JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
JULIAN ASSANGE, MWANZILISHI WA MTANDAO WA WIKILEAKS AKAMATWA

> #WikiLeaks ilichapisha taarifa za siri za Serikali mbalimbali mwaka 2010

> 2012 alikimbilia ndani ya Ubalozi wa Ecuador Jijini London baada ya kuanza kusakwa na US & Sweden

Soma > https://jamii.app/AssangeArrested
UINGEREZA: Mwanzilishi wa Mtandao wa #Wikileaks, Julian Assange ambaye amefungwa jela ya Belmearsh tangu 2019 ameruhusiwa kumuoa mpenzi wake Stella Moris akiwa jela

> Uingereza inatambua haki ya wafungwa ya kuomba kufunga ndoa wakiwa jela

Soma https://jamii.app/NdoaAssange
#JFLeo
Uingereza imeidhinisha Julian Assange kupelekwa Nchini Marekani ambapo anatafutwa kuhusiana na nyaraka zilizofichuliwa na mtandao wa #WikiLeaks mwaka 2010 na 2011

> Nyaraka hizo zilionesha Wanajeshi wa Marekani wakiua Raia Nchini Afghanistan

Soma - https://jamii.app/AssangeExtradition
👎14👍2🔥2💩1
Mwanzilishi wa #WikiLeaks, Julian Assange, ameachiwa huru na Mahakama baada ya makubaliano ya kukiri kosa la kuvunja Sheria za Ujasusi za Marekani, makubaliano ambayo yamemaliza kifungo chake Nchini Uingereza

Assange (52) amekiri kosa moja la jinai la kula njama ya kupata na kufichua Hati za Siri za Ulinzi wa Taifa za Marekani, kesi yake ilifanyika katika Kisiwa cha #Saipan kutokana na Assange kukataa kwenda Marekani

Uamuzi huo umefikiwa baada ya Serikali ya Australia kulipa Dola 520,000 (Tsh. Bilioni 1.36) ambazo Assange atazilipa lakini tayari Pauni 277,000 (Tsh. Milioni 919.4) zimepatikana kupitia michango ya Watu mbalimbali

Aidha, hukumu ya kumuachia huru Assange imeeleza hatakiwi kuingia Marekani hadi atakapopata Kibali Maalum

Soma https://jamii.app/JulianAssange24

#JamiiForums #HumanRights #SocialJustice #FreedomOfExpression #Diplomacy
👍5