JamiiForums
56.3K subscribers
32.7K photos
1.82K videos
29.9K links
Official JamiiForums Telegram Channel | Be Informed, Engaged & Entertained
Download Telegram
ISRAEL vs PALESTINA: Mpaka sasa Vifo vya Wapalestina vimefikia 83 huku Watu 480 wakijeruhiwa kutokana na Mapigano yanayoendelea

- Mapigano hayo kati ya Israel na kundi la Wanamgambo wa #Hamas yamesababisha uharibifu mkubwa huko Gaza

#GazaUnderAttack #IsraelPalestineConflict
ISRAEL/GAZA: Watu zaidi ya 1,100 wameripotiwa kupoteza maisha katika mapigano kati ya #Israel na #HAMAS wakiwemo Watoto zaidi ya 100 na majeruhi zaidi 3,000

Kwa mujibu wa #AlJazeera na #Reuters, Watu zaidi ya 123,000 wamelazimika kuyakimbia makazi yao kutokana na mashambulizi hayo

Aidha, takwimu zinaonesha kwa kipindi cha miaka 15 kutoka Mwaka 2008, mapigano kati ya Israel na #Palestina yamegharimu maisha ya Watu zaidi ya 7,500, ambapo kumekuwa na wastani wa siku 100 za mapigano tangu wakati huo

Soma https://jamii.app/GazaDeaths

#JamiiForums #JFMatukio #Diplomacy #HumanRights
ISRAEL: Maafisa wa #Tanzania wanaendelea kuwatafuta Watanzania wawili waliokuwa Kusini mwa #Israel ambapo kuna vita kati ya Taifa hilo na wapiganaji wa #Hamas kutoka #Palestine

Balozi wa Tanzania Nchini Israel, Alex Kallua amesema Wanafunzi hao waliokuwa katika mafunzo ya vitendo, wametafutwa hadi Hospitali walikolazwa majeruhi wa vita lakini hawajapatikana

Kati ya Watanzania 350 wanaoishi Israel, 260 ni Wanafunzi wanaosomea Masuala ya Kilimo

Soma https://jamii.app/TZIsrael

#Diplomacy #IsraelPalestineWar #Governance #JamiiForums
Umoja wa Mataifa (UN) umesema umejulishwa na Jeshi la #Israel kuwa Wakazi wa Gaza Kaskazini wanatakiwa kuondoka eneo hilo ndani ya Saa 24 zijazo wakati huu ambapo kuna mashambulizi yanaendelea kati ya Jeshi la Israel dhidi ya Wanamgambo wa #Hamas

#UN imesema jambo hilo ni gumu kutekelezeka kutokana na mazingira yaliyopo kwa kuwa idadi hiyo ni nusu ya watu wote wanaoishi #Gaza

Soma https://jamii.app/24HoursGaza

#Diplomacy #IsraelPalestineWar #Governance #JamiiForums
Shirika la Kutetea Waandishi wa Habari (CPJ) linakadiria Waandishi takriban 22 wamepoteza Maisha tangu kuanza kwa Mapigano kati ya Israel na Jeshi la Hamas Oktoba 7, 2023

#CPJ inahusisha vifo 15 kati ya hivyo na mashambulizi ya anga yaliyofanywa na #Israel na Mawili kutoka kwa #Hamas, huku Waandishi 8 wakijeruhiwa na Watatu hawajulikani walipo

Soma https://jamii.app/CPJReport

#IsraelHamasWar #PressFreedom #FreedomOfSpeech #HumanRights #JamiiForums
Serikali ya #Rwanda imetuma Tani 16 za msaada wa Vyakula, dawa za binadamu na vifaa vya matibabu kwa Watu wa #Gaza Nchini #Palestine kutokana na vita inayoendelea baina ya #Israel na Kundi la #Hamas

Msaada huo umefikishwa kwa wahusika kupitia Taasisi ya Jordan Hashemite Charity Organisation (JHCO)

Licha ya kutoa msaada kwa Watu wa Palestina, Rwanda ni miongoni mwa Nchi zenye uhusiano wa karibu na Israel ambapo Waziri Mkuu wa Israel, #BenjaminNetanyahu alitembelea Rwanda Mwaka 2016

Soma https://jamii.app/RwandaGaza

#Governance #Diplomacy #IsraelHamasWar #JamiiForums
UMOJA WA MATAIFA: ZAIDI YA WATU 10,000 WAMEUAWA GAZA

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres, mashambulizi yanayoendelea #Gaza pia, yamesababisha athari kubwa kwa Watoto ambapo kila baada ya dakika 10 Mtoto mmoja anauawa

Guterres amesema hadi sasa takriban Watoa Huduma 89 wa UN wamepoteza maisha wakati wakiwa katika zoezi la kutoa misaada kwa waathirika wa mapigano kati ya #Israel na #Hamas

Soma https://jamii.app/GazaFatality

#JamiiForums #Governance #HumanRights #IsraelHamasWar #ChildRights
Akiwa katika Ziara ya Kikazi, Jijini #TelAviv Nchini Israel, Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (#IPU) Dkt. Tulia Ackson ameielekeza Kamati inayoshughulikia Masuala ya Mashariki ya Kati ya Umoja huo kutafuta suluhusho linaloweza kuhakikisha amani na usalama vinapatikana kufuatia mgogoro unaoendelea baina ya #Israel na #Hamas

Amesema "Kamati yetu inayoshughulikia Masuala ya Mashariki ya Kati itakuwa hapa siku zijazo kutafuta uhalisia wa mgogoro huu na kuleta taarifa ambayo tutapata nafasi ya kuijadili ili tuone huko mbele tunakokwenda tunawezaje kuwa na amani na usalama kwa watu wote."

Soma https://jamii.app/DktTuliaIsrael

#JamiiForums #Governance #IsraelPalestineConflict
UTAFITI: Mwaka 2023 umetajwa kuwa na idadi kubwa ya vifo na majeruhi ya Raia ndani ya kipindi cha Miaka 10 iliyopita kulingana na Utafiti wa Shirika la Kutoa Misaada Kuhusu Vurugu za Kivita (AOAV) la England

Ongezeko la vifo kwa Asilimia 112 ni kutoka Mwaka 2022 hadi 2023 ambapo vita ya #Israel na #Hamas imechangia kwa kiasi kikubwa ikifuatiwa na migogoro inayoendelea Urusi na #Ukraine, Sudan, #Myanmar na #Somalia

Milipuko ya 2023 ilikuwa 7,307 kutoka 4,322 ya Mwaka 2022, vifo vya Raia vilikuwa 15,305 na matumizi ya silaha zinazorushwa hewani yaliongezeka kwa 226% (kutoka matukio 519 hadi 1,694)

Soma https://jamii.app/Milipuko2023

#HumanRights #CivilRights #Governance #JamiiForums
UFARANSA: Mshambuliaji wa Al-Ittihad ya Saudi Arabia, #KarimBenzema amefungua mashtaka akidai Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa, Gerald Darmanin amemchafulia jina lake kwa kusema Benzema ana uhusiano na Kundi la Muslim Brotherhood lililopigwa marufuku katika Nchi kadhaa zikiwemo Misri, Urusi na Saudi Arabia

Oktoba 2023, Darmanin alitoa madai hayo baada ya Benzema kuandika kupitia #X akieleza kuwa anaunga mkono watu wa #Gaza kutokana na kuathiriwa na vita inayoendelea baina ya #Israel na #Hamas, ambapo alieleza Watoto na Wanawake ni waathirika Wakubwa

Hii si mara ya kwanza kwa Darmanin kumshambulia Benzema, aliwahi kufanya hivyo akidai nyota huyo aligoma kuimba Wimbo wa Taifa wa Ufaransa alipokuwa akiichezea timu hiyo

Soma https://jamii.app/BenzemaFile

#JFSports #Governance #HamasIsraelWar #JamiiForums
#JuliaSebutinde ambaye amechaguliwa kwa kipindi cha Miaka 3 amekuwa Jaji wa ICJ kwa zaidi ya Miaka 10. Hapo awali aliendesha kesi kadhaa za uhalifu wa kivita, ikiwa ni pamoja na kufunguliwa mashtaka kwa Rais wa zamani wa #Liberia Charles Taylor

Sebutinde mzaliwa wa #Uganda alikuwa Jaji pekee katika jopo la Wanachama 17 wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kupiga kura dhidi ya hatua zote 6 zilizopitishwa na Mahakama ya ICJ katika kesi iliyofunguliwa na Afrika Kusini, ambapo Israel iliamriwa ichukue hatua za haraka kuzuia Mauaji ya halaiki inapopambana na Wanamgambo wa #Hamas huko #Gaza

Serikali ya Uganda ilijitenga na maoni pinzani ya Jaji Sebutinde ikisema hawakilishi msimamo wa nchi hiyo katika mzozo huo

Soma https://jamii.app/JajiSebutinde

#JamiiForums #Democracy #Diplomacy #Governance
ISRAEL: Baraza la Mawaziri linaloongozwa na Waziri Mkuu, #BenjaminNetanyahu limepiga Kura na kuunga mkono uamuzi wa Serikali kufungia shughuli zote za Kituo cha Televisheni cha #AlJazeera kwa muda wote wa Vita kati ya #Israel na Wanamgambo wa #Hamas

Kwa mujibu wa taarifa ya Netanyahu, Serikali imefikia uamuzi huo ikidai Kituo hicho kinachofadhiliwa na Serikali ya Qatar kimekuwa kikiripoti Habari ambazo zinatishia Usalama wa Taifa, ingawa Al Jazeera inaweza kupinga uamuzi huo kupitia Mahakama

Aidha, kufungiwa kwa Al Jazeera kunakuja ikiwa ni saa chache tangu Serikali ya Israel ikatae kusitisha mashambulizi katika eneo la Gaza huku Waziri Mkuu Netanyahu akidai kusitisha Vita itakuwa sawa na kuwaogopa Hamas

Soma https://jamii.app/AlJazeeraBan

#JamiiForums #PressFreedom #Governance #HumanRights
ISRAEL: Waziri wa Fedha, Bezalel Smotrich na Waziri wa Usalama wa Taifa, Itamar Ben-Gvir, wametishia kujiuzulu na kuvunja Muungano wa Serikali iwapo Waziri Mkuu, #BenjaminNetanyahu atakubali pendekezo la kusitisha mapigano Gaza lililotolewa na Rais #JoeBiden, wakisema wanapinga makubaliano yoyote kabla ya #Hamas kuharibiwa kabisa

Pendekezo la Biden lingeanza na kusitisha mapigano kwa Wiki 6 ambapo Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lingeondoka maeneo yenye Watu wengi Gaza, Makubaliano ambayo yangesababisha kuachiliwa kwa mateka wote, kusitisha mapigano kwa kudumu na mpango mkubwa wa ujenzi upya wa Gaza

#Netanyahu amesisitiza hakutakuwa na usitishaji wa kudumu wa mapigano hadi uwezo wa kijeshi na wa kiutawala wa Hamas utakapoharibiwa na mateka wote kuachiliwa, huku Kiongozi wa upinzani, Yair Lapid akiahidi kuunga mkono Serikali ikiwa itakubali kusitisha Mapigano

Tangu kuanza kwa Mapigano Oktoba 7, 2023 Zaidi ya Watu 36,000 wameuawa Gaza

Soma https://jamii.app/GazaCeasefire

#JamiiForums #IsraelVsHamas
#Israel na Hamas wamefikia makubaliano ya kusitisha mapigano kwa lengo la kumaliza Miezi takriban 15 (tangu Oktoba 7, 2023) ya mzozo katika ukanda wa #Gaza

Makubaliano ya usitishaji mapigano ya kwanza yalifanyika Novemba 2023 na kudumu kwa takriban Wiki moja. Katika kipindi hicho, mateka 105 waliokuwa wakishikiliwa na #Hamas hasa Wanawake, Watoto, na Wazee waliachiliwa, huku Israeli ikiwaachia huru wafungwa takriban 240 wa Kipalestina

Aidha, Hamas na washirika wake wanashikilia Watu 94 (Hai na Wafu) waliotekwa kutoka Israeli ingawa idadi halisi inafikiriwa kuwa kubwa zaidi. Katika ya hao 84 ni raia wa Israeli, 8 ni raia wa Thailand, 1 kutoka Nepal na 1 kutoka Tanzania

Soma https://jamii.app/GazaCeasefireDeal

#JamiiForums #HumanRights