JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Dkt. Aikande Kwayu (JamiiForums) anasema Linapokuja suala la kuondoa #Ukoloni, 'Decolonization' sio kitu cha kufanyika mara moja. Mchakato huu inatakiwa uwe endelevu

Lengo kuu linatakiwa kuwa kumpa Mtu uwezo wa kujisimamia mwenyewe yaani 'Self-determination'. Hata baada ya #Uhuru bado tuko kwenye aina fulani ya Ukoloni

Asasi za Kiraia (AZAKI) zilianzishwa ili kuwajengea Wananchi uwezo wa kujisimamia na kujitawala, kuweza kujieleza na kushiriki kwenye masuala muhimu yanayowahusu. Kwa kifupi kazi zetu zote lengo lake ni #Decolonization

Tunapaswa kujiuliza sisi kama #AZAKI, katika huu mchakato wa 'Decolonization' hususani ukiangalia ukweli kwamba tunapata Fedha za kazi zetu kutoka Mataifa ya Nje, tunakuwa sehemu ya kukuza au kuondoa Ukoloni?

#JamiiForums #CSOWeek2023 #WikiYaAZAKI2023 #Governance