JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
NJOMBE: WANAWAKE WASIOLIPA MCHANGO WA UJENZI WADAIWA KUFUNGIWA KWA SAA 9

> Uongozi wa Kijiji cha Luduga wilayani Wanging'ombe umekiri kuwakamata wasiolipa mchango wa ujenzi wa Sekondari, lakini wamesema hawajafungiwa wakiwa na watoto

Soma - https://jamii.app/MchangoSekondari
MAREKANI YATOA TAHADHARI KWA RAIA WAKE KUHUSU KIMBUNGA JOBO

- Ubalozi wa Marekani jijini Dar umewataka Wananchi kusalia nyumbani na kutosafiri

- Mashirika ya Hali ya Hewa yanatabiri Kimbunga hicho kuwa kikubwa zaidi kwa Tanzania tangu 1952

Soma - https://jamii.app/USCycloneJobo
LISSU: KESI ZINAZONIKABILI ZIANGALIWE KWA JICHO LA PILI, NILIBAMBIKIZIWA

> Tundu Lissu ameomba kuhakikishiwa usalama na kulipwa gharama za matibabu na Mafao ya Ubunge ili arejejee nchi

> Pia, ametaka wafungwa wa kisiasa waachiwe huru

Soma https://jamii.app/LissuTanzania
#JFSiasa
RSF: UHURU WA VYOMBO VYA HABARI UPO MASHAKANI ZAIDI KIPINDI CHA #COVID19

- Habari zinazohusu maendeleo ya COVID-19 zimekuwa zikizuiliwa kwenye Nchi nyingi Duniani

- Norway, Finland na Sweden ndizo zilikuwa na Uhuru wa Vyombo vya Habari wa kutosha

Soma - https://jamii.app/PressFreedomCorona
TMA: USAHIHI WA TAARIFA ZA HALI YA HEWA UMEONGEZEKA HADI 80%

> TMA imesema ina wataalamu na vifaa vya kisasa hivyo inatoa taarifa sahihi

> Mamlaka hiyo imewataka Wananchi kujihadhari na Kimbunga Jobo kinachotarajiwa kuifikia Dar Aprili 25, 2021

Soma https://jamii.app/TMA80Percent
NAPE: WATU WANASTAAFU WANAKAA MPAKA WANAKUWA WANYWA GONGO BILA KUPEWA STAHIKI ZAO

- Mbunge huyo ameitaka Serikali ifanyie Uchunguzi madai ya Walimu waliopandishwa madaraja bila Mishahara yao kubadilika na waliofutiwa barua za kupandishwa madaraja

Soma - https://jamii.app/NapeStahikiWalimu
JAJI KIONGOZI: WANAOPELEKA KESI MAHAKAMANI BILA USHAHIDI WACHUKULIWE HATUA

> Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Dkt. Eliezer Fereshi amesema kesi zinazopelekwa bila ushahidi hupelekea mahabusu kuwa wengi na kesi kuchukua muda mrefu

Soma https://jamii.app/KesiBilaUshahidi
NAIBU SPIKA: BUNGE HALINA TAARIFA YA MBUNGE KUVULIWA UANACHAMA

> Akiwa Bungeni, Mbunge Jesca Kishoa (Viti Maalum) alisema ameondolewa kwenye Chama

> Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson asema hawana Mbunge asiye na Chama akimtaka afute kauli yake

Soma https://jamii.app/BungeTaarifa
MBUNGE CCM: BIASHARA ZA MBOWE HAZIJAFUNGWA NA SERIKALI, ALIDANGANYA WATANZANIA

- Jacqueline Ngonyani amesema biashara anazozifanya Freeman Mbowe ni za urithi na alikuwa anazifanya bila kuwapa mrejesho Wanafamilia ndipo walipokwenda Mahakamani

Soma https://jamii.app/NgonyajiMbowe
KLABU YA SIMBA YAFUNGIWA KUFANYA USAJILI KWA MUDA

- Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limeifungia Klabu ya Simba kusajili kwa kipindi kimoja kufuatia kutomlipa beki wao wa Ghana, Asante Kwasi

- Wametakiwa kumlipa Tsh. Milioni 25

Soma - https://jamii.app/FifaSanctionSimba
#JFLeo
ASKOFU GWAJIMA: KUNA WATU WENGI MAHABUSU KWA KUBAMBIKIWA UHUJUMU UCHUMI

Mbunge wa Jimbo la Kawe, Mch. Josephat Gwajima amesema kuna watu 1,701 walio mahabusu ama kwa Utakatishaji Fedha au Uhujumu Uchumi

- Ameongeza β€œHaingii akilini kwanini Masheikh wa Uamsho wako ndani mpaka leo ni miaka 9. Itakuwaje mkagundua hawana hatia, mtawalipa nini kwa miaka waliyopoteza? Wangehukumiwa ikajulikana"

Soma https://jamii.app/GwajimaUtakatishaji
MNYIKA: TULILITAARIFU BUNGE KUHUSU KUFUKUZWA UANACHAMA WA WABUNGE 19 WA VITI MAALUM

> Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema tarehe 01 na 19 Desemba 2020, walitoa taarifa Bungeni kuhusu kufukuzwa kwa Wabunge walioapa mbele ya Spika

Soma - https://jamii.app/BungeCHADEMA
GAMBO: WALIOFUKUZWA KWA VYETI FEKI WALIPWE STAHIKI ZAO

> Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo ameiomba Serikali iwalipe waliofukuzwa kwa Vyeti feki kwa kuwa ni sehemu ya mafanikio ya Serikali, pia mishahara yao ilikatwa kuchangia Mifuko ya Jamii

Soma https://jamii.app/GamboVyetiFeki
NAPE: CHAMA KIKIWAFUKUZA WANACHAMA WAKE, UAMUZI WAO UHESHIMIWE

- Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM) amesema Demokrasia ni pamoja na kuheshimu Taasisi zinazounda #Demokrasia ikiwemo Vyama vya Siasa

- Asema "Sasa hivi kuna Wanachama wapo Bungeni lakini CHADEMA ilishawafukuza. Kwanini wapo Bungeni? Wanatakiwa wasiwepo. Tufuate Sheria"

Tazama > https://youtu.be/_8c2NiSXZ7w
MBATIA: KWANINI TUNAWEKA β€˜PRESSURE’ HADI WATU WANAKIMBIA NCHI?

> M/kiti huyo wa NCCR-Mageuzi amesema CCM imevibagua Vyama vingine vya Siasa kwa miaka 5

> Atoa wito kwa Rais Samia kumuita Tundu Lissu arudi Nchini na Ukabila uliopo uondolewe

Soma https://jamii.app/MbatiaKatiba