JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SIMIYU: WANAFUNZI 219 WAKATIZA MASOMO KWA KUBEBA UJAUZITO MWAKA 2020

- Kati yao, Wanafunzi 42 ni Shule za Msingi na 177 wa Sekondari

- Wilaya ya Busega na Maswa zimetajwa kuwa na idadi kubwa ambapo Busega wapo 89 na Maswa ni 68

Soma - https://jamii.app/MimbaSimiyu2020
UJERUMANI: WATU 698 WAFARIKI KWA #COVID19 NDANI YA SAA 24 ZILIZOPITA

> Idadi hiyo ni ya pili kwa ukubwa kurekodiwa tangu Corona kuripotiwa nchini humo

> Mawaziri wa Afya wa Majimbo wanakutana kuandaa mpango wa kutoa chanjo kuanzia Desemba 27

Soma https://jamii.app/Germany700Died
BAYUME MOHAMED HUSEN: MSWAHILI ALIYEUAWA KWENYE KAMBI ZA MANAZI UJERUMANI

> Mahjub Adam Mohamed au Bayume Mohmed Husen alizaliwa 1904 Dar. Alipigana Vita ya Kwanza ya Dunia, 1914 Tanganyika ikiwa Koloni la Ujerumani

> Alikwenda kuishi Ujerumani, mwaka 1941 alikamatwa kwa kosa la kuzaa na wanawake wa kijerumani na kuchafua rangi

Soma https://jamii.app/SwahiliNAZI
MANYARA: RC AAMRISHA WATUMISHI WA IDARA YA ELIMU KUONDOLEWA

> RC Mkirikiti ameagiza Watumishi wenye zaidi ya miaka mitano Wilayani Hanang kuondolewa kwa kuwa hawana ubunifu wa kuinua Elimu

> Hanang imefanya vibaya kielimu kwa miaka 3 mfululizo

Soma https://jamii.app/RCManyara
UREMBO: MAMBO YA KUZINGATIA KWA MWANAMKE ANAPOJIREMBA

- Kope: Ni vyema ukawasiliana na Wataalamu wa mambo ya Urembo kwa ushauri na siyo kukurupuka

- Rangi ya mdomo(Lipsticks): Kila mwanamke ana midomo tofauti hivyo rangi inakwenda sambambana na rangi ya ngozi

- Marashi (manukato): Haipendezi kwa mwanamke anayepulizia manukato yanayonukia sana mpaka yakawakera wengine

Soma - https://jamii.app/MakeupTips
#Urembo
UMUHIMU WA MAMA MJAMZITO KULA MLO KAMILI

> Mlo kamili ni muhimu kwa maendeleo mazuri ya afya ya mjamzito na kumuepusha na hatari ya kujifungua #MtotoNjiti

Pamoja na mlo kamili, mjamzito hupewa virutubisho vya ziada(supplements)

Soma > https://jamii.app/UjauzitoMlo

#JamiiForums #DMF
RAIS MWINYI: NIVUMILIENI NICHUKUE MAAMUZI MAGUMU

> Rais wa #Zanzibar amewataka wananchi kuvumilia maamuzi hayo ili kukomesha ufisadi na ubadhirifu wa mali za Umma

> Amesema, amebaini ufisadi katika maeneo mengi ndani ya Mwezi 1 aliokaa madarakani

Tazama https://youtu.be/obxi4Rq7yIo
WAZIRI MKUU ATOA SIKU 7 WAKURUGENZI WAJIELEZE KWANINI MAGARI YAO NI YA GHARAMA KUBWA

> Ameagiza Maofisa wanaochambua maombi ya ununuzi na Wakurugenzi wajieleze

> Amesema, magari hayo ni mzigo kwa wananchi na matumizi mabaya ya Fedha za Umma

Soma https://jamii.app/7DaysPM
AFRIKA YAANZA KUPIGWA NA WIMBI LA PILI LA #CORONAVIRUS

> Maambukizi yameripotiwa kuongezeka kwa baadhi ya nchi zenye watu wengi tangu mwezi Septemba

> Afrika Kusini na #Nigeria ni kati ya nchi zinazorekodi maambukizi mengi kwa siku

Soma - https://jamii.app/IIWaveAfrica
#NIGERIA: WANAFUNZI WALIOTEKWA WAACHIWA HURU

> Wanafunzi 344 waliotekwa na Boko Haram wameachiwa huru wakiwa na hali nzuri

> Gavana Aminu Bello Masari amesema, wamepata wavulana wengi, sio wote. Idadi kamili ya waliotekwa bado haijulikani

Soma https://jamii.app/WaachiwaHuru
KENYA: AKAA JELA MIAKA 8 KWA USHAHIDI WA UONGO WA KUMBAKA BINTIYE

> Mahakama imemuachia huru Julius Wambua ambaye alihukumiwa kifungo cha maisha baada ya Mtoto wake kufundishwa na Mama yake kuidanganya Mahakama kwasababu ya mgogoro na Mumewe

Soma - https://jamii.app/FreedFalseAllegations
DPP: NI KOSA KUWAREJESHEA FEDHA WALIOWEKEZA QNET

> Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), Biswalo Mganga amesema, ni kosa kuwarejeshea fedha wanaodai kutapeliwa na QNET kwa sababu biashara iliyokuwa inafanywa na kampuni hiyo ni upatu haramu

Soma - https://jamii.app/DPPFedhaQNET
KENYA: BUNGE LA SENETI LAMUONDOA MADARAKANI GAVANA SONKO KWA KUKIUKA KATIBA

- Gavana Mike Sonko anadaiwa kukiuka Misingi ya Katiba, kutumia Ofisi vibaya na kukosa uwezo wa kuiongoza Nairobi

- Uchaguzi wa Gavana mpya utafanyika siku 60 zijazo

Soma https://jamii.app/MikeSonkoRemoved
KENYA: GAVANA WA NYAMIRA AFARIKI KWA #COVID19

> Gavana wa Nyamira, John Nyagarama(74) amefariki kwa #COVID19 akiwa Hospitali ya Nairobi akipatiwa matibabu

> Nyagarama alilazwa kwa wiki tatu ambapo baadaye alihitaji kuongezewa Oxygen

Soma https://jamii.app/KenyaGavana
ATHARI ZA KISAIKOLOJIA KWA WASICHANA WANAOBEBA MIMBA KATIKA UMRI MDOGO

- Mimba za utotoni zinaathiri mwenendo na tabia za Msichana

- Asipopata matibabu ya kisaikolojia uwezekano wa kufanya ukatili dhidi ya Mtoto ni mkubwa

- Mimba ina madhara mengi zaidi kwani Msichana anaweza kumkataa au kumkimbia #Mtoto

- Lakini anapokuwa na mtoto huyo, uchungu unazidi na anaweza akaendeleza tabia za ukatili dhidi ya Mtoto

Soma - https://jamii.app/MimbaSaikolojia

#MimbaZaUtotoni
ARUSHA: MADEREVA WANAOTUMIA VILEVI KUWEKWA RUMANDE MPAKA MWAKA MPYA

- RC wa Arusha, Idd Kimanta amesema, kumekuwa na ajali zisizo za lazima ktk Sikukuu za Mwisho wa Mwaka, zinazosababishwa na Madereva wazembe wanaokunywa pombe kupita kiasi

Soma - https://jamii.app/UleviDerevaSikukuu
RAIS WA ZAMANI WA BURUNDI AFARIKI

> Rais Pierre Buyoya (71) amefariki Nchini Ufaransa kutokana na #COVID19

> Aliongoza kwa miaka 13 baada ya kumpindua Jean-Baptiste Bagaza 1987

> Oktoba 2020, alihukumiwa kwa mauaji ya Rais Melchior Ndadaye

Soma https://jamii.app/BurundiBuyoya
VIJUE VYANZO VYA HAKI ZA BINADAMU NCHINI

- Chanzo kikuu ni Katiba ya Tanzania ya 1977

- Sambamba na Katiba vyanzo vingine ni kama vile

- Sheria ya Mtoto Namba 21 ya mwaka 2009

- Sheria ya Watu Wenye Ulemavu Namba 9 ya mwaka 2010

Sheria ya Kuzuia na Kudhibiti UKIMWI Namba 28 ya 2008

- Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini namba 6 ya 2004

- Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura ya 20(R.E. 2002)

- Mikataba ya Haki za Binadamu ya Kimataifa na kikanda ambayo Tanzania imeiridhia

Soma - https://jamii.app/HRTz
#HakiZaBinadamu
DARAJA LA BUSISI KUPEWA JINA LA RAIS MAGUFULI ILI AKUMBUKWE

> Daraja la Kigongo-Busisi lenye urefu wa Kilomita 3.2 litagharimu Tsh. Bilioni 699.2

> Waziri Mkuu amewataka Watanzania kupuuza kauli ya kwamba Serikali inajali vitu badala ya watu

Soma https://jamii.app/DarajaBusisiMagufuli
FAHAMU MALENGO YA SERIKALI KATIKA KUPAMBANA NA UMASIKINI

> Ktk Ilani ya CCM (2020-2025), Serikali itafuatilia utoaji wa Elimu ya #Ujasiriamali unaofanywa na wadau ili kuhakikisha #Elimu hiyo inakidhi viwango

> Kuwezesha Vijana, #Wanawake na Wajasiriamali kujiajiri kwa kuwapatia mafunzo na kurasimisha shughuli zao

Soma - https://jamii.app/IlaniCCM
#Poverty #Accountability