JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#USAFIRISHAJI: Ni muhimu Mamlaka kuhakikisha Abiria wanapewa Huduma sawa na iliyotangazwa kwenye tiketi za Mabasi wanazozinunua ili kupata thamani ya Fedha zao

Hii itasaidia kuzuia tatizo la Abiria kukata tiketi za daraja la juu lakini wanaelekezwa kupanda Gari za daraja la chini

Kunahitajika #Uwazi na #Uwajibikaji katika sekta ya Usafiri wa Umma

#JamiiForums #Transport #PublicTransport #KeroZaUsafiri #JFUwajibikaji23 #JFHuduma #ServiceDelivery
👍3
UINGEREZA: Chama cha #LiberalDemocrats kimependekeza mpango wa kutoza faini ya hadi Pauni 1,000 (takriban Tsh. 3,589,596) kwa Watu wanaosikiliza Muziki au kutazama Video kwa sauti kubwa katika Usafiri wa Umma

Lengo ni kukabiliana na tabia zisizo za kiungwana na kulinda Haki ya Abiria wanaotamani safari tulivu. Serikali imesema iko tayari kuangalia wazo hilo na inatafiti namna ya kulitekeleza

Utafiti wa hivi karibuni umeonesha asilimia 38 ya watu hukumbana mara kwa mara na kelele zisizotakiwa kutoka kwa wengine kwenye Usafiri wa Umma, huku wengi wao wakihisi kutokuwa huru kukemea tabia hiyo.

Soma https://jamii.app/FineHeadphoneDogders

#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance #PublicTransport #HeadphoneDogders #UKPolitics