JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MIZENGO PINDA: WATOTO WASIDANGANYWE KWAMBA KUNA AJIRA

> Waziri Mkuu Mstaafu ameishauri Serikali kubadilisha mfumo wa elimu nchini ili kuwaandaa vijana katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira

> Amesema ajira ni chache sana

Zaidi, soma https://jamii.app/PindaMfumoElimu
KISUTU, DAR: KIZIMBANI KWA KULAWITI NA KUSAMBAZA VIDEO ZA NGONO

- 'Video Vixen', Aisha Juma anadaiwa kusambaza video za ngono huku akijua ni kosa

- Samwel Philemon anadaiwa kumuigilia kinyume na maumbile Mshtakiwa Aisha huku akijua ni kosa

Soma - https://jamii.app/KizimbaniKusambazaVideoNgono
DKT. VINCENT MASHINJI ATIMKIA CCM

> Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, amefika ofisi ndogo za CCM, Lumumba na kuomba nafasi ya kujiunga na CCM

> Asema ametafakari kwa kina na amebaini CHADEMA haijajizatiti kuleta maendeleo kwa wananchi kama CCM

Soma https://jamii.app/MashinjiKuamiaCCM
UGANDA: WATOTO WAWILI WAFARIKI, WENGINE 11 WALAZWA BAADA YA KULA VIBAMA/MABUMUNDA YENYE SUMU

> Watoto hao wa familia moja walipika vitafunwa hivyo na kutumia dawa ya kuua wadudu wakidhani ni mafuta ya kula

> Polisi wanachunguza kisa hicho

Soma - https://jamii.app/WatotoSumuUganda
CHINA KUSAFISHA PESA ILI KUKABILIANA NA MAAMBUKIZI YA #CORONA

> Benki Kuu imesema itasafisha, kutibu na kuharibu fedha ikiwa ni njia ya kuzuia ueneaji wa #coronavirus

> Pesa zinazotoka ktk maeneo hatari kama hospitali na sokoni zitaharibiwa

Soma https://jamii.app/FedhaCorona
SHERIA YA ULINZI WA DATA KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

> Nchi za Kenya na Uganda zilipitisha Sheria ya #UlinziWaData ikiwa ni hatua ya kuhakikisha Mataifa na Wananchi wao wanapata haki ya Faragha na Ulinzi wa Data

> Mpaka sasa Tanzania haina Sheria mahususi kwa ajili ya #UlinziWaData ingawa zipo tetesi kuwa Serikali imeandaa Muswada wa Sheria hiyo utakaowasilishwa Bungeni

> Sheria hii itasaidia kuweka muongozo wa namna taarifa za watu zitakuwa Zikikusanywa, Kutunzwa na Kutumika. Mchakato wa sheria hii umekwama wapi kwa #Tanzania?

Zaidi, soma > https://jamii.app/EADataProtection

#DataProtection #UlinziWaData
MAKETE: WANANCHI WAMTUHUMU MWANAKIJIJI MWENZAO KUWAINGILIA WANAWAKE (KIMWILI) KISHIRIKINA

> Wananchi wa kitongoji cha Ikonda Bondeni wamemfukuza Mateso Mbilinyi wakimtuhumu kuwaingilia kimwili kwa njia ya ushirikina baadhi ya wanawake wa kitongoji hicho huku akipita mtaani na kujisifia kwa vitendo hivyo

> Mateso anadaiwa kuhamia eneo hilo akitokea kijiji cha Ilevelo kwa tuhuma hizohizo

Soma - https://jamii.app/UshirikinaNgono
SAMAKI ANAYETUMIA UMEME KUJIHAMI, WENGI HUDHANI NI CHUNUSI

> Samaki Mkunga anaweza kuzalisha Volts 650 na pigo lake 1 linatosha kumfanya mtu akose nguvu na kuzama

> Anaweza kukua hadi kufikia urefu wa Mita 1.8 na anaishi kwenye maji baridi

Zaidi, soma https://jamii.app/ElectricEel
SIMIYU: ZAIDI YA NG’OMBE 1,400 WADAIWA KUFA MIKONONI MWA MAAFISA WA PORI

> Walikamatwa 2017 walipokuwa ndani ya pori la akiba. Mahakama iliamuru warudishwe kwa wafugaji lakini waliendelea kushikiliwa

> Baadhi ya ng'ombe wa thamani ya laki 5 waliuzwa kwa laki 1

Soma https://jamii.app/NgombeWafaSimiyu
RWANDA: SHIRIKA LA HAKI ZA BINADAMU LATAKA KIFO CHA KIZITO MIHIGO KUCHUNGUZWA

> Mkurugenzi wa Shirika hilo Kanda ya Afrika ya Kati amesema wana mashaka na kifo chake na hii sio mara ya kwanza mtu kufariki katika mazingira ya kutatanisha akiwa chini ya Ulinzi wa Polisi

Soma - https://jamii.app/UchunguziKifoKizitoMihigo
KAGERA: ALIYEKUWA KIONGOZI WA UVCCM AKUTWA AMEFARIKI DUNIA

Mwili wa Jaspar Jasson, umekutwa pembeni ya barabara ukiwa na alama shingoni

> Polisi wamesema uchunguzi wao umebaini kuna dalili zote za marehemu kujinyonga kwani mwili ulikuwa na michubuko shingoni

Soma https://jamii.app/AkutwaAmekufa
GHANA: WAHADHIRI 2 WASIMAMISHWA KAZI KWA TUHUMA ZA UNYANYASAJI WA KIJINSIA

> Video iliyochukuliwa kisiri ilionyesha matukio yao lakini wote wamekana madai hayo

> Prof. Gaympo amesimamishwa miezi sita na Dkt. Butakor miezi minne, bila mshahara

Zaidi, soma https://jamii.app/UnyanyasajiKijinsia
UPDATE: Idadi ya vifo kutokana na #CoronaVirus imefikia 2,004, huku idadi ya maambukizi ikiongezeka hadi 74,185

- Hong Kong imeripoti kifo cha pili kutokana na maambukizi ya Virusi hivyo

- Aidha, Mamlaka za Urusi zinazosimamia uthibiti wa Virusi ya Corona zimesema Raia wa China hawataruhusiwa kwa muda kuingia nchini humo kuanzia Februari 20 2020
10% UNAYOLIPA SERIKALI ZA MTAA WAKATI WA MANUNUZI YA NYUMBA/KIWANJA HAIPO KISHERIA

> 10% ni rushwa kwa kuwa haipo kisheria na haitolewi risiti. Fedha yoyote inayotolewa bila aliyetoa kupewa risiti ni fedha ambayo ina ufisadi ndani yake

> Kifungu cha 10 cha Sheria ya Mikataba kimesema mkataba unaokubalika kisheria ni ule uliofanywa kwa hiari huru, wahusika wenye sifa, malipo halali na mali halali

Soma zaidi https://jamii.app/Asilimia10SMZ
SUDAN KUSINI YAKUMBWA NA UVAMIZI WA NZIGE

> Waziri wa Kilimo, Onyoti Adigo, amesema Nzige wameonekana katika jimbo la Equatoria karibu na mipaka ya Ethiopia, Kenya na Uganda

> Amesema Mamlaka zitajaribu kuwadhibiti

Zaidi, soma https://jamii.app/NzigeSudaniKusini
HATUA ZA KUSAJILI BIASHARA YAKO KUWA KAMPUNI

> Chagua jina: Kampuni lazima iwe na jina linalotambulika na linalojitofautisha na majina ya makampuni mengine nchini

> Andaa Waraka na Katiba ya Kampuni: Wasilisha kwa Msajili waraka wa kampuni na katiba ya kampuni na Waraka huu lazima uwe na mhuri wa mwanasheria.

> Jaza fomu 14a&14b zinazopatikana kwenye tovuti ya BRELA. Fomu hiyo itajazwa na mmoja wa Wakurugenzi wa kampuni na itatiwa muhuri na Wakili

Zaidi, soma https://jamii.app/KusajiliKampuni
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
KESI NA. 456 (JAMHURI v JAMIIFORUMS): HUKUMU YAAHIRISHWA KWA MARA YA NNE

> Awali ilipangwa kutolewa Novemba 26, 2019 ikapangwa tena kutolewa Disemba 06, 2019; baadae ikapangwa kutolewa Jan 22, 2020 kisha ikapangwa kutolewa leo Feb 19, 2020. Sasa itasomwa Aprili 2, 2020

> Shauri hili limeanza kusikilizwa mwezi Disemba 2016 na miongoni mwa mashauri 3 yaliyofunguliwa wakati huo. Moja liliisha Juni 2018 baada ya washtakiwa kukutwa hawana kesi ya kujibu. Shauri jingine linaendelea chini ya Hakimu Shaidi na litatajwa Feb 27
MAGEREZA YATAKIWA KUANZA KUJITEGEMEA KWA CHAKULA

- Kamishna wa Magereza, Suleiman Mzee amewataka Wakuu wa Magereza Nchini kujitegemea kwa chakula cha Wafungwa na huduma nyingine

- Amewataka kufanya hivyo kuanzia Machi 1, 2020 akisema Jeshi hilo lina fursa za kuweza kujitegemea
YA KUZINGATIA UNAPOENDA KUONGEA/KUWATEMBELEA WATEJA

> Usimpotezee muda na andaa kufikisha ujumbe kwa dk 3. Kama mteja hataki kuzungumza nawe panga kukutana naye siku nyingine

> Kuwa msikivu na hakikisha kila taarifa anayokupatia unaihifadhi

Zaidi, soma https://jamii.app/BiasharaMauzo
UMOJA WA MATAIFA: ULIMWENGU UMESHINDWA KULINDA KIZAZI KIJACHO

> Ripoti ya UN imesema Ulimwengu umeshindwa kulinda Watoto dhidi ya hatari za kiafya, lishe hafifu na mabadiliko ya tabia nchi

> Mtoto 1 kati ya Watoto 10 havuti hewa safi

Zaidi, soma - https://jamii.app/RipotiWatotoUN