JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Timu ya Taifa ya Tanzania (#TaifaStars) imeibuka na ushindi katika mechi zake mbili za kirafiki, kwenye michuano ya CECAFA 3 Nations Tournament ikiwa ni maandalizi ya kuelekea Michuano ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani ya Nchi (#CHAN) 2024 inayotarajiwa kuanza Agosti 2, 2025.

Taifa Stars ilianza vyema kwa kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Uganda Julai 22, 2025, kupitia bao la Iddi Suleimani, kabla ya leo Julai 27, 2025, kushinda 2-1 dhidi ya Senegal kwa mabao ya Abdul Suleiman (#Sopu) na Ibrahim Hamad (#Bacca).

Taifa Stars itacheza na Burkina Faso katika ufunguzi wa CHAN 2024 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kuanzia Saa 2:00 Usiku.

Soma zaidi https://jamii.app/TaifaStars

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFSports
2
MICHEZO: Klabu ya #SimbaSC imeingia makubaliano na Kampuni ya Michezo ya Kubashiri #Betway kuwa mdhamini mkuu kwa mkataba wenye thamani ya Tsh. Bilioni 20 kwa Miaka mitatu.

Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Simba, Zubeda Sakuru amesema “Udhamini huu unaonyesha namna Simba imedhamiria kuleta mabadiliko ya kuwa klabu kubwa.”

Ikumbukwe, udhamini huo mpya unakuja baada ya Simba kuachana na mdhamini wake mkuu, Kampuni ya M-Bet bila kuwekwa wazi kilichotokea ambapo Mwaka 2023 pande hizo zilisaini mkataba wa Miaka mitano wenye thamani ya Tsh. Bilioni 26.1.

Soma Zaidi https://jamii.app/MdhaminiMkuuSimba

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFSports
MICHEZO: Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars", inatarajiwa kushuka dimbani leo Agosti 2, 2025 kuikabili Burkina Faso katika mechi ya ufunguzi ya michuano ya Mataifa kwa Wachezaji wa Ndani (#CHAN) 2024 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuanzia Saa 2:00 Usiku.

Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa Kombe la TotalEnergies CAF CHAN ambayo safari hii inafanyika kwa mfumo wa pamoja katika nchi tatu za Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Kenya na Uganda.

Ikumbukwe, kuwa bingwa mtetezi wa michuano hii ni Senegal ambayo ilitwaa taji hilo nchini Algeria Mwaka 2022 baada ya kuifunga Algeria kwa mikwaju ya penalti.

Je, unadhani Taifa Stars inaweza kufika hatua ipi kwenye michuano hiyo?

Zaidi soma https://jamii.app/TanzaniaUfunguziCHAN

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFSports #JFMatukio
2
MICHEZO: Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” imeibuka na ushindi wa Magoli 2-0 dhidi ya Burkina Faso katika mchezo wao wa kwanza wa CHAN 2024, wafungaji wakiwa ni Selemani Sopu dakika ya 45+3 kwa mkwaju wa penalti na Mohamed Hussein aliyefunga dakika ya 71.

Stars sasa inajiandaa kurejea dimbani kuivaa Mauritania siku ya Jumatano, Agosti 6, 2025, katika mchezo wao wa pili wa Kundi B ambalo pia linajumuisha Madagascar, Mauritania, Central African Republic na Burkina Faso.

Michezo mingine itaendelea Agosti 3, 2025 ambapo Madagascar watacheza na Mauritania kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar Es Salaam, Kenya na Congo DRC wakilipiga mwenye Uwanja wa Moi International Sports Centre.

Zaidi soma: https://jamii.app/TanzaniaUfunguziCHAN

#JamiiForums #JamiiAfrica #JamiiSports #JFSports
2👎1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR ES SALAAM: Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila akionesha uwezo wa kucheza Muziki wa Singeli katika hafla iliyoandaliwa kusherehekea ushindi wa Timu ya Taifa ya Tanzania (#TaifaStars) wa Magoli 2-0 dhidi ya #BurkinaFaso katika michuano ya CHAN, jana Agosti 2, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa.

Soma zaidi https://jamii.app/RCChalamila

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFSports #JFEntertainment
5👎3😁1
UFARANSA: Klabu ya Le Havre Athletic (Le Havre AC) inayoshiriki Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, #MbwanaSamatta (32), ambaye anajiunga na timu hiyo akitokea Klabu ya PAOK ya Ugiriki.

Samatta anakuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligue 1, akiendeleza rekodi yake ya soka barani Ulaya, baada ya kuzitumikia klabu za Aston Villa ya England, KRC Genk na Royal Antwerp za Ubelgiji, Fenerbahce ya Uturuki na PAOK ya Ugiriki.

Le Havre Athletic Club ni moja ya klabu za zamani zaidi nchini Ufaransa, ilianzishwa Mwaka 1884, iliwahi kushinda ubingwa wa Ufaransa Mwaka 1899, na imejijengea umaarufu kwa kukuza vipaji akiwemo #PaulPogba na #RiyadMahrez.

Soma zaidi https://jamii.app/SamattaAtimkiaLigue1

#JamiiForums #JamiiAfrica #JamiiSports #JFSports
DAR: Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” imeandika historia mpya kwenye michuano ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN 2024) baada ya kufikisha alama 6 katika Kundi B baada ya kushinda Goli 1-0 dhidi ya Mauritania, Agosti 6, 2025.

Mchezo ujao wa Kundi B, #Tanzania inatarajiwa kuivaa Madagascar mnamo Agosti 9, 2025, siku hiyo pia Jamhuri ya Kati itaivaa Mauritania.

Zaidi soma https://jamii.app/MechiTanzania

#JamiiForums #JamiiAfrica #JamiiSports #JFSports
1
Bodi ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imeitoza faini Shirikisho la Soka Tanzania (#TFF) Dola 10,000 (takriban Tsh. Milioni 25) kwa kuvunja masharti ya usalama na ulinzi yaliyoainishwa katika Ibara ya 82 na 83 za Kanuni za Nidhamu za CAF, pamoja na Ibara ya 24 na 28 za Kanuni za Usalama na Ulinzi.

Mashtaka hayo yametokana na tukio la ukiukwaji wa taratibu za usalama wakati wa mechi kati ya #Tanzania dhidi ya #BurkinaFaso kwenye Michuano ya CHAN 2024 inayoendelea, ambapo mashabiki walifanya vitendo vya utovu wa nidhamu katika mchezo huo uliomalizika kwa Tanzania kushinda Magoli 2-0.

Pia, Bodi hiyo imeipiga faini Shirikisho la Soka Kenya (FKF) Dola 5,000 (takriban Tsh. Milioni 12) kwa sababu ya msongamano wa watu (stampede) na kuingia bila idhini na Dola 10,000 (takriban Tsh. Milioni 25) kwa kosa la kuwashambulia Wafanyakazi wa #CAF na wageni.

Soma zaidi https://jamii.app/TFFFine

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFSports #Accountability #Uwajibikaji
Timu ya Taifa ya #Tanzania “Taifa Stars” imepata ushindi wa Magoli 2-1 dhidi ya #Madagascar katika Michuano ya CHAN 2024 na hivyo kufikisha Pointi 9 katika Kundi B na kujihakikishia nafasi ya kucheza hatua inayofuata ya Robo Fainali.

Clement Mzize ndiye aliyeifungia Stars Magoli yote kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam ambapo inakuwa imeshinda michezo mitatu mfulizo, ikisaliwa na mchezo mmoja dhidi ya Jamhuri ya Kati unaotarajiwa kupigwa Agosti 16, 2025.

Madagascar imepata goli kupitia kwa Mika Razafimahatana. Michezo inayofuata inatarajiwa kuchezwa Jumapili Agosti 10, 2025 kutoka katika Kundi A; Kenya vs Morocco, Zambia vs Angola.

Kushiriki mjadala bofya https://jamii.app/StarsAgosti9

#JFSports #JamiiForums #JamiiAfrica
1
Mdau wa JamiiForums.com anaeleza, "Msimu wa 2025/26 unatarajia kuanza hivi karibuni, nyota wa soka la Bongo, Clatous Chotta Chama na Jonas Mkude waliokuwa Yanga kwa sasa wapo huru, mastaa hao waliowahi kuwa ‘panga pangua’ kwenye kikosi cha Simba unadhani safari yao sasa itahamia wapi msimu ujao?”

Kushiriki mjadala bofya https://jamii.app/ChamaMkude

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFSports