JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UPDATE: Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi yatupilia mbali Hoja zote 7 za Utetezi ktk pingamizi la kuitaka Mahakama isipokee kielelezo chenye maelezo ya Mshtakiwa Mohammed Ling'wenya

Jaji Joachim Tiganga amepokea kielelezo

Soma https://jamii.app/UamuziPingamizi
MDAU: TABIA UNAZOTAKIWA KUACHA ILI KUTOKA ULIPO NA KUSONGA MBELE

1) Kujilinganisha na Wengine: Tabia hii ni mwizi wa furaha yako. Mtu pekee wa kujilinganisha naye ni wewe mwenyewe

2) Kurudia Makosa: Kukosea kupo katika maisha na hilo lipo wazi, ila jifunze kwa makosa kisha songa mbele

3) Kushindwa kusema Hapana: Kama unataka kuwa na maisha ya wasiwasi na yasiyo na furaha basi shindwa kusema Hapana

Soma - https://jamii.app/TabiaSOC

#StoriesOfChange
Baadhi ya Wawasilishaji na Wadau walioshiriki katika Warsha ya kujadili Mapendekezo ya Mabadiliko ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni (2020) ulioandaliwa na Jamii Forums kwa kushirikiana na CIPESA - Uganda

Warsha imefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Four Points by Sheraton (zamani New Africa Hotel) jijini Dar es Salaam leo

#JamiiForums
TUNISIA: SHUGHULI ZA BUNGE KUSITISHWA HADI UCHAGUZI UTAKAPOFANYIKA

Tangu aliposimamisha Bunge na kumfukuza aliyekuwa Waziri Mkuu, Rais Kais Saied ameendelea kushikilia Madaraka akisisitiza uamuzi huo ulihitajika kutokana na mwenendo mbaya wa Siasa

Soma - https://jamii.app/RaisKaisBunge
HALI YA UTEKELEZAJI WA MAPENDEKEZO YA CAG KWA OR - TAMISEMI

Ripoti ya Ukaguzi 2019/20 inaonesha kati ya Mapendekezo 15 yaliyotolewa na CAG 2018/19, Ofisi ya Rais – TAMISEMI haikutekeleza pendekezo lolote kikamilifu

Mapendekezo 6 yapo katika hatua mbalimbali za utekelezaji, Mapendekezo 5 hayajatekelezwa na Mapendekezo 4 yamejirudia

Soma - https://jamii.app/UtekelezajiMapendekezo

#JFUwajibikaji
BELARUS: KIONGOZI WA UPINZANI AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 18

Sergei Tikhanovsky amekutwa na hatia ya kuandaa machafuko na kuchochea chuki

Alipanga kugombea ktk Uchaguzi Mkuu 2020 dhidi ya Rais Lukashenko ambaye amekuwepo madarakani tangu 1994

Soma - https://jamii.app/KifungoMpinzani
Fainali ya Shindano la #MissWorld2021 iliyotarajiwa kufanyika Desemba 16, 2021 huko Puerto Rico imeahirishwa kwa siku 90 kutokana na #COVID19

Washiriki na Wafanyakazi wa Shindano wamewekwa karantini kabla ya kuruhusiwa warudi katika Nchi zao

Soma - https://jamii.app/SuspMissWorld
Shirika la Waandishi Habari Wasiokuwa na Mipaka (RSF) limesema kwa sasa kuna Waandishi wa Habari 488 waliofungwa jela Duniani kote

Idadi ya waliokamatwa imeongezeka kwa 20% kutokana na ukandamizaji Nchini #Myanmar, Belarus na Hong Kong

Soma https://jamii.app/488JournalistsJail
#PressFreedom
Kiongozi Mkuu wa ACT - Wazalendo, Zitto Kabwe ametangaza kukutwa Virusi vya Corona baada ya kupatwa na Mafua

Asema "Chanjo imesaidia kutopata madhara makubwa na nimejitenga ili kutoambukiza wengine"

Asisitiza Wananchi kuchukua tahadhari kwa kuvaa Barakoa na kujiepusha na mikusanyiko

Soma - https://jamii.app/ZittoCoronaPos
#UVIKO3
KOREA KASKAZINI: Serikali imepiga marufuku Wananchi kucheka, kunywa pombe na kufanya sherehe kwa Siku 11 wakiadhimisha Miaka 10 ya Kifo cha Kim Jong II

Kim Jong II alikuwa Rais Mwaka 1994 - 2011 na nafasi yake ilichukuliwa na Mwanae, Kim Jong Un

Soma - https://jamii.app/BanLaughing
AFYA: Wizara ya Afya imesema hali ya mafua inayowakumba watu wengi kwa sasa ni mafua ya kawaida ambayo hutokea kutokana na vipindi vya hali ya hewa

> Imetoa wito kwa wanaojisikia kuchoka, kikohozi na kifua kufika Vituo vya Afya kwa matibabu

Soma https://jamii.app/MafuaYaKawaida
FUATILIA TAARIFA ZA KIRUSI CHA OMICRON KUTOKA VYANZO SAHIHI

Jamii inashauriwa kupata taarifa za #CoronaVirus pamoja na Kirusi kipya kwa Wataalamu wa Afya na vyanzo vinavyoaminika

Usisambaze taarifa mpya mpaka ujiridhishe imethibitishwa

Soma - https://jamii.app/TaarifaChanjo

#UVIKO3
SUDAN: Waziri Mkuu wa Sudan, Abdalla Hamdok ametaka kuwepo Makubaliano ya Kisiasa ili kulinda Taifa hilo

Maandamano zaidi yamepangwa kufanyika leo kuadhimisha miaka mitatu ya maandamano yaliyopelekea Omar al-Bashir kupinduliwa

Soma - https://jamii.app/SudanHamdok
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi amewaasa Wazazi kutopeleka watoto maeneo ya mikusanyiko isiyo ya lazima ili kupunguza hatari ya kupata maambukizi ya #COVID19

> Abiria wametakiwa kuelimishwa hatari ya kujazana ktk mabasi

Soma https://jamii.app/Dec25UVIKO

#UVIKO3
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi amewaasa wanaosafiri kwenda vijijini kwa sherehe za mwisho wa mwaka kuwalinda wazee dhidi ya maambukizi ya #COVID19

> Amesema kwa sasa visa vya maambukizi vinaongezeka kwa kasi

Soma https://jamii.app/WazeeVijijini
#UVIKO3
DR-CONGO: Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Jeshi la Uganda yametangaza kufanikiwa kuharibu ngome muhimu za Waasi wa ADF zilizopo Jimbo la Kivu na Ituri huko Kaskazini mwa DRC

> Kampeni dhidi ya ADF ilianza Novemba 30

Soma https://jamii.app/UgandaDRCWaasi
#JFLeo