JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) linaongoza kikao cha kujadili uwezekano wa Kombe la Dunia kufanyika kila baada ya Miaka 2 badala ya 4 ya sasa

CAF inaunga mkono mabadiliko hayo, lakini Mashirikisho ya Soka Ulaya na Kusini mwa #America yanapinga

Soma - https://jamii.app/TimeWorldCup
#Sports
SERIKALI: 80% YA WATANZANIA WALIOUGUA COVID-19 HAWAKWENDA HOSPITALI

Wizara ya Afya kupitia Ofisi ya Mpango wa Taifa wa Chanjo imesema 5% ya waliougua walifikishwa ICU

> Bado mwamko wa Chanjo unasuasua hasa Mikoa ya Kanda ya Ziwa

Soma https://jamii.app/WatzHospCorona
#UVIKO3
Wizara ya Afya imekanusha taarifa za uwepo wa wimbi la 4 la #COVID19 na kusema kuwa ongezeko la maambukizi halimaanishi uwepo wa wimbi hilo

> Imesema uwepo wa Wimbi jipya ni pale ongezeko la maambukizi linapokuwa kwa kipindi cha siku 14-21

Soma https://jamii.app/TzOmicron
#UVIKO3
UFILIPINO: Idadi ya vifo kutokana na Kimbunga kikali kilichoipiga Nchi hiyo imeongezeka kufikia Watu 375

Watu wengine 56 bado hawajulikani walipo, takriban Watu 380,000 wameyakimbia makazi yao huku wengine 500 wakijeruhiwa

Soma - https://jamii.app/DeathsStormPhill
#Philippines
UINGEREZA: Kutokana na Mataifa mengi kuweka ulazima wa Cheti cha uthibitisho wa kuchanjwa imebainika Matapeli wanawarubuni Watu kupitia #Facebook ili kuwauzia Vyeti feki

Facebook imesema itaondoa ujumbe wowote utakaobainika kufanya hivyo

Soma - https://jamii.app/FakeCoronaCards
#UVIKO3
#OMICRON: Wizara ya Afya ya #India imerekodi maambukizi 200 ya Omicron na maambukizi 5,326 ya aina nyingine za Virusi vya #COVID19 kwa saa 24 zilizopita

Aidha, vifo vipya 453 vimeripotiwa na kufanya idadi ya vifo kufikia 478,007

Soma https://jamii.app/OmicronIndia
#UVIKO3
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), imebaini 42.1% ya Watu walio na Shinikizo la Damu ambalo huambatana na tatizo la kukoroma wako hatarini kukosa pumzi usingizini

Pia, Watu wanaougua Kisukari, wenye Mzio, Uzito uliopindukia na upana wa shingo uliokithiri, nao wamo hatarini kiafya kwa kukosa hewa usingizini

Soma - https://jamii.app/KoromaPumzi
#Afya
CHINA YAFUTA AKAUNTI ZA MITANDAO YA KIJAMII YA β€˜MALKIA WA MITANDAO’

Huang Wei mwenye wafuasi zaidi ya Milioni 110 afutiwa akaunti zake kwa tuhuma za kukwepa kodi

Anatuhumiwa kuuza vitu vya thamani ya takribani Tsh. Trilioni 3.07 bila kulipa kodi

Soma - https://jamii.app/MalkiaWaMitandao
UCHAGUZI WA LIBYA MASHAKANI. KAMATI ZA UCHAGUZI ZAVUNJWA SIKU 2 KABLA

Desemba 24, ni Siku ambayo Walibya kwa mara ya kwanza wangepata nafasi ya kuchagua Rais

Kuvunjwa Kamati hizo kunamaanisha uwezekano wa kufanyika Uchaguzi ni mdogo

Soma https://jamii.app/ElectionLibya

#ElectionLibya
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
GHANA: Wabunge wametwangana makonde #Bungeni baada ya kutokea ubishani wakati wa mjadala juu ya Sheria ya tozo ya Miamala ya Kidijitali

Ugomvi huo ulianza baada ya Mbunge wa Upinzani kumzuia Msaidizi wa Spika kunyanyuka kwenda kupiga kura

Soma - https://jamii.app/TozoGhanaMPs
#JFLeo
UMOJA WA ULAYA WAPITISHA SHERIA MPYA ZA USAFIRI

Cheti cha #COVID19 cha Umoja huo ni halali kutumika kwa Wasafiri kwa miezi tisa baada ya kukamilika kwa Chanjo

Sheria hizo mpya zitaanza kutumika katika Mataifa 27 ya Wanachama kuanzia Februari 1. Mataifa yatalazimika kuruhusu Wasafiri waliopata Chanjo kamili kuingia katika maeneo yao

Soma - https://jamii.app/EUWasafiri
#UVIKO3
πŸ‘1
UGANDA: WABUNGE 38 WALIOKUWA ARUSHA WAKUTWA NA CORONA

Safari ya Wabunge zaidi ya 200 na Wafanyakazi 125 imeingia doa baada ya kurudi kutoka kwenye mashindano ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jijini Arusha na kukutwa na #COVID19

Soma - https://jamii.app/MPUGCoronaAR

#UVIKO3
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekipiga faini ya Tsh. milioni 2 Kituo cha Televisheni cha Wasafi kwa kosa la kurusha maudhui yaliyokashifu imani ya Kikristo

Pia, wametakiwa kuomba radhi watazamaji kuanzia Desemba 23 hadi 25 mara tatu kwa siku kila baada ya saa nne kwa kosa hilo

Soma - https://jamii.app/WasafiFainiTCRA
#JFLeo
SERIKALI YAILIPA PSSSF TSH. TRILIONI 2.17

Serikali imeanza kulipa madeni kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ili Wastaafu wasisumbuke kupata stahiki zao

Deni lililobaki litaendelea kulipwa kwa mfumo wa Hati Fungani

Soma - https://jamii.app/DeniPSSSF

#JFLeo
Kikao cha 18 cha Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kimekubali Mchakato wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwa Mwanachama

Baraza la Mawaziri EAC laagizwa kuanza mazungumzo na DR Congo kwa ajili ya kujiunga na Jumuiya hiyo

Soma - https://jamii.app/DRCEAC

#JFLeo
LIBYA: UCHAGUZI WA RAIS KUTOFANYIKA DESEMBA 24, 2021

Kamati ya Bunge la Libya imesema haitawezekana kuandaa Uchaguzi wa Rais kama ilivyopangwa

Haijafafanuliwa kama tarehe nyingine imepangwa, au ikiwa Uchaguzi huo umefutwa kabisa

Soma - https://jamii.app/NoElectionLibya
#LibyaElection
#SYRIA: Shirika la Haki za Binadamu Nchini humo limesema machafuko yalisababisha vifo vya Watu 3,746 Mwaka 2021 huku 360 wakiwa ni Watoto

Idadi hiyo ya vifo ndiyo ya chini zaidi kuwahi kurekodiwa katika vita hivyo vya muongo mmoja

Soma - https://jamii.app/DeathsSyria21
#HumanRights
KENYA: MWANAFUNZI AFARIKI KWENYE SHINDANO LA KULA BOFLO NA SODA

Sherehe za kumpata mshindi wa kula Mkate wa Boflo na kunywa soda zimegeuka kuwa simanzi, baada ya Harrison Oduor Ouma kunyongwa na mlo huo

Wanafunzi walikuwa wakishiriki mashindano hayo siku ya mwisho kabla ya kwenda likizo ya Mwaka Mpya

Soma - https://jamii.app/KifoBofloKE
#JFLeo
ASKARI ALIYEKATAA RUSHWA YA TSH. MILIONI 10 ASHUSHWA CHEO

Askari Meshack Samson aliyepandishwa kutoka Sajenti kuwa Stesheni Sajenti mwaka 2019 ameshushwa cheo kwa utovu wa nidhamu

Polisi yasema alikataa kusoma kozi ya kuendana na cheo kipya

Soma - https://jamii.app/UtovuNidhamu
NDEGE KUTOKA TANZANIA KUTORUHUSIWA UAE KUANZIA DESEMBA 25

Mamlaka ya Udhibiti wa Majanga ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) imechukua hatua hiyo kufuatia ongezeko la Visa vya #Omicron

Nchi nyingine zilizozuiwa ni Kenya, Ethiopia na Nigeria

Soma - https://jamii.app/NdegeTzUAE

#UVIKO3