JamiiForums kwa Kushirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) zitaendesha mjadala Septemba 5, 2024 kupitia XSpaces kuanzia Saa 12:00 Jioni hadi Saa 2 Usiku
Mjadala utaangazia hali ya Mifumo ya Haki Jinai na masuala ya Haki za Binadamu nchini kwa kulinganisha na Mapendekezo ya Tume ya Rais ya Haki Jinai
Shiriki Mjadala https://jamii.app/HakiJinaiSpaces
#JamiiForums #Governance #HumanRights #CriminalJusticeReforms #JFHakiRaia #JFSpaces #LHRCSpaces

AFCON 2025: Timu ya Taifa ya Tanzania ‘#TaifaStars’ imeambulia pointi moja katika matokeo ya 0-0 ya mchezo wa kwanza wa Kundi H dhidi ya Ethiopia kwenye kuwania Kufuzu Michuano ya Afrika (AFCON 2025), wakitoana jasho kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam
Baada ya matokeo hayo mchezo unaofuata ni dhidi ya Guinea (Septemba 10, 2024) ambapo utachezwa kwenye Uwanja wa Charles Konan Banny, Nchini Ivory Coast ambapo Guinea wamechagua kutumia kama Uwanja wao wa Nyumbani
Timu mbili zitakazoongoza Kundi zitafuzu kucheza michuano hiyo ambayo inatarajiwa kufanyika Nchini Morocco
Soma https://jamii.app/TanzaniaEthiopia
#JFSports #AFCON2025 #JamiiForums

DAR: Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema “Kuna Wakandarasi mnaochukua zabuni za Ujenzi wa Majengo lakini baada ya kusaini mkataba, Uswahili unaanza mpaka aliyekupa kazi anajiuliza hawa ndio Wazawa ambao Serikali inawatengenezea mazingira ya kuwapatia fursa mara dufu? Natoa onyo msimamie na muheshimu taaluma zenu.”
Bashungwa ameagiza Bodi ya Usajili ya Wakandarasi (CRB), Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) na Bodi ya Usajili ya Wakadiriaji Majengo na Wabunifu wa Majengo (AQRB) kuchukua hatua baadhi ya Kampuni ya Makandarasi ya ujenzi yanayoshindwa kutekeleza kazi kwa weledi (Makanjanja)
Amesema hayo leo Septemba 4, 2024 katika mkutano wa Wadau wa Miundombinu, ambapo ameongeza “Wapo ambao wakipewa malipo ya awali, hawayapeleki kwenye Mradi wanapeleka katika matumizi yao binafsi. Kuna Wateja wamekuja na nimeagiza uchunguzi ufanyike kuhusu Wakandarasi Makanjanja.”
Soma https://jamii.app/WakandarasiWazawa
#JFMatukio #JFUwajibikaji #ServiceDelivery #JamiiForums

#MICHEZO: Mshambuliaji wa Uruguay, Luis Suarez (37) ametangaza rasmi kustaafu Soka la Kimataifa
Akizungumza na Waandishi wa Habari Septemba 3, 2024, Mjini Montevideo amethibitisha kuwa Mchezo wa Kufuzu Kombe la Dunia Septemba 6, 2024 ndio utakuwa mchezo wake wa mwisho katika Timu yake ya Taifa
Suarez ni miongoni mwa Wafungaji Bora katika Timu ya Taifa ya Uruguay akiwa na magoli 69 katika michezo 142 aliyochezea timu yake
Soma https://jamii.app/SuarezQuitsInternationalFootball
#JamiiForums #JFSports

Linda Yaccarino, Mtendaji Mkuu wa Mtandao wa Kijamii wa X (zamani Twitter) aliandika nukuu hiyo Agosti 26, 2024 katika Ukurasa wake wa X akinukuu hotuba ya Rais wa Kwanza wa Marekani, George Washington aliyoitoa mwaka 1783
#JamiiForums #GoodMorning #AmkaNaJF #FreeSpeech #JFQuotes #NukuuZaJF #FreedomOfExpression

KENYA: Miezi 18 tangu Kampuni ya Huduma za Intaneti ya Starlink iingie nchini humo, imedaiwa Mitandao ya Simu imeanza kupata changamoto ya ushindani sokoni ikiwemo kwenye gharama na uhakika wa huduma
Kwa mujibu wa Tovuti ya Citizen Digital, Kampuni ya Safaricom imeandika barua kwa Mamlaka ya Mawasiliano (CA) ikiitahadharisha Serikali kuwa uwepo wa Watoa Huduma za Intaneti kwa Setilaiti unaweza kusababisha mwingiliano wa kimawasiliano hivyo kuathiri ubora wa huduma
Soma https://jamii.app/IntanetiCompee
#JamiiForums #DigitalRights #JFHuduma #JFDigitali #ServiceDelivery #DigitalWorld

JIUNGE NA 'CHANNEL' YETU YA WHATSAPP KWA TAARIFA MBALIMBALI
JamiiForums inaendelea kukupa nafasi ya kupata Taarifa na Elimu kwa ukaribu na urahisi zaidi, kupitia Mtandao wa WhatsApp
Jiunge na familia ya JamiiForums kwa kubofya https://jamii.app/JFonWhatsApp
#DigitalRights #DigitalWorld #JamiiForums

Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2003, nguli wa Soka Duniani, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo hawamo kwenye orodha ya Wachezaji walioteuliwa kuwania Tuzo ya Ballon d'Or.
Messi alishinda Tuzo hiyo mara 8 huku Ronaldo akishinda mara 5
Orodha ya Wachezaji 30 walioteuliwa kuwania imewajuisha Jude Bellingham, Lamine Yamal, Nico Williams, Alejandro Grimaldo, Dani Olmo, Rodri, Dani Carvajal, Kylian Mbappe, Vinicius Junior na Lautaro Martinez
Mdau, unadhani nani anastahili ushindi wa Tuzo ya Ballon d'Or 2024?
Mjadala https://jamii.app/TuzoZaSoka2024

HAKI ZA BINADAMU: Mahakama ya Wilaya ya Tanga inatarajiwa kutoa uamuzi wa kuhusu maombi ya Jeshi la Polisi kutaka Kada wa CHADEMA, Kombo Mbwana asipewe dhamana kutokana na sababu za Upelelezi unaoendelea dhidi ya kada huyo
Kombo ambaye aliripotiwa kutoweka kwa zaidi ya siku 29 na baadaye Jeshi la Polisi Tanga kutangaza kumshikilia, anakabiliwa na kesi ya Jinai akidaiwa kutumia Vifaa vya Mawasiliano ikiwemo Laini ya Simu isiyo na usajili wake
Imeelezwa kuwa licha ya Mashtaka hayo kuwa na dhamana na Mahakama kueleza dhamana yake iko wazi tangu aliposomewa mashtaka Julai 16, 2024, Vyombo vinavyomshikilia havijatekeleza uamuzi wa Mahakama hadi sasa
Soma https://jamii.app/KomboDhamana
#JamiiForums #Governance #HumanRights #JFHakiRaia #SocialJustice #PoliceBrutality #CrimanalJustice

Mdau wa Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ndani ya JamiiForums.com amesema anatamani kufahamu ni kwa namna gani Wanaume wanaweza kushiriki katika Kampeni za Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Wasichana kuanzia ngazi ya familia, akidai baadhi yao wamekuwa wakiona hawahusishwi katika Kampeni hizo
Ukatili wa Mitandaoni ni aina mojawapo ya aina za Ukatili wa Kijinsia ambapo Wanawake hunyanyaswa katika Majukwaa ya Kidigitali kutokana na jinsia yao
Unadhani ni kwa namna gani Wanaume wanaweza wakashiriki kupinga Ukatili dhidi ya Wanawake hasa Ukatili wa Mitandaoni?
Mjadala https://jamii.app/WanaumeNaGBV
#EndGBV #PingaUkatiliMtandaoni #UkatiliMtandaoni #OnlineSafety #DigitalRights #JFWomen

TANZIA: Mwanariadha wa Uganda na Mshiriki wa Michezo ya Olimpiki, Rebecca Cheptegei amefariki dunia kutokana na majereha aliyopata baada ya kuchomwa Moto na mpenzi wake
Cheptegei alihamishiwa Nchini Kenya kwaajili ya Matibabu zaidi huku taarifa zikieleza sababu ya mpenzi wake kummwagia Petroli na kumchoma moto ni Mgogoro wa Ardhi
Kabla ya kifo chake, Mwanariadha huyo alishiriki Mbio za Olimpiki jijini Paris 2024 na kushika nafasi ya 44, pia, aliwahi kushika nafasi ya 14 katika Mbio za Michuano ya Mabingwa wa Dunia mwaka 2023
Soma https://jamii.app/CheptegeiDies
#JamiiForums #JFMatukio #RIPCheptegei

DODOMA: Mkutano wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (Annual Non-Government Organizations Forum) unaendelea leo Septemba 5, 2024 ikiwa ni siku ya pili kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete
Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana na Baraza la Taifa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO), ulianza Septemba 4, 2024 na unatarajiwa kuhitimishwa kesho Septemba 6, 2024
Baadhi ya malengo ya Mkutano ni Kujenga Uelewa wa pamoja kuhusu Uratibu na Usimamizi wa Mashirika hayo (NGO’s), kujadili mchango wa wao katika Maendeleo ya Taifa, kubainisha shughuli za Mashirika zinavyoweza kwenda sambamba na mipango ya Kitaifa na kuimarisha uhusiano baina ya Serikali na Mashirika hayo
Soma https://jamii.app/ANGOF2024
#JFMatukio #Governance #ANGOsForum2024 #ANGOF2024 #JamiiForums

CHINA: Serikali ya Rais Xi Jinping imeahidi kutoa takriban Dola za Marekani Bilioni 50 (zaidi ya Tsh. Trilioni 139.39) kwaajili ya kufadhili shughuli mbalimbali za Ushirikiano wake na Mataifa ya Afrika
Kupitia Mkutano wa Wakuu wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), uliohusisha Wakuu wa Nchi 53 za Afrika, Jinping amesema China haitaki maslahi ya ubinafsi na makubaliano kati ya China na Afrika yanalenga kufanya maisha kuwa bora kwa watu wa Afrika
Kupitia Mkutano huo, Serikali China ilisaini Hati ya Makubaliano mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan na Rais Hakainde Hichilema ikiwa ni kwaajili ya Uboreshaji wa Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA)
Soma https://jamii.app/FOCAC2024
#JamiiForums #Diplomacy #Governance #AfricasBusiness #FOCAC2024