JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
WADAU: SHULE ZA β€˜ENGLISH MEDIUM’ ZIMEFANYA WAZAZI KUWA WALIMU

> Wazazi ndani ya JamiiForums wanajadili kuhusu 'Homeworks' wanazopewa watoto toka shuleni. Baadhi wanaona ni vyema mzazi kushiriki kazi za mtoto ili kujua maendeleo yake huku wengine wakiona kama wanapewa kazi ya kufundisha watoto ilhali wamelipa ada

> Je, una maoni gani kuhusu hili?

Soma https://jamii.app/ShuleEnglishMedium
SUDAN KUSINI: RAIS ATANGAZA BUNGE JIPYA

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir ameunda Bunge jipya ambalo lina Wabunge kama Makubaliano ya Septemba 2018 yalivyotaka

> Wabunge waliotangazwa wanajumuisha Wabunge 128 kutoka kundi la waasi wa zamani, SPLM-IO

Soma https://jamii.app/SudanKusiniBunge
NAMNA YA KUMJENGEA MTOTO TABIA YA UMAKINI KATIKA UTENDAJI WAKE

> Jaribu kutengenezea mazingira yenye utulivu ili aweze kuzingatia kazi aliyopewa. Televisheni, Muziki, Kelele na Simu za Rununu ni vizuizi vikubwa kwa Mtoto kuwa makini

> Mtafutie Michezo itakayomsaidia kuboresha kiwango chake cha umakini. Michezo kama Puzzles husaidia kuchemsha Ubongo wa Mtoto

Soma - https://jamii.app/FocusChildren
#Malezi #JFLeo
MBUNGE: WANAUME WANAJADILI SANA KUHUSU SIMBA NA YANGA KULIKO AFYA ZAO

Mbunge Viti Maalum (CCM), Hawa Mchafu, amesema kama nguvu zaidi ingetumika kujadili masuala ya #Afya ikiwemo kupima VVU, huenda vita dhidi ya ugonjwa huo ingekuwa nyepesi

Soma - https://jamii.app/WanaumeAfya
#JFLeo
RAIS ATEUA MAJAJI WA MAHAKAMA YA RUFANI NA MAHAKAMA KUU

Rais Samia Suluhu ameteua Majaji 7 wa Mahakama ya Rufani na 21 wa Mahakama Kuu akiwemo Biswalo Mganga aliyekuwa DPP

Amemuongezea miaka 2 Jaji Sivangilwa Mwangesi wa Mahakama ya Rufani

Soma https://jamii.app/TeuziMajaji
GWAJIMA: SIPINGI CHANJO LAKINI TAIFA LISIWE SEHEMU YA MAJARIBIO

Mbunge wa Kawe asema "Miaka ijayo tunaweza kuwa na Taifa lisilo na Watu wanaofikiri vizuri na kufanya maamuzi. Ni ujinga kuruhusu Taifa zima kuwa majaribio eti kwasababu tuna haraka”

Soma - https://jamii.app/GwajimaChanjo
DAR: VIBANDA KATIKATI YA JIJI KUONDOLEWA KABLA YA MEI 18

Jumanne Shauri (Mkurugenzi) amesema hawajazuia Wafanyabiashara bali wanatakiwa watumie meza ili wakimaliza waziondoe na kuacha maeneo wazi

> Sheria ya Mipango Miji hairuhusu kujenga vibanda

Soma https://jamii.app/VibandaJijiniDsm
#JFLeo
NDEGE ZA #SOMALIA ZAPIGWA MARUFUKU KUINGIA ANGA LA KENYA

Mamlaka ya Anga imesema ndege za dharura za kitabibu na walio na ujumbe wa masuala ya kibinadamu ya UN zitaruhusiwa kuingia

> #Kenya na Somalia zimekuwa na mzozo wa Mpaka tangu 2014

Soma https://jamii.app/NdegeSomaliaKenya
#JFLeo
WHO: MTU 1 KATI YA 500 ANAWEZA KUPATA CHANJO KWA NCHI ZINAZOENDELEA

Shirika la Afya Duniani limesema hali ilivyo kwa Nchi zinazoendelea ni tofauti ikilinganishwa na Nchi zilizoendelea, ambapo mtu 1 kati ya 4 amepata Chanjo ya Ugonjwa wa #COVID19

Soma > https://jamii.app/ChanjoUpatikanaji
SIMIYU: MUME AUA MKEWE KISHA NAYE KUJINYONGA KUTOKANA NA WIVU WA MAPENZI

Edward Manyangu(41) Mkazi wa Busega anadaiwa kumuua Dalali Maunga(41) kwa kumpiga na kitu kizito kichwani akimtuhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mwanaume mwingine

Soma - https://jamii.app/VifoNdoaBusega
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
WALIMU KUWA NA ARI KAMA MWALIMU YUSUPH KUNAWEZA KUONGEZA UELEWA WA WANAFUNZI?

Mwalimu Yusuph Mohamed Yusuph ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Ikorongo Mkoani Mara anayeonekana akifundisha kwa kutumia mbinu nyingi za kuwaburudisha Watoto

Je, ari na ubunifu alionao unaweza kuongeza thamani katika Uelewa wa Wanafunzi wanaofundishwa?

#JamiiForums #Elimu