JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAREKANI: DEREK CHAUVIN AKUTWA NA HATIA YA KUMUUA GEORGE FLOYD

> Aliyekuwa Afisa wa Polisi Minneapolis ametiwa hatiani kwa kupiga goti shingoni mwa George Floyd na kumsababishia kifo

> Kitendo hicho kimetajwa kuwa kinyume na Mafunzo ya Kipolisi

Soma https://jamii.app/ChauvinVsFloyd
AKAUNTI ZA BENKI ZA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU ZAFUNGULIWA

- Akaunti za Benki za Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) zilifungwa kwa takriban miezi 8 tangu Agosti 2020 kutokana na Uchunguzi wa tuhuma mbalimbali

Soma - https://jamii.app/OpenAccTHRDC
ATHARI ZA MSONGO WA MAWAZO (STRESS) MWILINI

- Huvuruga mzunguko wa usingizi ambapo huweza kuathiri vibaya na kusababisha kukosekana kabisa kwa usingizi

- Huvuruga mfumo wa Chakula Mwilini, Tumbo kujaa gesi, maumivu ya Tumbo, kushindwa kumeng'enya Chakula, kutapika na kichefuchefu

- Athari kwenye tishu za Ubongo ikiwemo kushindwa kutumia mbinu za utambuzi katika kudhibiti wasiwasi na hofu

Soma - https://jamii.app/MawazoHuzuni
SUDAN KUSINI: MAMLAKA YATEKETEZA CHANJO 60,000 ZA ASTRAZENECA

> Sudan Kusini imesema Chanjo ziliwasili zikiwa zimebakiza muda mdogo kabla ya kuisha matumizi

> CDC-Afrika imesema walikuwa na muda wa kutosha kutumia Chanjo kabla hazijapitwa wakati

Soma https://jamii.app/SudanKusiniAstraZeneca
UAE YAFIKIRIA KUZUIA SAFARI KWA AMBAO HAWAJAPATA CHANJO YA #COVID19

- Umoja wa Falme za Kiarabu umeshatoa Dozi Milioni 9.8 huku ikiwa na idadi ya Watu Milioni 10

- Watu wengi wenye umri kuanzia miaka 16 na zaidi wanapewa Chanjo bure

Soma - https://jamii.app/UnvaccinedUAE
TANZANIA YAPOROMOKA KTK KUIMARISHA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

- Ripoti ya 2020 ya Reporters Without Borders (RSF) imeitaja #Tanzania kushika nafasi ya 124 kati ya Nchi 180 Duniani

- Mwaka 2019 ilishika nafasi ya 118 huku 2018 ikiwa 93

Soma https://jamii.app/PressFreedom2021
#PressFreedom
MWANZA: RC AWASIMAMISHA WAKUU WA IDARA WATATU KUPISHA UCHUNGUZI

> Kaimu Mweka Hazina, Tabwe Seleman, Kaimu Afisa Manunuzi, Renatus Shule na Kaimu Mhandisi wa Sengerema, William Wandu wamesimamishwa kupisha uchunguzi wa ubadhirifu wa fedha uliotokea

Soma https://jamii.app/SengeremaWakuuWaIdara
WAZIRI WA TAMISEMI AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MTENDAJI WA BUHIGWE

- Waziri Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi Anosta Nyamoga ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu

- Amuagiza Katibu Mkuu wa TAMISEMI kupeleka timu ya uchunguzi

Soma - https://jamii.app/DEDBuhingweOut
WADUKUZI HUTUMIA NJIA ZIFUATAZO KUDUKUA TAARIFA ZA MTUMIAJI WA WI-FI

- Kwa kujiunganisha na Wi-Fi inayotumika

- Kwa kutengeneza 'Hotspot' za uongo

Soma> https://jamii.app/WiFiUdukuzi

#DataProtection #UlinziWaData
ZANZIBAR: MWANDISHI ADAIWA KUPIGWA NA ASKARI AKITEKELEZA MAJUKUMU YAKE

> Jesse Mikofu, Mwandishi wa Habari wa Mwananchi adaiwa kupigwa na kuharibiwa vifaa vyake vya kazi na Askari kwa kosa la kuwapiga picha Askari wakiwa wanawahamisha machinga

Soma https://jamii.app/MwandishiZnz
ZANZIBAR: RAIS HUSSEIN MWINYI AFANYA TEUZI

> Baadhi ya walioteuliwa na Rais Mwinyi ni Kanali Azana Msingiri kuwa Mkuu wa KMKM huku Kanali Makame A. Daima akiwa Kamishna Kikosi cha JKU

> Kanali Rashid Mzee Abdallah anakuwa Kamishna wa Zimamoto na Uokozi

Soma https://jamii.app/ZnzTeuzi
LINDI NA MTWARA ZATAHADHARISHWA KUHUSU KIMBUNGA CHA JOBO

> TMA imetahadharisha Mikoa ya mwambao wa Bahari ya Hindi hasa Lindi na Mtwara kuhusu Kimbunga ambacho kipo Kaskazini mwa Madagascar

> Kitasababisha ongezeko la upepo na mawimbi

Soma https://jamii.app/KimbungaJobo
CHAD: WAASI WATISHIA KUMTOA MADARAKANI RAIS WA MPITO (MTOTO WA RAIS IDRISS DEBY)

- Waasi wa 'Front for Change and Concord in Chad' wamesema wapiganaji wake kwa sasa wanaelekea katika Mji Mkuu wa N'Djamena

- Wasema #Chad sio Nchi ya kifalme

Soma - https://jamii.app/ChadCrisis
MAREKANI: BINTI WA MIAKA 16 APIGWA RISASI NA POLISI

> Ma’Khia Bryant ambaye ni Mmarekani Mweusi amefariki dunia baada ya kupigwa risasi nne na Polisi wa Colombus, Jimbo la Ohio kutokana na madai kuwa alishika kisu kuwadhuru Wasichana wengine

Soma https://jamii.app/RisasiMarekani
NCHI ZA MASHARIKI YA KATI ZATAJWA KUONGOZA KWA MAUAJI YA BINADAMU

- Shirika la Amnesty International limerekodi matukio 483 ya adhabu ya kifo Duniani mwaka 2020

- Nchini #Iran adhabu ya kifo inatumiwa kukandamiza wapinzani na waandamanaji

Soma - https://jamii.app/DeathsCentralEast
#MYANMAR: WATU MILIONI 3.4 WATASHINDWA KUPATA CHAKULA

> WFP imekadiria watu watashindwa kupata Chakula ndani ya miezi 3 - 6 ijayo, kutokana na kukosa Ajira na vyakula kupanda bei

> Watu 250,000 hawana makazi, na watu 738 wameuawa kutokana na ghasia

Soma https://jamii.app/MynamarNjaa