kifungo cha miaka 8 kwa kosa la kuharibu mali na kujeruhi watu wakiwemo Askari Polisi siku ya Uchaguzi Mkuu (Oktoba 28, 2020)

Katika utetezi walisema wahurumiwe kwa madai wana Familia zinazowategemea

Soma - https://jamii.app/LindiChadema

#JFSiasa
UNHCR: IDADI KUBWA YA WAKIMBIZI DUNIANI HUTOKEA NCHI TANO

Nchi hizo ni #Afghanistan, Myanmar, Sudan Kusini, Syria na #Venezuela

Kwa kila sekunde, kuna Mtu 1 anayakimbia Makazi yake kutokana na Mabadiliko ya Tabianchi/Hali ya Hewa

Soma - https://jamii.app/ClimateRefugees
#HumanRights
SHINYANGA: MBARONI KWA KUIBA MTOTO WA SIKU 20

Rehema Saidi (47) amekamatwa kwa tuhuma ya kuiba Mtoto Kituo cha Afya Lunguya

Wito umetolewa kwa Serikali kuimarisha ulinzi katika Vituo vya Afya na Zahanati ili kudhibiti wizi wa Watoto

Soma - https://jamii.app/WiziMtoto

#JFMatukio
WAZIRI NAPE: SHERIA YA ULINZI WA DATA NI YA MUHIMU

Amesema ni ya msingi katika Tanzania ya kidijitali ili watu wajiamini na kuwa huru

JamiiForums imekuwa mstari wa mbele kuitetea Haki ya Faragha kwa mujibu wa Ibara ya 16 ya Katiba

Soma https://jamii.app/NapeData

#DataProtection #DataPrivacy
MAREKANI YADAI INA ORODHA YA WANAOPASWA KUUAWA NA URUSI ITAKAPOIVAMIA UKRAINE

Marekani imedai miongoni mwa walengwa ni wapinzani wa kisiasa na makundi madogo ya watu wa Dini

Urusi imeendelea kukanusha kuwa na mpango wa kushambulia Ukraine

Soma - https://jamii.app/UrusiUkraine
#JFLeo
TANZANIA KUPATA MKOPO WA TRILIONI 1.5 KUTOKA BENKI YA DUNIA

Benki ya Dunia (WB) na #Tanzania zimesaini Mikataba ya Mkopo wa masharti nafuu wa Dola Milioni 650 kwa ajili ya Miradi ya kuboresha #Elimu na kuimarisha Usalama na umiliki ardhi

Soma - https://jamii.app/MkoboTrilioni

#Governance
HOJA: UNATAMANI UZEE WAKO UWEJE?

Mdau wa JamiiForums.com anasema akifikisha Miaka 60 hataki kutumia nguvu nyingi kutafuta riziki

Anatamani uwe wakati wa kukaa na Wajukuu zake. Pia, hatamani kuishi Mjini ambako kuna msongamano wa Watu

Je, nawe unataka Uzee wako uweje?

Mjadala - https://jamii.app/TamaaUzee
#Maisha
#MALI: Bunge la Mpito limepitisha kwa Kura zote Muswada wa kutawaliwa na Jeshi kwa miaka mitano. Mali iliingia katika Utawala wa Kijeshi baada ya Mapinduzi ya Mei 2021

Jumuiya mbalimbali zinashinikiza Utawala wa Kiraia kurejeshwa

Soma - https://jamii.app/MaliJeshi

#Democracy
Umoja wa Ulaya umewawekea Vikwazo Maafisa wa #Myanmar pamoja na #Biashara za Mafuta na Gesi kutokana na Mapinduzi ya Mwaka mmoja uliopita

50% ya Mapato ya Myanmar yanatokana na Fedha za Kigeni zinazopatikana kupitia rasilimali ya Gesi

Soma - https://jamii.app/EUBanMyanmar

#Democracy
BRAZIL: MAFURIKO YAUA WATU 176

Mvua kubwa iliyonyesha huko #Petropolis iliwafunika watu wengi kwenye tope na hadi sasa watu zaidi ya 110 bado hawajulikani walipo

Mvua zimesababisha mafuriko na maporomoko maeneo mbalimbali Nchini #Brazil

Soma - https://jamii.app/BrazilVifo176
#JFLeo
#PAKISTAN: WANAOKOSOA MAMLAKA MTANDAONI KUFUNGWA HADI MIAKA 5

Wanaokosoa Jeshi, Mahakama au Maafisa wa Umma Mtandaoni watafungwa Miaka 5 na hakuna dhamana

Wanaharakati wanasema Sheria inazidi kuminya Uhuru wa Kujieleza ktk Taifa hilo

Soma - https://jamii.app/PakistanLawSM
#FreeSpeech
JE, WAJUA; Leo 22/02/2022 ni #Palindrome, ikimaanisha Namba inaweza kusomeka kwa kwenda mbele au kurudi nyuma bila kupoteza thamani

Pia leo ni 'Ambigram' ambayo humaanisha Sanaa inayoweza kufanya neno/namba lisomeke juu chini, na chini juu

Soma https://jamii.app/Paliondrome

#TwosDay
DAKTARI: MATUMIZI YA P2 HUCHANGIA MIMBA KUTUNGA NJE YA KIZAZI

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Godfrey Chale akizungumza na Global amesema utafiti uliofanyika #Ghana 2003 ulionesha Vidonge vya P2 husababisha Mimba kutungwa nje hasa kwa wanakosea matumizi

Soma - https://jamii.app/P2EctopicPreg
#Afya