JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ISRAEL: Zaidi watu 80,000 wamepinga pendekezo la Waziri Mkuu #BenjaminNetanyahu kutaka #Bunge liwe na Mamlaka ya kubatilisha maamuzi yoyote ya Mahakama ya Juu

> Wakosoaji wanasema mageuzi hayo yatalemaza Uhuru wa Mahakama

Soma https://jamii.app/SupremeCourtIS

#Governance #Democracy
👍14
Serikali ya #Rwanda imetuma Tani 16 za msaada wa Vyakula, dawa za binadamu na vifaa vya matibabu kwa Watu wa #Gaza Nchini #Palestine kutokana na vita inayoendelea baina ya #Israel na Kundi la #Hamas

Msaada huo umefikishwa kwa wahusika kupitia Taasisi ya Jordan Hashemite Charity Organisation (JHCO)

Licha ya kutoa msaada kwa Watu wa Palestina, Rwanda ni miongoni mwa Nchi zenye uhusiano wa karibu na Israel ambapo Waziri Mkuu wa Israel, #BenjaminNetanyahu alitembelea Rwanda Mwaka 2016

Soma https://jamii.app/RwandaGaza

#Governance #Diplomacy #IsraelHamasWar #JamiiForums
5👎2
#DIPLOMASIA: Rais #JoeBiden amemwambia Waziri Mkuu wa Israel, #BenjaminNetanyahu kwamba Marekani haitashiriki katika hatua ya kulipiza kisasi dhidi ya Iran baada ya shambulio la ndege zisizo na rubani na makombora usiku wa Aprili 13, 2024

Tishio la vita ya wazi kati ya #Iran na Israel ambaye ni mshirika mkubwa Marekani, linaliweka eneo la Mashariki ya Kati katika hali ya wasiwasi, hali inayosababisha Mataifa ya Kiarabu na Mamlaka za Kimataifa kama #UN kuingilia kati

Iran imeripotiwa kuingia katika Mgogoro na #Israel ikiituhumu kushambulia Ubalozi wake huko #Damascus na kuua Watu 7 akiwemo Jenerali wa Jeshi la Iran

Soma https://jamii.app/IsraelVsIran2024

#JamiiForums #IranVsIsrael #MiddleEastWar #Diplomacy
😱3👍2👎1😁1
ISRAEL: Baraza la Mawaziri linaloongozwa na Waziri Mkuu, #BenjaminNetanyahu limepiga Kura na kuunga mkono uamuzi wa Serikali kufungia shughuli zote za Kituo cha Televisheni cha #AlJazeera kwa muda wote wa Vita kati ya #Israel na Wanamgambo wa #Hamas

Kwa mujibu wa taarifa ya Netanyahu, Serikali imefikia uamuzi huo ikidai Kituo hicho kinachofadhiliwa na Serikali ya Qatar kimekuwa kikiripoti Habari ambazo zinatishia Usalama wa Taifa, ingawa Al Jazeera inaweza kupinga uamuzi huo kupitia Mahakama

Aidha, kufungiwa kwa Al Jazeera kunakuja ikiwa ni saa chache tangu Serikali ya Israel ikatae kusitisha mashambulizi katika eneo la Gaza huku Waziri Mkuu Netanyahu akidai kusitisha Vita itakuwa sawa na kuwaogopa Hamas

Soma https://jamii.app/AlJazeeraBan

#JamiiForums #PressFreedom #Governance #HumanRights
👍6👎1
ISRAEL: Waziri wa Fedha, Bezalel Smotrich na Waziri wa Usalama wa Taifa, Itamar Ben-Gvir, wametishia kujiuzulu na kuvunja Muungano wa Serikali iwapo Waziri Mkuu, #BenjaminNetanyahu atakubali pendekezo la kusitisha mapigano Gaza lililotolewa na Rais #JoeBiden, wakisema wanapinga makubaliano yoyote kabla ya #Hamas kuharibiwa kabisa

Pendekezo la Biden lingeanza na kusitisha mapigano kwa Wiki 6 ambapo Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lingeondoka maeneo yenye Watu wengi Gaza, Makubaliano ambayo yangesababisha kuachiliwa kwa mateka wote, kusitisha mapigano kwa kudumu na mpango mkubwa wa ujenzi upya wa Gaza

#Netanyahu amesisitiza hakutakuwa na usitishaji wa kudumu wa mapigano hadi uwezo wa kijeshi na wa kiutawala wa Hamas utakapoharibiwa na mateka wote kuachiliwa, huku Kiongozi wa upinzani, Yair Lapid akiahidi kuunga mkono Serikali ikiwa itakubali kusitisha Mapigano

Tangu kuanza kwa Mapigano Oktoba 7, 2023 Zaidi ya Watu 36,000 wameuawa Gaza

Soma https://jamii.app/GazaCeasefire

#JamiiForums #IsraelVsHamas
👍4