JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Serikali imeshauriwa iendelee kutenga fedha kwa ajili ya kulipa malimbikizo ya madai ya Watumishi na hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa Halmashauri zilizoshindwa kupeleka Makato ya Mishahara ya Watumishi katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii

> Hii ni kwa mujibu wa Taasisi ya Wajibu ktk uchambuzi wa Ripoti ya CAG 2019/20

Soma - https://jamii.app/MikopoMishahara
#JFUwajibikaji
CHANGAMOTO ZINAZOMKABILI MTOTO NJITI

Mtoto njiti anaweza kuwa na changamoto ya kupumua hivyo punde tu baada ya kuzaliwa, anatakiwa kupatiwa huduma ya kwanza

Hawezi kuhimili baridi hivyo lazima azaliwe kwenye chumba chenye joto la kutosha

Wana hatari kubwa ya kupata maambukizi kwasababu kinga yao ya mwili haijakomaa

Soma - https://jamii.app/WatotoNjiti

#WorldPrematurityDay
Namna bora ya kuzuia na kukomesha Unyanyasaji na Ukatili dhidi ya Watoto ni lazima jambo hilo liwe jukumu la Jamii nzima na sio Mzazi mmoja mmoja

Mshiriki wa 'Stories Of Change' anasema jukumu la makuzi ya Watoto limeachwa kwa Wazazi tu na endapo Mtu mwingine akishuhudia Mtoto anapitia Ukatili wengi huwa hawafanyi chochote

Msome - https://jamii.app/UkatiliWattJamii

#UkatiliWatoto
CHILE: RAIS PINERA ANUSURIKA KUONDOLEWA MADARAKANI

Wajumbe wa Baraza la Senate waliopiga kura ni 24, idadi ambayo ni chini ya kura 29 zinazohitajika huku waliopinga wakiwa 18

Endapo mchakato ungefaulu, angekabiliwa na kifungo cha hadi miaka 5

Soma - https://jamii.app/RaisChileAnusurika
Katika ukusanyaji wa Mapato ya Serikali Kuu, CAG alibaini;

a) Kupotea kwa kodi ya Tsh. Bilioni 12.14 ya Mafuta lita milioni 16.55 yaliyoingizwa Nchini kama Mafuta ambayo yalikuwa yanakwenda Nchi jirani lakini hayakutoka nje ya Nchi

b) Kutokusanywa kwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya Tsh. bilioni 8.90 kutokana na Wafanyabiashara kushusha thamani ya Mauzo katika ripoti zao za Mwezi

Soma - https://jamii.app/MapatoSerikaliKuu

#JFUwajibikaji
Taarifa binafsi ni taarifa yoyote inayokutambulisha, iwe inahusiana na Maisha yako binafsi, Kitaaluma, au ya umma (Mfano: Majina, Namba za Simu, Anwani n.k)

Ni mara ngapi umeshakutana na taarifa za Watu wengine katika Mazingira ambayo hukupaswa kukutana nazo? Kama ni mara nyingi, basi huenda hata taarifa zako zinazagaa bila wewe kujua

Ungana nasi katika Mjadala wa Haki ya faragha na ulinzi wa taarifa binafsi kupitia Clubhouse ya JamiiForums Novemba 18, 2021

#JamiiForums #dataprivacy
SUDAN: Laini za Simu zimedaiwa kufungwa kabla ya Maandamano yaliyopangwa kufanyika katika Mji Mkuu wa Nchi hiyo, Khartoum kupinga Utawala wa Kijeshi

Huduma za Intaneti zimeendelea kuminywa tangu Oktoba 25 licha ya kuwepo maagizo ya kuzirejesha

Soma - https://jamii.app/LainiSimuSdn
UJERUMANI: Kansela Angela Merkel asema Nchi hiyo inapambana na Wimbi la Nne la #COVID19. Visa vipya 52,826 vimerekodiwa saa 24 zilizopita

Mawaziri wa Majimbo yote 16 wanatarajiwa kukutana na kujadili namna ya kupambana na Maambukizi

Soma - https://jamii.app/UVIKOUjerumani

#UVIKO3
Taarifa binafsi ni taarifa yoyote inayokutambulisha, iwe inahusiana na Maisha yako binafsi, Kitaaluma, au ya umma (Mfano: Majina, Namba za Simu, Anwani n.k)

Ni mara ngapi umeshakutana na taarifa za Watu wengine katika Mazingira ambayo hukupaswa kukutana nazo? Kama ni mara nyingi, basi huenda hata taarifa zako zinazagaa bila wewe kujua

Ungana nasi katika Mjadala wa Haki ya faragha na ulinzi wa taarifa binafsi kupitia Clubhouse ya JamiiForums Novemba 18, 2021

#JamiiForums #dataprivacy
#SUDAN: Vikosi vya Usalama vimewaua Waandamanaji 15 na kufanya idadi ya waliouawa tangu kuzuka wimbi la kupinga Utawala wa Kijeshi kufikia 39

Wengi wa waliopoteza maisha wana majeraha ya risasi kwenye shingo au viungo vingine vya mwili

Soma - https://jamii.app/SudanDeathsProtest
#Democracy
DALILI ZINAZOASHIRIA MAGONJWA YA AFYA YA AKILI

1. Kimwili: Mwili kukosa Nguvu, kukosa usingizi au kulala kupita kiasi. Kukosa hamu ya kula, kutokutulia (kuhamanika) au kujitenga

2. Kiakili: Kukosa umakini wa shughuli za kila siku. Kusahau haraka au kupoteza kumbukumbu. Kukosa uwezo wa kupambanua mambo. Kusikia sauti ambazo hazipo na kuona vitu ambavyo havipo

3. Kihisia: Huzuni na wasiwasi au woga kupita kiasi. Hasira za haraka hata kupiga wengine. Msongo wa Mawazo, kujitenga na Watu, kutokujijali kiusafi na kujaribu kujiua

Soma zaidi - https://jamii.app/SignsMentalDisorder
#MentalHealthMatters
MAPUNGUFU KATIKA USIMAMIZI WA MALI ZA MAMLAKA YA SERIKALI ZA MITAA

Kutokuwepo Hati za Umiliki wa Ardhi zenye thamani ya Tsh. Trilioni 1.14 katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa 27 kutokana na uzembe wa Menejimenti za Halmashauri husika kutopima Ardhi zinazozimiliki

Kutokuwekwa Namba za Utambulisho na kutohifadhiwa vyema kwa mali za kudumu zenye thamani ya Tsh. Bilioni 2.81 zilizonunuliwa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa 18

Soma - https://jamii.app/MapungufuMali

#JFUwajibikaji
MDAU: MFUMO WA ELIMU UHUSISHE MASUALA YA AFYA YA AKILI

Watoto hutumia muda mwingi Shule, na katika kuhakikisha wanafikia kiwango stahiki cha uwezo wao ni muhimu kuhusisha msaada madhubuti katika Afya yao ya Akili

Mdau anapendekeza uhusishwaji wa Afya ya Akili ktk Mfumo wa Elimu za Msingi na Sekondari kwasababu Shule huchangia katika ukuaji wa Mtoto

Soma - https://jamii.app/AfyaAkiliElimu

#MentalHealth #StoriesOfChange
Rais Samia amesema anatambua Miji mingi mikubwa inakabiliwa na uhaba wa maji unaopelekea Mgao wa Maji na Upungufu wa Umeme

Asema, "Bado kuna Wananchi wengi wameendelea kuvamia vyanzo vya maji kwa kuyachepusha kwa ajili ya matumizi mengine"

Soma - https://jamii.app/MajiUmeme

#JFLeo
Rais Samia ameagiza Wakuu wa Mikoa na Kamati za Ulinzi kuhakikisha Ulinzi unawekwa kwenye Vyanzo vyote vikuu vya Maji

Asema, "Hatuwezi kuweka rehani maisha ya Watanzania wengi kwa faida ya wachache. Wanaochepusha Vyanzo vya Maji ni watu wachache"

Soma - https://jamii.app/VyanzoMajiUlinzi
MWANZA: Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesisitiza umuhimu Tafiti kujikita zaidi katika kubaini kwanini Kanda ya Ziwa inaongoza kwa Waathirika wa Saratani

Imeelezwa, Wanawake ni wahanga wakubwa wakikumbwa na Saratani za Kizazi na Matiti

Soma - https://jamii.app/SarataniKandaZiwa
KENYA: RAIS KENYATTA ASAINI SHERIA YA KUZUIA 'MICHEPUKO' KUPATA MIRATHI

Rais Uhuru Kenyatta ametia saini Miswada 3 ukiwemo Muswada unaozuia Wanawake ambao hawapo ktk Ndoa kupata mirathi Wapenzi wao wanapofariki

Mirathi itatolewa kwa Wanafamilia tu

Soma - https://jamii.app/SuccessionBillKE
CHANJO ZA COVID-19 HAZIATHIRI NGUVU ZA KIUME

Ripoti iliyotolewa na Taasisi inayojihusisha na Uandishi wa Makala za Afya Marekani (JAMA) inasema Chanjo haiingilii Mfumo wa Uzazi wa Mwanaume, bali hujenga Mfumo wa Kingamwili

Soma - https://jamii.app/ChanjoNguvuKiume

#UVIKO3 #CoronaVirus
Katiba husaidia kuipatia Nchi dira na maono ya wapi wanatoka na wapi wanakwenda. Pia, huwakumbusha Viongozi wajibu wao ili wasivuke mipaka ya utendaji wao

Mshiriki wa 'Stories Of Change' anasema Nchi zilizopiga hatua katika Utawala Bora na Uwajibikaji sio kwamba Wananchi wake wana akili sana bali ni mfumo mzuri wa Katiba walizonazo

Soma - https://jamii.app/KatibaUtawalaBora
#Democracy #Accountability
Ni mara ngapi umeshakutana na taarifa za wengine ktk Mazingira ambayo hukupaswa kukutana nazo? Kama ni mara nyingi, basi huenda hata taarifa zako zinazagaa bila wewe kujua

Ungana nasi katika Mjadala huu kupitia Clubhouse ya JamiiForums

Link - https://www.clubhouse.com/join/jamiiforums/2gXFqw3K/MzaY4W7B

#JamiiForums #DataPrivacy