JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ARUSHA: BAADHI YA MALI ZA NGURDOTO MOUNTAIN LODGE ZAUZWA KULIPA MADAI YA MISHAHARA

> Watu 93 waliokuwa Wafanyakazi walifungua kesi wakidai Tsh. Milioni 129 za malimbikizo ya mishahara

> Mahakama itatoa amri Mei 4, 2021 kuhusu mali hizo

Soma https://jamii.app/HoteliArusha
INDIA YAREKODI MAAMBUKIZI MAPYA 300,000 KWA SIKU 6 MFULULIZO

- Ndani ya saa 24 zilizopita, visa 323,144 vya #COVID19 vimerekodiwa na maambukizi yamefikia Milioni 17.64

- Vifo 2771 vimerekodiwa lakini Wataalamu wanaamini idadi halisi ni kubwa zaidi

Soma https://jamii.app/VisaCOVIDIndia
KIKWETE: SITARAJII KOFIA YA UENYEKITI WA CHAMA KUTOFAUTISHWA NA URAIS

> Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, amesema Rais wa #Tanzania huwa Mwenyekiti wa CCM Taifa ili kuepuka migongano ambayo inaweza kujitokeza ikiwa Mwenyekiti na Rais watatofautiana

Soma - https://jamii.app/UenyekitiCCM
#NIGERIA: WANAMGAMBO WAVAMIA KAMBI NA KUUA WANAJESHI 33

> Wanajeshi wa kambi ya #Mainok ktk Jimbo la Borno wameuawa na wapiganaji wa Dola ya Kiislamu (IS)

> Wapiganaji walifika kambini hapo na nguo za Jeshi na Magari 16 na kuiteka kambi

Soma - https://jamii.app/NigeriaIS
LIGI KUU KUENDELEA KUTIMUA VUMBI LEO

- Baada ya kushinda michezo 4 mfululizo, Simba leo inashuka dimbani kukipiga dhidi ya Dodoma Jiji majira ya saa 1:00 usiku

- Mchezo mwingine utakaopigwa leo ni kati ya Gwambina dhidi ya Mwadui majira ya saa 10:00 jioni

#JamiiForums #Sports
CCM-DODOMA: KATIBA ILIYOPO INAFAA, HAKUNA ULAZIMA WA KUICHOKONOA

- Halmashauri Kuu ya CCM Dodoma imesema #Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 bado inafaa

- Imesema Katiba imewezesha kufanyika mabadiliko ya Uongozi wa juu bila mgogoro

Soma https://jamii.app/CCMKatibaMpya
JULIAN NAGELSMANN KUWA KOCHA WA BAYERN MUNICH

- Bayern imemtangaza Nagelsmann (33) kuwa Kocha wao kuanzia Julai 1, 2021 baada ya kuilipa Leipzig £ milioni 21.7

- Kocha huyo wa Leipzig ana uwiano wa ushindi wa 58% akiwa na timu hiyo kwa miaka 2, ameshinda mechi 53/90

#JFLeo
MAENEO YA KAMBI KUREJESHWA SERIKALINI BAADA YA WAKIMBIZI KUONDOKA

- Naibu Waziri Mambo ya Ndani amesema maeneo yote ya kambi yatarejeshwa Serikalini ili yapangiwe matumizi

- Pia hakuna mgogoro wa Ardhi baina ya Kambi ya Nyarugusu na Kata ya Makere

Soma https://jamii.app/KambiWakimbizi
UNAUMIZWA NA MAMBO YALIYOPITA? FANYA YAFUATAYO (SEHEMU 1)

- Jifunze kusamehe na kusahau, kutokuwa tayari kusamehe kutakufanya uendelee kuumizwa na mambo yaliyopita na kushindwa kuendelea na maisha yako

- Jiruhusu kusikia maumivu, linapokukuta jambo la kuumiza kama kufiwa ni vyema ukaruhusu maumivu kwa wakati ule ili yaishe kutofanya hivyo kutasababisha uumie kwa muda mrefu zaidi

#JamiiForums #Msongo
UNAUMIZWA NA MAMBO YALIYOPITA? FANYA YAFUATAYO (SEHEMU 2)

- Kubaliana na hali halisi acha kutamani mambo yawe kama yalivyokuwa awali

- Usijilaumu sana unapofanya makosa, tumia hiyo kama nafasi ya kujifunza

#JamiiForums #Msongo
BULAYA: FIDIA YA WANAOHARIBIWA MALI NA WANYAMAPORI NI NDOGO. KUNA DOUBLE STANDARD

- Amesema kumekuwa na 'Double Standard' ambapo mifugo inapoingia hifadhini fidia kubwa hotozwa lakini wanyamapori wanapoharibu mali za wananchi fidia yake ni kidogo

Soma > https://jamii.app/BulayaBungeni
UCL: REAL MADRID KUKABILIANA NA CHELSEA NUSU FAINALI

- Real Madrid itakuwa nyumbani kuialika Chelsea katika dimba la Estadio Alfredo Di Stefano, majira ya saa 4:00 usiku

- Katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya timu hizo zimekutana mara 3, Chelsea imeshinda michezo 2 na kutoka sare mchezo mmoja

#JamiiForums #JFSports
MAANDAMANO YA KUPINGA UTAWALA WA JESHI YAIBUKA CHAD

- Waandamanaji wanataka Utawala wa Kiraia kurejeshwa kufuatia kifo cha Rais Deby

- Baadhi ya Wapinzani wameita kitendo cha Jeshi kuchukua madaraka kuwa Mapinduzi na kuwataka Wananchi kuandamana

Soma > https://jamii.app/ChadProtests
MBEYA: MIILI NA KICHWA VYAOKOTWA KWENYE HIFADHI

> Polisi Wilayani Mbarali wamethibitisha kuokota miili miwili na kichwa ktk Hifadhi ya Taifa ya Ruaha

> Aidha, imetaarifiwa kuna Familia zinadai ndugu zao wanne kutoonekana kwa siku kadhaa

Soma - https://jamii.app/MiiliVichwaRuaha
NDUGAI AHOJI KWANINI FEDHA ZINAKWAMA WIZARANI

- Spika wa Bunge, Job Ndugai amehoji kwanini Fedha zinazokuja kwa ajili ya Mazingira zinakwama Wizara ya Fedha

- Amtaka Waziri kujiandaa akisema, "Siku ya Wizara yake nitakamata Shilingi mimi mwenyewe"

Soma https://jamii.app/SpikaWizaraFedha
VPL: SIMBA YAENDELEA KUJIKITA KILELENI MWA MSIMAMO WA LIGI

- Simba imeendelea kujitengenezea nafasi nzuri kileleni mwa Msimamo wa Ligi Kuu baada ya kuitandika Dodoma Jiji goli 3-1

- Magoli ya Simba yamefungwa na C. Mugalu 8' 68', L. Miquissone 56' huku goli la Dodoma Jiji likifungwa na C. Mkangala 29'

- Kwa matokeo hayo Simba inafikisha alama 61 ikiwa ni alama 4 juu ya Yanga inayoshika nafasi ya pili kwa alama 57

#JamiiForums #JFSports