JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Unafahamu vitu vinavyoweza kukuweka katika hatari ya kupata Kiharusi?

Je, ni kwa kiasi gani mwenendo wako wa maisha unaweza kupelekea kupata Kiharusi?

Kufahamu zaidi, Ungana nasi katika Mjadala na Wataalamu utakaofanyika Clubhouse leo Desemba 13

Link - https://www.clubhouse.com/join/jamiiforums/YcIowdFT/xkaQ6BkE
DROO YA #UCL: CHELSEA vs LILLE, MAN. UTD vs ATLETICO

- Baada ya droo ya hatua ya 16 Bora kurudiwa, Chelsea imepewa Lille huku Man. Utd ikipewa Atletico Madrid

- PSG itakutana na R. Madrid, Juventus vs Villarreal, Man. City vs Sporting CP na Liverpool vs Inter Milan

#JFSports
Fuatilia Mjadala huu unaoendelea hivi sasa ndani ya Clubhouse ya JamiiForums

Link - https://www.clubhouse.com/join/jamiiforums/YcIowdFT/xkaQ6BkE

#JamiiForums
Yanayojiri katika Mjadala kuhusu Magonjwa ya Kiharusi na Kupooza unaoendelea hivi sasa kupitia Clubhouse

Ungana nasi - https://www.clubhouse.com/join/jamiiforums/YcIowdFT/xkaQ6BkE

#JamiiForums #Stroke #Kiharusi
JF SCHEDULED MAINTENANCE

Kuanzia saa Sita Kamili hadi saa Nane Kamili usiku wa leo tovuti ya JamiiForums.com itakuwa haipatikani kufuatia maboresho yanayotarajiwa kufanyika wakati huo

Tunashukuru kwa kuendelea kutumia huduma zetu na asante kwa ushirikiano wako

#JamiiForums
MAREKANI: Wamarekani 40,000 wametapeliwa kupitia matangazo ya kujifanya Kampuni inatoa zawadi. Utapeli unaozidi kukua kwa miaka 3 iliyopita

Kwa miezi tisa ya mwanzo ya Mwaka 2021 jumla ya Dola milioni 148 sawa na Tsh. Bilioni 340.6 zimetapeliwa

Soma - https://jamii.app/UtapeliWaZawadi
ELON MUSK APINGA KULAZIMISHA WATU KUPATA CHANJO YA #COVID19

Mmiliki wa Kampuni ya #Tesla amesema kulazimisha Watu kupata Chanjo au kuwafukuza kazi si sahihi

Ametoa wito Watu washawishiwe kupata Chanjo badala ya kulazimishwa

Soma - https://jamii.app/ElonMusk

#UVIKO3
UFUATILIAJI WA USALAMA WA CHANJO ZA COVID-19 NI ENDELEVU

Shirika la Afya (WHO) limesema ufuatiliaji wa usalama ni muhimu kitaifa, kikanda na kimataifa

Mchakato unahusisha wadau na Wataalamu wa Afya ili kuhakikisha usalama kila mara

Soma - https://jamii.app/ChanjoUfuatiliaji

#UVIKO3
Kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake 3 inatarajiwa kuendelea leo

Mahakama inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu pingamizi la Mshtakiwa Mohammed Ling'wenya aliyepinga Mahakama kupokea kielelezo kinachodaiwa kuwa ni maelezo yake

Soma - https://jamii.app/UamuziPingamizi
SUDAN: Polisi wametumia Mabomu ya Machozi kutawanya Waandamanaji waliokusanyika karibu na Makazi ya Rais Jijini Khartoum

Tangu Mapinduzi kufanyika Nchini humo Oktoba 25, watu wapatao 50 wameripotiwa kupoteza maisha huku mamia wakijeruhiwa

Soma - https://jamii.app/KhartoumProtests

#JFLeo
GHANA: Mamlaka nchini Ghana zimetangaza kupiga faini Mashirika ya Ndege yatakayosafirisha Raia wa Kigeni ambao hawajapata chanjo

> Mashirika yatalipa Dola 3,500 (sawa na Tsh. Milioni 8) kwa kila msafiri asiyepata chanjo ya #COVID19

Soma https://jamii.app/WasichanjaGhana

#UVIKO3