JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KUFUZU #AFCON2021: TANZANIA KUNDI MOJA NA TUNISIA NA LIBYA

- CAF yatangaza makundi ya kufuzu kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2021 itakayofanyika Cameroon

- Tanzania ipo Kundi J, pamoja na Tunisia, Libya na Equatorial Guinea

Zaidi, soma https://jamii.app/KufuzuAfcon2021
MICHEZO: TAIFA STARS KUIKABILI EQUATORIAL GUINEA LEO

- Timu ya Taifa ya #Tanzania, Taifa Stars leo inashuka Dimbani saa 4:00 usiku kutafuta tiketi ya kufuzu #AFCON2021 dhidi ya Equatorial Guinea

- Stars ipo Group J yenye timu za Tunisia wenye alama 10, Equatorial Guinea alama 6, Taifa Stars wakiwa na alama 4 na Libya alama 3

- Baada ya mechi ya leo, Taifa Stars watakuja kukipiga na Libya jijini Dar es Salaam Machi 28, 2021.

#JamiiForums #Michezo #Sports
GUINEA: Kiongozi aliyeingia Madarakani kwa kuipindua Serikali, Kanali Mamady Doumbouya ameikabidhi Timu ya Taifa Bendera ili kwenda kushiriki Michuano ya kombe la #AFCON2021

Mamady ameiambia Timu hiyo "Rudini na Kombe la sivyo mtarudisha Fedha zote tulizowekeza kwenu"

#Sports
#AFCON2021: NANI KUWA BINGWA?

Michuano hiyo inaanza kesho Januari 9, kwa wenyeji #TeamCameroon kuivaa #TeamBurkinaFaso majira ya saa 1:00 jioni (EAT)

#TeamAlgeria ambaye ni Bingwa Mtetezi, #TeamCameroon, #TeamSenegal na #TeamEgypt zinapewa nafasi kubwa kuwa Bingwa

#JFSports
#AFCON2021: CAMEROON YAANZA KWA USHINDI

- Mtayarishaji wa Mashindano hayo #TeamCameroon imeanza kwa ushindi wa goli 2-1 dhidi ya #TeamBurkinaFaso katika mchezo wa ufunguzi

- Mchezo unaofuata saa 4:00 usiku (EAT) ni kati ya #TeamEthiopia na #TeamCapeVerde

#JFSports
#AFCON2021: GUINEA, MOROCCO ZAPATA USHINDI

Mchezo wa 2 wa Kundi B kwa siku ya leo, umemalizika kwa #TeamGuinea kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya #TeamMalawi

Pia, mchezo wa kwanza wa Kundi C kwa leo, umemalizika kwa #TeamMorocco kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya #TeamGhana

#JFSports
#AFCON2021: REFA AMALIZA MPIRA MARA 2 KABLA YA DK 90

Janny Sikazwe ameibua utata kwenye mechi ya Tunisia na Mali baada ya kumaliza mchezo ktk dk ya 85, kisha kuruhusu uendelee na kumaliza tena ktk dk ya 89.43

- Mali imeshinda kwa goli 1-0

Soma https://jamii.app/RefaJanny

#JFSports
#AFCON2021: CAMEROON, BURKINA FASO ZAFUZU HATUA YA MTOANO

Mwenyeji wa michuano, #TeamCameroon ameingia hatua ya mtoano baada ya kutoka sare ya goli 1-1 na #TeamCapeVerde

Aidha, #TeamBurkinaFaso imetinga hatua hiyo baada ya kutoka sare ya goli 1-1 na #TeamEthiopia

#JFSports
#AFCON2021: SENEGAL, GUINEA ZAFUZU HATUA YA MTOANO

#TeamSenegal imefuzu kucheza hatua ya mtoano ya michuano baada ya kutoka sare ya 0-0 na #TeamMalawi

Aidha, #TeamGuinea imefuzu kwenda hatua hiyo licha ya kufungwa goli 2-1 na #TeamZimbabwe katika mechi ya mwisho

#JFSports
#AFCON2021: BINGWA MTETEZI, ALGERIA ATOLEWA

#TeamAlgeria imetolewa kwa kufungwa goli 3-1 na #TeamCotedIvoire katika mchezo wa mwisho wa kundi

Equatorial Guinea imeifunga #TeamSierraLeone goli 1-0

Cote d’Ivoire na #TeamEquatorialGuinea zafuzu kucheza hatua ya mtoano

#JFSports
#AFCON2021: HATUA YA MTOANO KUENDELEA KESHO

Hatua ya makundi ya michuano hiyo inayofanyika Cameroon imemalizika Januari 20, 2021.

Timu 16 zilizofuzu kucheza hatua ya mtoano zitaendelea na michuano kesho.

Je, ni timu gani unaipa nafasi ya kuweza kuondoka na Kombe?

#JFSports
#AFCON2021: BURKINA FASO YAFUZU KUINGIA ROBO FAINALI

- #TeamBurkinaFaso imefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali kwenye michuano hiyo baada ya kuifunga #TeamGabon kwa mikwaju ya penati 7-6

- Timu hizo zilimaliza dakika 120 za mchezo zikiwa zimefungana goli 1-1

#JFSports
#AFCON2021: SENEGAL YAFUZU KUCHEZA ROBO FAINALI

- #TeamSenegal imefuzu baada ya kuifunga #TeamCapeVerde goli 2-0 ndani ya dk 90. Wachezaji wawili wa Cape Verde walipewa kadi nyekundu

- Senegal itakutana na mshindi wa mechi kati ya #TeamMali na #TeamEquatorialGuinea

#JFSports
MOROCCO YAFUZU KUCHEZA ROBO FAINALI #AFCON2021

- #TeamMorocco imefuzu kwa kuifunga #TeamMalawi goli 2-1 ndani ya dk 90

- Morocco itakutana na mshindi kati ya #TeamCotedIvoire na #TeamEgypt

- Hii ilikuwa ni mechi ya 10 ya Malawi kwenye michuano na imeshinda mechi 2

#JFSports
#AFCON2021: EGYPT YAINGIA NUSU FAINALI

- #TeamEgypt imefanikiwa kuingia nusu fainali baada ya kuifunga #TeamMorocco goli 2-1 baada ya dk 120

- Egypt itakutana na #TeamCameroon kwenye nusu fainali

- Mechi inayofuata ni kati ya #TeamSenegal na #TeamEquatorialGuinea

#JFSports
#AFCON2021: SENEGAL YAINGIA NUSU FAINALI

- #TeamSenegal imefanikiwa kuingia nusu fainali baada ya kuifunga #TeamEquatorialGuinea goli 3-1

- Senegal itakutana na #TeamBurkinaFaso kwenye nusu fainali

#JFSports
#AFCON2021: SENEGAL YAINGIA FAINALI

- #TeamSenegal imeingia fainali kwa kuifunga #TeamBurkinaFaso goli 3-1 ndani ya dakika 90

- Senegal itacheza fainali na mshindi wa mechi ya kesho kati ya #TeamCameroon na #TeamEgypt

- Burkina Faso itashindania nafasi ya 3 na timu itakayofungwa kesho

#JFSports
#AFCON2021: MISRI YATINGA FAINALI

#TeamEgypt imeingia fainali kwa kumfunga mwenyeji wa michuano, #TeamCameroon kwa penati 3-1 baada ya kutofungana ndani ya dk 120

Misri sasa itacheza fainali na #TeamSenegal huku #TeamCameroon ikiivaa #TeamBurkinaFaso kusaka mshindi wa 3

#JFSports
#AFCON2021: #TeamSenegal imetwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuifunga #TeamEgypt 4-2 kwa mikwaju ya penati

Hii ni mara ya kwanza kwa Senegal kutwaa Ubingwa huo baada ya kucheza jumla ya Fainali tatu za #AFCON

Soma https://jamii.app/SenegalAFCON

#JFSports