JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TANZANIA YATAJWA KUWA NA HALI MBAYA YA ULINZI WA KIDIGITALI NA ULINZI WA DATA

> Utafiti uliofanywa na Comparitech ya nchini Uingereza umeitaja Tanzania katika orodha ya Nchi zilizo na changamoto ya #UlinziWaKidigitali

> Takwimu zinaonesha 28.03% ya Simu nchini Tanzania zimeingiliwa na virusi vya mtandao huku 14.7% ya Kompyuta zikiwa zimeingiliwa na virusi

Soma > https://jamii.app/DataProtectionTz

#DataProtection
TUME YA UCHAGUZI YAONGEZA SIKU 3 ZA UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA

> NEC imeongeza muda wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Dar es Salaam

> Zoezi hilo litafungwa rasmi Februari 23, 2020

Zaidi, soma - https://jamii.app/UandikishajiWapigaKura
RAIS WA KLABU YA PSG APIGWA FAINI KWA KUTOA RUSHWA

- Nasser Al-Khelaifi amepigwa faini na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ya Switzerland kwa kumpa rushwa Katibu wa zamani wa FIFA, Jerome Valcke

- Madai hayo yanahusiana na wakati Al-Khelaifi akiwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Utangazaji ya BeIN
UGANDA: MWANAHARAKATI DKT. STELLAH NYANZI AACHIWA HURU

- Ameachiwa huru leo baada ya Jaji kusema alihukumiwa kimakosa

- Agosti 2019 alihukumiwa miezi 18 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumdhalilisha Mtandaoni Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Zaidi, soma https://jamii.app/StellaNyanziHuru
LESOTHO: CHAMA TAWALA CHAMTAKA WAZIRI MKUU KUJIUZULU LEO

> Thomas Thabane aliahidi kujiuzulu baada ya Polisi kumhusisha kwenye mauaji ya Mkewe wa kwanza, lakini ameshindwa kutekeleza ahadi hiyo

> Chama hicho chadai hawezi kubaki madarakani

Zaidi, soma https://jamii.app/ThabaneKujiuzuluLesotho
HOJA: FAHAMU KUHUSU NDEGE BUNDI NA KUHUSISHWA KWAKE NA VIFO

> Mdau wa JamiiForums anadai Bundi anaponekana kifo hutokea kwa sababu ya uwezo wa kuvuta harufu ya mzoga kutoka mbali

> Ameeleza kuwa Binadamu huanza kufa 'organ' za mwili na Bundi anapoonekana, dalili mtu ameshaanza hatua za kufariki

Kujadili, tembelea https://jamii.app/FahamuKuhusuBundi
MAONI: KANUNI ZITUNGWE KUDHIBITI KUREKODIWA KWA MATUKIO YANAYODHALILISHA WATOTO SHULENI

> Mdau wa JamiiForums ameomba Wizara ya Elimu ipige marufuku Walimu kurekodi Watoto bila ridhaa yao

> Amesema ili kumlinda mtoto, kuwepo na adhabu hata ya kufukuzwa kazi kwa atakayebainika kurekodi

Kujadili, tembelea https://jamii.app/MawazoYaMdau
JE, UCHUMI NI SABABU YA MAHUSIANO MENGI KUTODUMU NA VIJANA WENGI KUTOOA?

> Mdau wa JamiiForums anadai kuna ongezeko la mahusiano/ndoa kuvunjika na vijana wengi kuchelewa kuoa au kutooa

> Anadai kuwa moja ya changamoto kubwa katika kuchangia suala hili ni kipato cha wahusika

Kujadili, tembelea https://jamii.app/MahusianoUchumi
SUDANI KUSINI: RAIS KIIR NA MPINZANI WAKE WAKUBALIANA KUUNDA SERIKALI YA MUUNGANO

> Rais Salva Kiir na Riek Machar wameridhia kuunda Serikali ya Muungano

> Makubaliano hayo yanatarajiwa kumaliza vita ya takriban miaka 6 nchini humo

Soma https://jamii.app/MuunganoSudaniKusini
RWANDA YAPINGA UCHUNGUZI HURU WA KIFO CHA MSANII KIZITO

- Uchunguzi huo ni juu ya kifo cha Msanii Kizito Mihigo anayedaiwa kujinyonga akiwa Kituo cha Polisi

- Imesema yenyewe ni nchi huru inayojitawala na inayoweza kuchunguza kitu chochote

Zaidi, soma https://jamii.app/RwandaUchunguziKifoKizito
LESOTHO: WAZIRI MKUU KUSHTAKIWA KWA MAUAJI YA MKEWE

- Waziri Mkuu Thomas Thabane (80) atashtakiwa kwa mauaji ya Mke wake wa kwanza, Lipolelo Thabane

- Aidha, Thabane anakabiliwa pia na kesi ya kujaribu kumuua mtu mwingine aliyekuwepo wakati Lipolelo akiuawa

Zaidi, soma https://jamii.app/WaziriMkuuKushtakiwa-LSTH
#CORONAVIRUS: VIFO VYAFIKIA 2,247 HUKU WAATHIRIKA WAFIKIA 76,691

- Idadi hiyo ni kwa Dunia nzima huku kukiwa na vifo 11 nje ya 'Mainland China'

- Idadi ya vifo sehemu nyingine; Japan (3), Hong Kong (2), Iran (2), Taiwan (1), Ufilipino(1), Korea Kusini (1) na Ufaransa (1)
MBOWE: TUNAWAFAHAMU WOTE WANAOTAKA KUHAMA CHADEMA

- Amesema wanawafahamu Wanachama wote wa CHADEMA wenye nia ya kutengeneza migogoro na baadaye kuhama

- Amebainisha kuwa hawawezi kuwafukuza kwani baadaye watalalamika wameonewa na kufukuzwa

Zaidi, soma https://jamii.app/MboweVsWanaoondokaCDM
TUNDUMA: POLISI WAZUIA MKUTANO WA MBUNGE, WADAI KUNA UWEZEKANO WA UVUNJIFU AMANI

> Polisi wamezuia mkutano wa Mbunge Frank Mwakajoka (CHADEMA) wakidai kuna taarifa za Kiintelijensia zinazoashiria kuwepo uwezekano wa kutokea uvunjifu wa amani

Zaidi, soma https://jamii.app/ZuioMkutanoTunduma
UINGEREZA: ASILIMIA 61 YA WANAWAKE HUUAWA NA WAUME ZAO

> Utafiti huo umetokana na kesi ambazo zimeripotiwa na wahusika wamepatikana na hatia

> Zaidi ya theluthi ya waliouawa walijaribu kuachana na wapenzi wao. Wengi waliouawa wana umri kati ya 25-34

Zaidi, soma https://jamii.app/WanawakeKuuawa
DIDIER DROGBA ADAIWA KUONDOLEWA KATIKA NAFASI YA MSHAURI WA RAIS WA CAF

- Inadaiwa amefukuzwa kwa kushindwa kutimiza majukumu yake chini ya Rais wa CAF, Ahmad Ahmad

- Pia, inaelezwa kuwa hajawahi kushiriki tukio lolote la CAF tangu kuteuliwe kwake

Zaidi, soma https://jamii.app/DrogbaAfutwaKaziCAF
DAR: BEI YA GESI YA KUTUMIA MAJUMBANI YAPANDA

- Mtungi mdogo ulikuwa Tsh. 17,000 sasa ni Tsh. 22,000, mitungi mikubwa Tsh. 49,000 sasa ni Tsh. 50,000 hadi Tsh. 54,000

- Watumiaji wamesema ongezeko hili linaongeza ugumu wa maisha kwani vitu vingi vimepanda

Zaidi, soma https://jamii.app/BeiGesiMajumbani
UKRAINE: RAIA WASHAMBULIA MABASI YALIYOBEBA WATU WALIOONDOLEWA CHINA KUTOKANA NA CORONA

> Wakazi wa Novi Sanzhary wameshambulia mabasi yaliyobeba Raia takriban 70 waliotoka Wuhan

> Wamedai wanawekwa katika hatari ya kupata maambukizi

Zaidi, soma https://jamii.app/CoronaUkraine
RUVUMA: WAWILI WAFARIKI BAADA YA KUSOMBWA NA MAJI

> Watu wawili kutoka Kata ya matumbi wamesombwa na maji

> Mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha Mito kufurika na kuharibu miundombinu ya barabara na madaraja

Zaidi, soma https://jamii.app/VifoMvuaRuvuma
TAMBUA UMRI WA MATAIRI YA GARI LAKO ILI KUEPUSHA AJALI ZA KUPASUKA KWA TAIRI

> Muda wa matumizi ya matairi ni miaka 4 tangu kutengenezwa, Sio tangu ufunge kwenye gari

> Ukipita muda huo, tairi linakuwa katika hatari ya kupasuka wakati wowote

Zaidi, soma https://jamii.app/TairiZaGari