JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MDAU: KUFANYA MAKOSA NI JAMBO LA MUHIMU KWA BINADAMU

Anasema Watu wengi hawana Maendeleo binafsi hususani Kiuchumi kwa kuwa wanaogopa kukosea na kuendelea kufanya mambo yale yale

Kufanya makosa humsaidia Mtu kujitambua, kugundua kipaji chake, kuleta ugunduzi, kutatua changamoto za Maisha, kuleta Mawazo mbadala pamoja na kuboresha Afya ya Ubongo na Akili

Msome - https://jamii.app/FaidaMakosa

#StoriesOfChange
MGAWANYO WA MAJUKUMU KATI YA MUME NA MKE NDANI YA NDOA

Kifungu cha 63 cha Sheria ya Ndoa kinaweka wajibu kwa Mume kumtunza Mke wake kwa kumpa mahitaji yote muhimu kama Mavazi, Chakula na Malazi kulingana na uwezo wake

Mke pia atakuwa na jukumu hilo tu ikiwa Mume hawezi kutunza Familia kwasababu za ugonjwa hasa wa Kiakili na Ulemavu.

#JamiiForums #16DaysOfActivism
Desemba 10 kila mwaka ni Maadhimisho ya Siku ya #HakiZaBinadamu

Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres amesema vitisho vipya vimeibuka kwa Haki za Msingi za Binadamu. Mamilioni ya Watoto wanakosa Haki yao ya kupata Elimu. Ukosefu wa Usawa nao unaongezeka

#HumanRightsDay
IKULU, DAR: Tanzania na Kenya zimekubaliana masuala mbalimbali ikiwemo kuimarisha Mpaka, kushirikiana kupambana na COVID-19 na kushirikiana kwenye Sekta ya Utalii

Rais Samia ameeleza hayo baada ya Utiaji Saini wa Hati za Makubaliano na Ushirikiano

Soma -https://jamii.app/TZKEMakubaliano
Upungufu wa Miundombinu ya Shule huathiri ufanisi wa utoaji #Elimu kwa Shule za Sekondari hasa kwa Wanafunzi wa Jinsia ya Kike

Ili kutatua changamoto za upungufu wa Miundombinu zilizoibuliwa na CAG, Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI zinashauriwa kutoa kipaumbele zaidi kwenye upangaji na utoaji wa Bajeti ya Miundombinu

Soma - https://jamii.app/MiundombinuShule

#JFUwajibikaji
MAKABIDHIANO YA VYUMBA VYA MADARASA KUFANYIKA DESEMBA 31

Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu ameongeza siku 15 kwa Halmashauri zote kukamilisha Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa

Madarasa yatakabidhiwa Desemba 31, 2021 badala ya Desemba 15 ya awali

Soma - https://jamii.app/MadarasaDec31
KENYA: ATOWEKA BAADA YA KUTUMIA PESA YA BOSI WAKE 'KUBET'

Robert M'munoru (20) kutoka Kaunti ya Lamu hajulikani alipo hadi sasa baada ya kutumia pesa za Bosi wake takriban Tsh. Milioni 3.8 kuchezea mchezo wa bahati nasibu na zikaliwa

Robert ambaye ametoweka tangu November 28, 2021 ameacha ujumbe Dukani kwa Bosi wake na alikwenda Kituo cha Polisi kukiri kutumia Fedha hizo na kuomba Bosi apewe shamba lake lililopo Meru kama fidia

Soma - https://jamii.app/FedhaBosiBet
GHANA YAPIGA MARUFUKU WASAFIRI WASIOPATA CHANJO

Raia walio nje watatakiwa kupata Chanjo watakapotua. Raia wanaosafiri nje ya nchi lazima wachanjwe

Mamlaka zimechukua hatua hiyo kutokana na wasiwasi maambukizi yataongezeka wakati wa sikukuu

Soma - https://jamii.app/ChanjoGhana

#UVIKO3
KENYA: RAILA ODINGA ATANGAZA KUWANIA NAFASI YA URAIS UCHAGUZI 2022

Kiongozi wa ODM ameahidi Serikali yake itatenga Ksh. bilioni 2 za kuwapa Vijana kila Mwaka

Pia, kila Mkenya atakuwa na Bima ya Afya huku Serikali ikiwalipia wasiojiweza

Soma - https://jamii.app/OdingaPres2022

#Democracy
KARIAKOO DERBY: SIMBA NA YANGA KUVAANA KWA MKAPA

Watani wa jadi katika soka la Tanzania, Klabu za Simba na Yanga zitapimana ubavu leo katika mchezo wa Ligi ya NBC utakaochezwa majira ya saa 11:00 jioni

Yanga inaongoza Ligi ikiwa na alama 19 huku Simba ikiwa na alama 17 katika nafasi ya pili na timu zote zikiwa zimecheza michezo 7

Je, Simba itafanikiwa kuishusha Yanga kileleni?

#JamiiForums #KariakooDerby
UJERUMANI: Bunge limepiga kura kuifanya Chanjo dhidi ya Virusi vya Corona kuwa sharti la kisheria kwa Wafanyakazi wa Sekta ya Afya kuanzia Machi 2022

Wafanyakazi wa Hospitali na ktk Vituo vya Wazee watalazimika kuthibitisha wamepata Chanjo

Soma - https://jamii.app/VaccHealthStaffGerm
#UVIKO3
POLEPOLE: NIMEPATA MASHTAKA YA KURUSHA MAUDHUI YANAYOPOTOSHA KUHUSU CORONA

Asema amepokea Mashtaka yanayosema kupitia Kipindi chake cha Shule ya Uongozi, amerusha Maudhui yanayoweza kuchochea Watanzania kuweza kugomea Kampeni ya Kitaifa ya #COVID19

Soma https://jamii.app/MashtakaPolepole

#JFLeo
SIMBA NA YANGA ZATOSHANA NGUVU KWA MKAPA

- Klabu za Simba na Yanga zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya goli 0-0 katika mchezo wa Ligi ya NBC

- Yanga inaendelea kuwa kileleni mwa Ligi ikifikisha alama 20 na Simba inabaki katika nafasi ya 2 ikiwa na alama 18

#JFSports
BENIN: Mahakama imemhukumu mmoja wa Wapinzani wakuu wa Rais Patrice Talon, Reckya Madougou, kifungo cha miaka 20 jela kwa kuhusika katika vitendo vya ugaidi

Hukumu yake imekuja siku chache baada ya Mpinzani mwingine kuhukumiwa miaka 10 gerezani

Soma - https://jamii.app/ReckyaBenin
MAREKANI: 70 WAPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA KIMBUNGA

Gavana wa Jimbo la #Kentucky amesema idadi ya vifo inaweza kuzidi 100 kwa rekodi za Majimbo mengine

Kimeharibu Kiwanda cha Mishumaa, eneo la Kampuni ya #Amazon na nyumba ya wazee ya Arkansas

Soma https://jamii.app/TornadoDeathUS
#JFLeo
DAR: Rais Samia Suluhu Hassan amesema Polisi wanapokamata watu hawatakiwi kufanya vitisho, lakini hali inayoonekana Mitaani ni ya vitisho na kutia hofu

Asema, "Wakati mwingine mtu anakamatwa bila kosa la maana. Zipo tuhuma za Rushwa zinasemwa"

Soma - https://jamii.app/RaisSamiaPolisi
AUSTRIA: Watu waliopata chanjo wataruhusiwa kuingia kumbi za sinema na burudani na maeneo mengine ya umma

> Wasiopata chanjo hawataruhusiwa kutoka nje na kujumuika na wenzao ila kwasababu za msingi kama kununua chakula na kumuona daktari

Soma https://jamii.app/AustriaCOVID19
#UVIKO3
Kiharusi ni hali inayotokea pale mishipa inayosambaza Damu kwenye Ubongo inapopatwa na misukosuko kiasi cha kushindwa kupeleka Damu kwenye Ubongo na hivyo kuathiri ufanyaji kazi wake

Unafahamu vitu vinavyoweza kukuweka katika hatari ya kupata Kiharusi? Je, ni kwa kiasi gani mwenendo wako wa maisha unaweza kupelekea kupata Kiharusi?

Kufahamu mengi zaidi, Ungana nasi katika Mjadala na Wataalamu utakaofanyika kupitia Clubhouse leo Desemba 13, 2021

Link - https://www.clubhouse.com/join/jamiiforums/YcIowdFT/xkaQ6BkE
AFRIKA KUSINI: Rais Cyril Ramaphosa amepima na kukutwa na #COVID19. Anaendelea na matibabu na majukumu ameyaacha kwa Naibu Rais, David Mabuza

> Alianza kuonesha dalili baada ya kutoka kwenye ibada ya Kumbukumbu ya Rais FW Klerk

Soma https://jamii.app/RamaphosaMaambukizi

#UVIKO3
Mshiriki wa #StoriesOfChange amesema Wahalifu wa Mtandaoni huweza kupata taarifa kwa kushika kifaa cha Mtu au kutumia programu maalumu

Ameshauri kupakua programu ktk masoko yanayoaminika. Pia, Usinunue Simu au Kompyuta iliyotumika

Soma - https://jamii.app/CyberCriminals

#DigitalSecurity