JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
POLEPOLE: NIMEPATA MASHTAKA YA KURUSHA MAUDHUI YANAYOPOTOSHA KUHUSU CORONA

Asema amepokea Mashtaka yanayosema kupitia Kipindi chake cha Shule ya Uongozi, amerusha Maudhui yanayoweza kuchochea Watanzania kuweza kugomea Kampeni ya Kitaifa ya #COVID19

Soma https://jamii.app/MashtakaPolepole

#JFLeo
SIMBA NA YANGA ZATOSHANA NGUVU KWA MKAPA

- Klabu za Simba na Yanga zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya goli 0-0 katika mchezo wa Ligi ya NBC

- Yanga inaendelea kuwa kileleni mwa Ligi ikifikisha alama 20 na Simba inabaki katika nafasi ya 2 ikiwa na alama 18

#JFSports
BENIN: Mahakama imemhukumu mmoja wa Wapinzani wakuu wa Rais Patrice Talon, Reckya Madougou, kifungo cha miaka 20 jela kwa kuhusika katika vitendo vya ugaidi

Hukumu yake imekuja siku chache baada ya Mpinzani mwingine kuhukumiwa miaka 10 gerezani

Soma - https://jamii.app/ReckyaBenin
MAREKANI: 70 WAPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA KIMBUNGA

Gavana wa Jimbo la #Kentucky amesema idadi ya vifo inaweza kuzidi 100 kwa rekodi za Majimbo mengine

Kimeharibu Kiwanda cha Mishumaa, eneo la Kampuni ya #Amazon na nyumba ya wazee ya Arkansas

Soma https://jamii.app/TornadoDeathUS
#JFLeo
DAR: Rais Samia Suluhu Hassan amesema Polisi wanapokamata watu hawatakiwi kufanya vitisho, lakini hali inayoonekana Mitaani ni ya vitisho na kutia hofu

Asema, "Wakati mwingine mtu anakamatwa bila kosa la maana. Zipo tuhuma za Rushwa zinasemwa"

Soma - https://jamii.app/RaisSamiaPolisi
AUSTRIA: Watu waliopata chanjo wataruhusiwa kuingia kumbi za sinema na burudani na maeneo mengine ya umma

> Wasiopata chanjo hawataruhusiwa kutoka nje na kujumuika na wenzao ila kwasababu za msingi kama kununua chakula na kumuona daktari

Soma https://jamii.app/AustriaCOVID19
#UVIKO3
Kiharusi ni hali inayotokea pale mishipa inayosambaza Damu kwenye Ubongo inapopatwa na misukosuko kiasi cha kushindwa kupeleka Damu kwenye Ubongo na hivyo kuathiri ufanyaji kazi wake

Unafahamu vitu vinavyoweza kukuweka katika hatari ya kupata Kiharusi? Je, ni kwa kiasi gani mwenendo wako wa maisha unaweza kupelekea kupata Kiharusi?

Kufahamu mengi zaidi, Ungana nasi katika Mjadala na Wataalamu utakaofanyika kupitia Clubhouse leo Desemba 13, 2021

Link - https://www.clubhouse.com/join/jamiiforums/YcIowdFT/xkaQ6BkE
AFRIKA KUSINI: Rais Cyril Ramaphosa amepima na kukutwa na #COVID19. Anaendelea na matibabu na majukumu ameyaacha kwa Naibu Rais, David Mabuza

> Alianza kuonesha dalili baada ya kutoka kwenye ibada ya Kumbukumbu ya Rais FW Klerk

Soma https://jamii.app/RamaphosaMaambukizi

#UVIKO3
Mshiriki wa #StoriesOfChange amesema Wahalifu wa Mtandaoni huweza kupata taarifa kwa kushika kifaa cha Mtu au kutumia programu maalumu

Ameshauri kupakua programu ktk masoko yanayoaminika. Pia, Usinunue Simu au Kompyuta iliyotumika

Soma - https://jamii.app/CyberCriminals

#DigitalSecurity
Unafahamu vitu vinavyoweza kukuweka katika hatari ya kupata Kiharusi?

Je, ni kwa kiasi gani mwenendo wako wa maisha unaweza kupelekea kupata Kiharusi?

Kufahamu zaidi, Ungana nasi katika Mjadala na Wataalamu utakaofanyika Clubhouse leo Desemba 13

Link - https://www.clubhouse.com/join/jamiiforums/YcIowdFT/xkaQ6BkE

#JamiiForums
MDAU: UMUHIMU WA KILA MTANZANIA KUJIFUNZA KIINGEREZA

Anasema kumekuwa na upotoshaji kuhusu Kiingereza, Watanzania wameaminishwa kujifunza Lugha hiyo si Uzalendo

Anasisitiza, Mtu asiyejua Kiingereza hatoweza kuendana na kasi ya dunia kwa sasa. Anashauri Serikali kuanzisha programu kuhamasisha watu kujifunza Kiingereza

Soma - https://jamii.app/WatanzaniaKiingereza

#StoriesOfChange
Ripoti ya CAG ya Miradi ya Maendeleo mwaka 2019/20 inaonesha kati ya mapendekezo 3,126 yaliyotolewa mwaka 2018/19, ni mapendekezo 1,071 sawa na 34% ndiyo yametekelezwa kikamilifu

Mapendekezo 623 sawa na 20% yapo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Mapendekezo 1,024 sawa na 33% hayajatekelezwa

Soma - https://jamii.app/UtekelezajiMapendekezo

#JFUwajibikaji
👍1
Unafahamu vitu vinavyoweza kukuweka katika hatari ya kupata Kiharusi?

Je, ni kwa kiasi gani mwenendo wako wa maisha unaweza kupelekea kupata Kiharusi?

Kufahamu zaidi, Ungana nasi katika Mjadala na Wataalamu utakaofanyika Clubhouse leo Desemba 13

Link - https://www.clubhouse.com/join/jamiiforums/YcIowdFT/xkaQ6BkE
DAR: Rais Samia amesema ifikapo 2025, Serikali inalenga Sekta ya Madini iweze kuchangia 10% ya Pato la Taifa

Asema, "Hali ya utoroshwaji Madini Nchini haikubaliki na hatutaruhusu Uhujumu huu kuendelea. Zifanyike doria ili wahusika wajulikane"

Soma - https://jamii.app/MadiniTZ
RAIS SAMIA AONYA VIONGOZI KUTUMIA UBABE MIGODINI

Amewataka Wakuu wa Wilaya, Wabunge na Serikali za Mitaa kutoa ushirikiano kwa Wananchi

Asema, "Wabunge ambao maeneo yenu miradi hii ipo, iwasaidie kujenga Maendeleo ya Nchi sio iwajenge ninyi"

Soma https://jamii.app/UbabeMigodini

#JFLeo
DROO YA #UEFA: MAN. UTD YAPANGIWA PSG, CHELSEA YAPEWA LILLE

- Droo ya Klabu Bingwa Ulaya hatua ya 16 Bora imefanyika leo ambapo Bingwa Mtetezi, Chelsea atakutana na Lille

- PSG itakutana na Man. Utd, Man. City itaivaa Villarreal na Liverpool itakutana na Salzburg

#JFSports #UCL
Taarifa ya Mwezi ya Maendeleo ya Uchumi inayotolewa na BoT imeonesha 23.2% ya Fedha zinazokopwa nje ya Nchi zimetumika kwa usafiri na Mawasiliano Oktoba 2021

16.2% ya Fedha hizo hutumika kwa ustawi wa Jamii na Elimu. Sekta ya Utalii imetumia 1.0%

Soma - https://jamii.app/DeniFedha
IRINGA: WATU 9 WAFARIKI KWA AJALI YA GARI LA MAGAZETI

Watu tisa wamefariki na wengine 3 kujeruhiwa baada ya Gari lililokuwa linatokea Dar kuelekea Mbeya kupata ajali Kijiji cha Mahenge

Chanzo cha Ajali hiyo ni Mwendokasi

Soma - https://jamii.app/AjaliMagazeti

#JamiiForums
#UEFA: DROO YA HATUA YA 16 KURUDIWA

- UEFA imesema droo hiyo itachezeshwa upya baada ya Man. Utd kwa bahati mbaya kupangwa dhidi ya Villarreal wakati timu hizo zimetoka kundi moja

- Pia, Man. Utd kuondolewa kama moja ya timu zinazoweza kukutana na Atletico Madrid

#JFSports
BoT: NDANI YA MWAKA, MASHIRIKA YA UMMA YAMEONGEZA KUKOPA NJE KWA 1024.2%

Taasisi za Umma zilikuwa zinadaiwa Tsh. Bilioni 119.1 Oktoba 2020 na Oktoba 2021 zinadaiwa Tsh. Trilioni 1.174

Deni la Taifa limeongezeka kwa Tsh. Trilioni 10.1 ndani ya Mwaka

Soma https://jamii.app/MashirikaYaUmma