JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
WADUKUZI HUTUMIA NJIA ZIFUATAZO KUDUKUA TAARIFA ZA MTUMIAJI WA WI-FI

- Kwa kujiunganisha na Wi-Fi inayotumika

- Kwa kutengeneza 'Hotspot' za uongo

Soma> https://jamii.app/WiFiUdukuzi

#DataProtection #UlinziWaData
ZANZIBAR: MWANDISHI ADAIWA KUPIGWA NA ASKARI AKITEKELEZA MAJUKUMU YAKE

> Jesse Mikofu, Mwandishi wa Habari wa Mwananchi adaiwa kupigwa na kuharibiwa vifaa vyake vya kazi na Askari kwa kosa la kuwapiga picha Askari wakiwa wanawahamisha machinga

Soma https://jamii.app/MwandishiZnz
ZANZIBAR: RAIS HUSSEIN MWINYI AFANYA TEUZI

> Baadhi ya walioteuliwa na Rais Mwinyi ni Kanali Azana Msingiri kuwa Mkuu wa KMKM huku Kanali Makame A. Daima akiwa Kamishna Kikosi cha JKU

> Kanali Rashid Mzee Abdallah anakuwa Kamishna wa Zimamoto na Uokozi

Soma https://jamii.app/ZnzTeuzi
LINDI NA MTWARA ZATAHADHARISHWA KUHUSU KIMBUNGA CHA JOBO

> TMA imetahadharisha Mikoa ya mwambao wa Bahari ya Hindi hasa Lindi na Mtwara kuhusu Kimbunga ambacho kipo Kaskazini mwa Madagascar

> Kitasababisha ongezeko la upepo na mawimbi

Soma https://jamii.app/KimbungaJobo
CHAD: WAASI WATISHIA KUMTOA MADARAKANI RAIS WA MPITO (MTOTO WA RAIS IDRISS DEBY)

- Waasi wa 'Front for Change and Concord in Chad' wamesema wapiganaji wake kwa sasa wanaelekea katika Mji Mkuu wa N'Djamena

- Wasema #Chad sio Nchi ya kifalme

Soma - https://jamii.app/ChadCrisis
MAREKANI: BINTI WA MIAKA 16 APIGWA RISASI NA POLISI

> Ma’Khia Bryant ambaye ni Mmarekani Mweusi amefariki dunia baada ya kupigwa risasi nne na Polisi wa Colombus, Jimbo la Ohio kutokana na madai kuwa alishika kisu kuwadhuru Wasichana wengine

Soma https://jamii.app/RisasiMarekani
NCHI ZA MASHARIKI YA KATI ZATAJWA KUONGOZA KWA MAUAJI YA BINADAMU

- Shirika la Amnesty International limerekodi matukio 483 ya adhabu ya kifo Duniani mwaka 2020

- Nchini #Iran adhabu ya kifo inatumiwa kukandamiza wapinzani na waandamanaji

Soma - https://jamii.app/DeathsCentralEast
#MYANMAR: WATU MILIONI 3.4 WATASHINDWA KUPATA CHAKULA

> WFP imekadiria watu watashindwa kupata Chakula ndani ya miezi 3 - 6 ijayo, kutokana na kukosa Ajira na vyakula kupanda bei

> Watu 250,000 hawana makazi, na watu 738 wameuawa kutokana na ghasia

Soma https://jamii.app/MynamarNjaa
VYANZO VYA MSONGO WA MAWAZO (STRESS) KATIKA ENEO LA KAZI

- Mshahara mdogo: Malipo madogo inatajwa kuwa sababu kubwa ya Msongo wa Mawazo kwa Wafanyakazi kutokana na kutokukidhi mahitaji kikamilifu

- Kukosekana kwa fursa za kukua kitaaluma: Ukuaji kitaalam unamaanisha kupata ujuzi mpya na uzoefu wa kazi ambao utasaidia kufikia lengo

- Kukosa nafasi ya kushiriki katika maamuzi: Hii inamaanisha Viongozi wa kati na wa juu huwasimamia Wafanyakazi wao kwa kuamua kila kitu bila kuwashirikisha wa chini

Soma https://jamii.app/MawazoHuzuni

#StressAwarenessMonth #Employees
KANUNI ZA BUNGE ZATENGULIWA KURUHUSU BAADHI YA VIONGOZI WAINGIE NDANI YA UKUMBI WA BUNGE

> Kanuni ya 160 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge toleo la Juni 2020 zatenguliwa ili Viongozi walioalikwa na Spika waingie ndani ya Ukumbi wa Bunge

Tazama https://youtu.be/Ezf66HMNV0k
UNATAKA KUSAJILI KAZI YA SANAA NA HUJUI VITU VINAVYOHITAJIKA? ANDAA VIFUATAVYO (SEHEMU YA 1)

- Nakala 2 za kazi yako ya sanaa

- Picha 2 za 'Passport Size'

- Nakala ya picha za utambulisho, Kitambulisho cha Kitaifa au cheti cha kuzaliwa

Soma > https://jamii.app/SajiliSanaa
KUKOSEKANA KWA DARAJA LOYA: KILA MWAKA WATU ZAIDI YA 20 WANAFARIKI

- Mbunge wa Igalula, Venant Protas, ameomba fedha za ujenzi ili kunusuru Wananchi wanasombwa na Mto

- Asema Ujenzi wa Daraja hilo umekuwa ukipigiwa kelele tangu Mwaka 2013

Soma - https://jamii.app/DarajaLoya
MAKETE: WATUMISHI WATATU WAHUKUMIWA KWA MAKOSA YA RUSHWA NA UBADHIRIFU

- Wamehukumiwa kifungo cha miaka 3 jela kila mmoja kwa kuomba, kupokea rushwa na ubadhirifu wa fedha za makusanyo ya ushuru kwa njia ya POS na hawakuziwasilisha kwa Halmashauri

Soma - https://jamii.app/JelaWatumishiMakete
UNATAKA KUSAJILI KAZI YA SANAA NA HUJUI VITU VINAVYOHITAJIKA? ANDAA VIFUATAVYO (SEHEMU YA 2)

- Ushahidi wa maandishi kuhusu uhusiano kati ya aliyeenda kusajili na wahusika wengine ikiwa ni kikundi

- Nakala ya makubaliano inayoonesha ushiriki wa wahusika wengine

Soma > https://jamii.app/SajiliSanaa

#JamiiForums #JFSanaa