JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAREKANI YAITAKA AFRIKA KUWA MAKINI NA SERIKALI ZENYE AHADI ZA MANENO MATUPU

> Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo amesema uhusiano wa kiuchumi na kibiashara na Marekani ndio njia ya Afrika kujikomboa kiuhalisi

> Inadaiwa dhumuni la Marekani ni kupunguza ushawishi wa uwekezaji wa China barani Afrika

Soma - https://jamii.app/USChinaAidsAfrika
#JFLeo
NJOMBE: AFARIKI DUNIA KWA KUPIGWA NA RADI, ALIOKUWA NAO WABAKI SALAMA

> Martin Nyigu (35) amepigwa na radi Februari 23, 2020 majira ya saa 9 alasiri akiwa saluni huku kinyozi na wateja waliokuwa wanasubiri huduma wakitoka salama

Soma https://jamii.app/RadiYauaNjombe
UPDATE: Idadi ya Watu waliofariki dunia kutokana na #CoronaVirus imefikia 2,619 huku vifo 27 vikiwa vimetokea nje ya Ardhi Kuu ya China (Mainland China)

- Aidha, Watu 79,356 Ulimwenguni wameambukizwa virusi hivyo huku Waathirika 24,734 wa China wakiruhusiwa kutoka hospitalini
AFYA: UNASHAURIWA KUTOFANYA HAYA MARA BAADA YA KUMALIZA KULA

> Kulala: Unashauriwa kusubiri angalau saa 2 kabla ya kulala ili kuepuka kupata ugonjwa wa mshtuko

> Kuvuta sigara: Kuvuta sigara mara baada ya kula ni hatari sawa na madhara yanayotokea kwa mtu aliyevuta sigara 10 kwa mara moja

> Kuoga: Kuoga mara baada ya kula kunasababisha kuongeza kasi ya mzunguko wa damu kwenye miguu na kupunguza kasi ya mzunguko wa damu tumboni ktk mmeng’enyo wa chakula

Zaidi, soma - https://jamii.app/DontsAfterMeal
WANAOHAMIA NDANI YA CCM WATAKIWA KUTOANZISHA MAKUNDI NDANI YA CHAMA

> Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally, amewataka wanachama ambao walikihama chama hicho na hivi sasa wameamua kurejea wasiwe chanzo cha kuanzisha makundi ndani ya chama

> Amesema CCM siku zote haina utamaduni wa kuishi kwa makundi hivyo wasiruhusu tabia ya uwapo wa makundi

Soma - https://jamii.app/MakundiCCM
HOJA: SHERIA MPYA YA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII INAUA NDOTO ZA VIJANA

> Mdau anadai, Kwa udogo wa mishahara vijana hutegemea ile 20% ya mshahara inayopelekwa PSSSF

> Kijana hutegemea achukue hela hiyo baada ya miaka 5 ili akajiajiri, lakini Sheria inataka uichukue ukiwa na miaka 55

> Amehoji mbona Wabunge hawajapitisha Sheria ya namna hii kwenye kiinua mgongo chao?

Soma https://jamii.app/MifukoYaHifadhi
KABENDERA AKIRI MAKOSA, DPP ARIDHIA

- Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ameridhia maombi ya Mwanahabari Erick Kabendera kukiri mashtaka yake na kuomba msamaha

- Aidha, DPP amewasilisha hati ya kuiruhusu Mahakama ya Kisutu kusikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Erick

Zaidi, soma https://jamii.app/DDPAridhiaMaombiKabendera
MBEYA: MADIWANI 11 WA CHADEMA WAJIUNGA CCM

- Katibu Mkuu wa CCM, Bashiru Ally amesema Madiwani 10 kati yao ni wa Kuchaguliwa na Mmoja ni wa Viti Maalumu

- Pia amesema, timu hiyo inaongozwa na Meya ikiwa na Viongozi Watatu wa Juu wa CHADEMA

Zaidi, soma https://jamii.app/Madiwani11CDM-CCMMbeya
KOREA KASKAZINI YAHOFIA KUPATA MAAMBUKIZI YA #CORONA

> Korea Kaskazini imewaweka kwenye karantini raia 380 wa kigeni walioingia nchini humo, ikiwa ni moja ya njia za kuzuia maambukizi ya #coronavirus

> Wengi wa raia hao wa kigeni ni Wanadiplomasia. Awali, raia wengine wa kigeni zaidi ya 200 waliwekwa kwenye karantini kwa muda wa siku 30 na baadaye kuruhusiwa baada ya kubainika kuwa hawana #coronavirus
KISUTU, DAR: KABENDERA AACHIWA HURU

- Mwandishi Erick Kabendera ameachiwa huru huku akitakiwa kulipa fidia kwa makosa yake yote mawili

- Ametakiwa kulipa Tsh. 250,000 au kifungo cha Miezi 3, adhabu inayoambatana na fidia ya Tsh. Milioni 172 kwa kushindwa kulipa kodi

- Katika kosa la pili, Mahakama imemtaka Erick Kabendera kulipa faini ya Tsh. Milioni 100 kama adhabu kwa kosa la Utakatishaji

Zaidi, soma https://jamii.app/DDPAridhiaMaombiKabendera
DODOMA: BINTI AMSHTAKI BABA YAKE KWA KUSHINDWA KUMPA MAHITAJI YA SHULE

> Tangu shule zifunguliwe amekuwa akisubiria sare na madaftari ili aanze kidato cha kwanza

> Wazazi wake walitengana na kugawana majukumu, lakini hakuna aliyetimiza majukumu yake

Soma https://jamii.app/MtotoAmshtakiMzazi
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: DKT. MASHINJI AHUDHURIA KESI KISUTU, AKUTANA NA VIONGOZI WA CHADEMA

- Dkt. Vincent Mashinji aliyehama CHADEMA na kujiunga CCM, amekutana na Viongozi CHADEMA leo Mahakamani

- Katika kesi hiyo, Mahakama imepanga kutoa hukumu Machi 20, 2020

Zaidi, soma https://jamii.app/MashinjiVsCDM-Mahakamani
ZIJUE HAKI MUHIMU ZA MTOTO

> Haki ya Kuishi: Hii inaanza pale mama anapopata ujauzito. Pia kuishi kwa mtoto baada ya kuzaliwa kunategemea upatikanaji wa mahitaji ya msingi

> Haki ya Kulindwa: Inahusu kuzuia vitendo viovu wanavyofanyiwa watoto katika hatua za ukuaji wao. Mtoto anahitaji ulinzi dhidi ya kazi nzito zisizowiana na umri wake, kudhulumiwa mali hasa kwa watoto yatima, kutupwa au kutelekezwa na wazazi

Tembelea - https://jamii.app/HakiMtotoTZ
KABENDERA ALIPA MILIONI 100, ATAKIWA KUMALIZIA KULIPA KWA MIEZI 6

- Mwanahabari Erick Kabendera ameachiwa baada ya kulipa faini ya Tsh. 250,000 na fidia ya Tsh. Milioni 100

- Alitakiwa kulipa fidia ya Tsh. Milioni 172 kwa Kukwepa Kodi na Tsh. Milioni 100 (aliyoilipa) kwa Kutakatisha fedha na faini ya Tsh. 250,000 (aliyoilipa)

Zaidi, soma https://jamii.app/DDPAridhiaMaombiKabendera
MAFIA, PWANI: WAVUVI WAOMBA WAKE ZAO KURUDISHWA KISIWA CHA NYORORO

> Wiki iliyopita, Mkuu wa Wilaya ya Mafia mkoani Pwani, Shaibu Nunduma aliamuru wanawake wote waondoke kwenye Kisiwa cha Nyororo ili wabaki wanaume, pia alitaka wanaume watakaoishi kisiwani hapo wawe ni wavuvi 100 kwa awamu tofauti

Soma https://jamii.app/WavuviWaombaWake
UJUE MMEA VETIVER KATIKA KUTUNZA MAZINGIRA

> 'Vetiver' ni aina ya nyasi ndefu zenye majani marefu. Mizizi yake ina uwezo wa kwenda mita 2 - 4 chini ya udongo

> Mizizi yake ina uwezo kuzuia mmomonyoko wa udongo. Upandaji wa mimea hii ni njia salama ya kutunza mazingira

Soma https://jamii.app/VertiverMazingira
UGANDA: WAPENZI WADAI FIDIA YA TSH. MILIONI 376 KWA KANISA BAADA YA KUFUTA NDOA YAO

> Wamedai fidia ya Tsh. milioni 376 kwa kanisa la ‘Church of Uganda’ baada ya kufuta ndoa yao iliyogharimu takriban Tsh. milioni 471 kuiandaa

Zaidi, soma https://jamii.app/WanandoaWadaiFidia
FAHAMU NAMNA YA KUDHIBITI HASIRA KWENYE MAPENZI

> Kama jambo limekuudhi kupita kiasi, badala ya kufoka, kupiga kelele hadi majirani wakasikia, jaribu kutuliza kwanza akili yako kwa kujipa muda wa kuvuta pumzi ndipo useme unachotaka kusema

> Endapo wenza wakiona ugomvi kati yao umekuwa mkubwa na hakuna maelewano, ni vyema mmoja wao akaondoka eneo husika ili kutoa muda kwa kila mmoja kutafakari juu ya kilichotokea

Zaidi, tembelea https://jamii.app/HasiraMapenzi
MAPAMBANO DHIDI YA #CORONA YAANZA KUZAA MATUNDA, MAAMBUKIZI MAPYA YAPUNGUA KWA 80%

> Wataalamu kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), wamesema wiki 2 zilizopita China, kila siku wagonjwa wapya zaidi 2,000 waliripotiwa lakini idadi ya wagonjwa waliothibitishwa jana ilikuwa 416, ambayo imepungua kwa 80%

> Hatua zinazochukuliwa na China kuhamasisha Serikali na watu wote katika jamii kupambana na #coronavirus, zimezuia maelfu ya wagonjwa wapya kutokea

#JFLeo
MHTF: WATU MILIONI 50 DUNIANI WANA MATATIZO YA UZAZI

> Katika tamaduni nyingi wanawake hubeba lawama mara baada ya mahusiano kushindwa kuleta watoto

> Hali hii husababisha wanawake kutengwa, waume zao kuoa wake wengine na hata ndoa kuvunjika

Soma https://jamii.app/MatatizoYaUzazi