JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KASHFA YA LUGOLA: UCHUNGUZI WAKAMILIKA KWA 99.9%

- Ni kuhusu Mkataba wa Ununuzi wa vifaa vya Jeshi la Zimamoto wenye thamani ya zaidi ya Tsh. Trilioni 1 kinyume na sheria

- TAKUKURU imesema Ushahidi muhimu dhidi ya tuhuma hizo umepatikana

Zaidi, soma https://jamii.app/KashfaLugolaUchunguzi
MWENDELEZO: Waziri Mkuu wa Lesotho, Thomas Thabane, ameshindwa kufika Mahakamani kusikiliza kesi ya mauaji ya Mkewe wa kwanza, Lipolelo Thabane iliyofunguliwa dhidi yake

- Hata hivyo, Mwanaye Potlako Thabane amezungumza kwa njia ya simu na Shirika la Habari la Reuters na kusema Baba yake ameenda Afrika Kusini kuonana na Daktari
UTAMADUNI WA KUFUNGA KUFULI NA KUITUPA FUNGUO BAHARINI ILI KUTUNZA NDOA

> Baadhi ya nchi zilizoendelea, watu wakishatoka kufunga ndoa hununua kufuli jipya lenye majina yao na kisha huenda kulifunga kwenye madaraja maalum kwa wanandoa na funguo hutupwa baharini

> Iwapo mtataka kuachana basi mtalazimika kuitafuta funguo yenu ndani ya maji ili mufungue kufuli kuonyesha mmeachana. Msipofanikiwa mtalazimika kurudisha mapenzi na kusahau kuhusu kutengana

Soma https://jamii.app/ViapoKutunzaNdoa
MBUNGE WA TANDAHIMBA KUPITIA CUF AJIUZULU NA KUJIUNGA CCM

- Mbunge wa Tandahimba (CUF), Katani Katani amejiuzulu Ubunge wake na kujiunga CCM

- Amepokelewa na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally aliyeanza ziara ya siku 3 Mkoani Mtwara

Zaidi, soma https://jamii.app/MbungeTandahimbaAjiungaCCM
UGANDA: NZIGE WATUMIKA KAMA CHAKULA

> Wakazi wa Kijiji cha Kitgum wanawakamata Nzige hao waliovamia Uganda mnamo Februari 18, 2020

> Hata hivyo, Serikali imeanza kunyunyizia dawa na raia wameonywa juu ya kuwakamata nzige maeneo yaliyopigwa dawa

Zaidi, soma https://jamii.app/NzigeWaliwaUganda
ARUSHA: TAKUKURU YAFANIKIWA KUOKOA HELA ZILIZODAIWA KUPOTEA KIMAZINGARA

> Fedha hizo za Kikundi cha Ujasiriamali cha Imani zilidaiwa kupotea kimazingara nyumbani kwa Mweka Hazina

> TAKUKURU ilimkamata Mweka Hazina huyo kwasababu za kiupelelezi na sasa ameanza kuzirejesha ambapo tayari amekabidhi Tsh. Milioni 23

Zaidi, soma https://jamii.app/TAKUKURUMil43
MAREKANI NA TALIBAN KUSAINI MAKUBALIANO YA KUSITISHA MAPIGANO

- Utiwaji saini wa makubaliano ya Amani kati ya Marekani na Taliban utafanyika
Februari 29, 2020 huko Doha, Qatar

- Kisha Marekani itaanza kuviondoa vikosi vyake huko Afghanistan

Zaidi, soma https://jamii.app/Makubaliano-USATaliban
UNADHANI KWANINI WASOMI WENGI HAWAFANIKIWI KWENYE MUZIKI?

> Baadhi ya wasomi hufanya muziki kujiajiri ila inadaiwa achache hufanya vizuri

> Moja ya sababu iliyotajwa ni kuwa Wasomi hutunga mashairi magumu huku wasikilizaji wakitaka mepesi

Kujadili, tembelea https://jamii.app/WasaniiWasomi
K-LYINN ADAI KUZUIWA KUINGIA KWENYE KABURI LA MENGI

- Mke wa Marehemu Regnald Mengi, Jacqueline Mengi (K-Lyinn) amedai kuzuiwa kuingia kwenye kaburi la mumewe hadi aombe ruhusa

- Amedai kuwa amenyamaza kwa mengi, amechoka, hatakaa kimya wala hatokubali kuona Wanaye wakisononeka

Zaidi, tembelea https://jamii.app/KlyinnAzuiwaKaburiMengi
MAREKANI: MSHAURI WA ZAMANI WA TRUMP AHUKUMIWA MIEZI 40 JELA

> Roger Stone alishtakiwa kwa makosa 7, yakiwemo ya kulidanganya Bunge na kuvujisha ujumbe wa barua pepe

> Rais Trump amesema anatamani kuona anasamehewa adhabu hiyo

Zaidi, soma - https://jamii.app/RogerStoneHukumu-US
NAMNA YA KUPIKA DAGAA WA KIGOMA KWA NYANYA CHUNGU NA NAZI

> Weka mafuta kwenye sufuria, kaanga dagaa halafu weka ndimu katia kitunguu, kaanga kiive weka nyanya, hoho na karoti

> Weka nyanyachungu na maji kidogo, kisha tui la nazi

Zaidi, tembelea https://jamii.app/MapishiDagaa
GEITA: BABA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUMLAWITI MTOTO WAKE WA KAMBO

> Kazimili Dotto atuhumiwa kumlawiti mtoto wake anayesoma darasa la pili

> Inadaiwa Februari 17, Mshtakiwa alimwita mtoto huyo na kumwomba amletee maji ya kunywa chumbani kwake na kisha kumlawiti

Zaidi, soma https://jamii.app/MtotoAlawitiwa
FAHAMU FAIDA NA NAMNA YA KUTENGENEZA ‘SCRUB’

> Weka Sukari, asali ikifuatiwa na maji ya ndimu kisha changanya

> Weka unga wa majani ya chungwa, kisha mafuta ya mzeituni na changanya vizuri

> Faida zake ni pamoja kufanya ngozi iwe ang'avu

Zaidi, tembelea https://jamii.app/KutengenezaScrub
JE, NI KWELI HAKUNA UTAJIRI WA HALALI?

> Mdau wa JamiiForums anadai lazima uwe mkwepa kodi, ununue hata magendo ili usitetereke kiuchumi

> Anaeleza kuwa ukiwa tajiri ili kuficha mabaya yako, utairudia jamii kwa kutoa sadaka na misaada

Kujadili, tembelea https://jamii.app/HakunaUtajiriHalali
MKAPA: MIHULA MIWILI YA URAIS NI KAMA UTAMADUNI WA TAIFA, MAGUFULI HAWEZI KUONGEZA

> Anaamini Rais Magufuli hawezi kuongeza mihula, hata yeye alipokuwa Rais, wazee wa Zanzibar walimuomba kuwe na mihula mitatu lakini aliwakatalia

Soma https://jamii.app/MkapaMagufuliMihula
#JFLeo
ZANZIBAR: KOCHA AFUNGIWA MIEZI SITA BAADA YA KUSHUSHA SURUALI KUSHANGILIA USHINDI

> ZFF imemfungia na kumpiga faini ya Tsh. 500,000 Suleiman Mohamed aliyeshangilia kwa kushusha suruali chini na kubaki na nguo ya ndani mbele ya mashabiki

Soma https://jamii.app/KochaNguoUwanjani
KENYA: MKE AACHIKA, BINTIYE AOLEWA NA ALIYEKUWA MUMEWE (BABA MLEZI)

> Ndoa yao ilivunjika baada ya mumewe kumuoa binti yake wa kwanza

> Binti huyo ana mtoto wa miaka mitatu ambaye amezaa na baba yake mlezi

Zaidi, soma https://jamii.app/BabaAmuoaMwanae
SAUDI ARABIA: MSANII WA KIKE ATAFUTWA KWA KUTOA VIDEO YA KUWASIFU WANAWAKE WA MAKKA

> Gavana wa Makka aliagiza waliofanya video hiyo wakamatwe kwa kuwa inatukana utamaduni wao

> Akaunti ya YouTube ya Asayel Slay imefungwa na video imefutwa

Zaidi, soma https://jamii.app/MwanamuzikiAtafutwa
KURA YA MAONI: TRUMP ANG’ARA, AONYESHA DALILI ZA KUWEZA KUREJEA MADARAKANI

> Akubalika kwa 49% huku akiwa na 48% zinazomkataa

> Kura hii inampa nafasi kubwa Trump kuweza kutetea kiti cha Urais nchini Marekani

Soma https://jamii.app/TrumpAkubalikaKuraMaoni
👍1