JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Ili somo la TEHAMA lieleweke vizuri ni muhimu kuwa na vitendea kazi sahihi katika ufundishaji wake

Je, Shule zetu zina vitendea kazi sahihi kufundishia somo hilo?

#JamiiForums #JFDigitali #JFElimu #DigitalRights

Video Credit: HakiElimu
πŸ‘2
Je, unajua kufanya mapenzi Mwanamke akiwa juu ni hatari kwa Afya ya Uume?

Unaweza kuwa unashangaa juu ya suala hili, ila ni dhahiri kuwa uume unaweza kuvunjika

Kwa maelezo zaidi tembelea JamiiForums.com, Jukwaa la JamiiCheck

Bofya hapa kufikia mada hii https://jamii.app/AfyaYaUume

#JamiiForums #JFElimu #JFAfya
πŸ€ͺ8🀣5πŸ‘3πŸ”₯1
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeanza kutoa mikopo ngazi ya Diploma kupitia Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB)

Wizara imesema kwa kuanzia Wanafunzi zaidi ya 8,000 watanufaika

Kufahamu zaidi kuhusu mikopo hii bofya link https://jamii.app/MikopoYaDiploma

#JamiiForums #JFElimu
πŸ‘7
Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ), Johnson Soah amesema mojawapo ya changamoto kubwa zinazokabili chuo chao ni ucheleweshaji wa malipo ya ada ambapo wameshuhudia Wazazi/Walezi wakichelewa kulipa Ada za Wanafunzi kwa maelezo kuwa β€˜hali ni ngumu’

Amesema hayo wakati wa Mahafali ya 28 ya #DSJ yaliyofanyika leo Desemba 15, 2023 chuoni hapo Ilala Jijini Dar es Salaam ambapo jumla ya Wanafunzi 309 walihitimu, kati yao wapo wa Astashada (183) na Stashahada (126)

Soma https://jamii.app/MahafaliDSJ23

#JFElimu #JFHuduma #Governance #JamiiForums
πŸ‘2❀1
ELIMU: Wewe ni Mwanafunzi unayejiandaa kwenda Kidato cha 5 ukiwa na ndoto ya kusoma Tahasusi (combination) fulani lakini umepangiwa tofauti na matarajio yako kutokana na sababu mbalimbali?

JamiiForums imezungumza na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini TAMISEMI, Nteghenjwa Hosseah ambaye amefafanua kuwa kabla ya kutuma maombi, mwanafunzi anatakiwa kuzingatia kama ana alama za kutosha (cut-off points) zinazomuwezesha kusoma Tahasusi husika

Maelekezo mengine ni kama yalivyoelezewa kwenye picha

Soma https://jamii.app/Tahasusi

#JamiiForums #JFElimu
πŸ‘1πŸ₯°1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
ELIMU: Wanafunzi 1,230,780 wamesajiliwa na wanatarajiwa kufanya mitihani ya kuhitimu Elimu ya Msingi kuanza leo Septemba 11, 2024, kati yao Wavulana ni Asilimia 46 na Wasichana ni Asilimia 54

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (NECTA), Dkt. Said Mohamed amesema masomo yatakayotahiniwa ni Sita ambayo ni Kiswahili, Kingereza, Sayansi na Teknolojia, Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi, Hisabati na Uraia na Maadili

JamiiForums inawatakia Wahitimu wote kila la kheri katika Mitihani yao.

Soma https://jamii.app/MitihaniSTD7

#JFElimu #JamiiForums
πŸ‘2
DAR ES SALAAM: Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imesema Wananchi wanatakiwa kushirikishwa katika kupendekeza kiasi cha Ada ambacho wanaweza kukilipa katika Shule za Mkondo wa Kingereza (English Medium) zinazomilikiwa na Serikali, huku ikielekeza Halmashauri zote nchini kutotegemea Shule hizo kama vyanzo vya mapato

Mwenyekiti wa Kamati, Husna Sekiboko amesema β€œInawezekanaje Shule ya Serikali inakuwa na gharama kubwa wakati Sera yetu inasema Elimu Bila Ada, hivyo maelekezo ya Kamati, Wananchi wanatakiwa kuamua wao kiasi gani wanachoweza kulipa, Elimu ni Huduma, Halmashauri ni mali ya Serikali.”

Amesema hayo, Septemba 10, 2024 wakati wa ziara ya Kamati ya kukagua Mradi wa Shule ya Awali na Msingi ya Richard Mgana iliyopo Kinondoni.

Soma https://jamii.app/ShuleZaEnglish

#JFHuduma #JFElimu #Accountability #JamiiForums
πŸ‘1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
RUVUMA: Rais Samia Suluhu Hassan amesema mabadiliko ya Mitaala ya Elimu Nchini yamefanyika ili kuendana na mabadiliko ya Dunia, lakini amesisitiza umuhimu wa kuwa na masomo ya Lugha za Kigeni ikiwemo Kichina, ili kuwa na uhusiano mzuri na Nchi Wadau wanaoshirikiana na Tanzania

Amesema hayo alipokuwa katika Shule ya Awali na Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Chief Zulu, Songea, leo Septemba 24, 2024

Soma https://jamii.app/MtaalaWaKichina

#JFMatukio #JFElimu #JamiiForums
πŸ‘2
DAR: Mdau anadai baadhi ya Walimu wanaowafanyisha Mitihani Wanafunzi kila Wikiendi kwa malipo, wamekuwa hawaangalii ubora wa Mitihani husika kwani wanaosahihisha ni Wanafunzi wenyewe

Anasema "Mzazi unalipa pesa ya mitihani lakini cha kushangaza mitihani ikiletwa ukikagua unakuta mtoto kakosa ila kawekewa tiki, ukimuuliza anakuambia wanaosahihisha ni wanafunzi wenzetu"

Soma https://jamii.app/MitihaniWikiendi

#JFElimu #Accountability #Governance #ServiceDelivery #ChildRights #JamiiForums
πŸ‘2
DAR: Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudai uwepo wa ratiba za masomo hadi Saa 4 Usiku unahatarisha usalama wa Wanafunzi, Chuo cha Ustawi wa Jamii kimesema kusoma vipindi vinavyoanza Asubuhi au Mchana ni uamuzi wa Mwanafunzi

Aidha, taarifa ya Chuo hicho imesema kuwa Chuo kina utaratibu wa kuwashirikisha Wanafunzi kila Rasimu ya Ratiba ya Masomo inapoandaliwa

Soma https://jamii.app/UstawiUfafanuzi

#Accountability #JFElimu #JamiiForums
πŸ‘1