JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KENYA: AL-SHABAAB WATUHUMIWA KUUA WATU WATATU

> Watu watatu wameuawa na wengine watano kujeruhiwa katika shambulio lilitokea Februari 19, 2020 la watu wanaodhaniwa kuwa ni Al Shabaab katika kaunti ya Mandera

Zaidi, soma https://jamii.app/WatatuWauawaKenya
MAREKANI: VIFUSI VYA UCHAFU, VYUMA VYAKUTWA NDANI YA TENKI ZA MAFUTA ZA NDEGE ZA BOEING 737

> Inadaiwa kuwa vifusi hivyo vya uchafu, vyuma na vifaa vingine viliachwa katika matenki ya mafuta wakati ndege zinaunganishwa

Zaidi, soma https://jamii.app/Boeing737Max
SHINYANGA: AFARIKI KWA KUNYWA POMBE KUPITA KIASI

- Nkuba Mawe (27) amekutwa amefariki kwenye vibaraza vya maduka katika mtaa wa Dome, Ndembezi

- Uchunguzi wa Daktari umebainisha kuwa hajafariki kwa kupigwa bali kwa kunywa pombe kupita kiasi

Zaidi, soma https://jamii.app/PombeNyingiYamuua
UGANDA: MKE WA RAIS MUSEVENI AITWA BUNGENI

> Spika Rebecca Kadaga ametoa wito wa mwisho kwa Janet Museveni, ambaye ni Waziri wa Elimu kufika Bungeni baada ya kutokea mkanganyiko wa kuanza kutumika kwa mtaala mpya wa Elimu ya Sekondari

Zaidi, soma - https://jamii.app/JanetMuseveniBunge-UG
WAFANYAKAZI WASIO NA UJUZI HATARINI KUNYIMWA VIZA KUINGIA UINGEREZA

> Viza zitatolewa kulingana na ujuzi, kiwango cha elimu, mshahara au taaluma

> Atakayetimiza vigezo atapewa alama 50. Ni lazima kufikisha 70 ili uweze kufanya kazi Uingereza

Zaidi, soma https://jamii.app/WasioNaUjuzi
KISUTU, DAR: MKANDARASI AFUNGWA JELA MIAKA 7 KWA UDANGANYIFU WA FEDHA

- Mkandarasi wa majengo, Alfred Ndeka (60) amehukumiwa kwa kujipatia Tsh. Milioni 116 kidanganyifu

- Ni baada ya kutolewa kwa ushahidi wa mashahidi 5 na vielelezo 11

Zaidi, soma https://jamii.app/MkandarasiJelaMiaka7
KENYA: KIJANA AJIANDIKIA R.I.P KABLA YA KUJIUA

> Dennis Yego (24) alimchoma kisu mkewe mara kadhaa na kisha kujinyonga

> Jumatatu 2:05 usiku, kupitia Facebook aliandika “Rest in peace to me.” Baadae akaandika, “kama unanidai nione kabla ya mchana wa kesho”

Zaidi, soma https://jamii.app/AjiandikiaKifo
NG’OMBE MWENYE REKODI YA PEMBE NDEFU

> Ng’ombe anayeitwa Poncho Via ameingia kwenye rekodi ya kuwa na pembe ndefu kuliko wote

> Pembe zake ukizipima kutoka mwisho wa pembe moja hadi pembe nyingine zinakuwa na urefu sm 323.74 sawa na mita 3.2

Zaidi, soma https://jamii.app/PembeNdefu
WAZIRI SIMBACHAWENE AWATAKA WATENDAJI WAKUU WA POLISI KUWAHOJI MAHABUSU

> Awataka Watendaji Wakuu wa Jeshi la Polisi wawahoji watuhumiwa waliopo mahabusu ya vituo vya Polisi

> Asema lengo la agizo hilo ni kudhibiti ubambikizwaji kesi ambao upo katika vituo mbalimbali nchini

Soma https://jamii.app/SimbachawenePolisi
POMPEO AONYA MPANGO WA SERIKALI YA AFRIKA KUSINI KUCHUKUA ARDHI BILA KULIPA FIDIA

> Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo amesema mpango huo ni hatari kwa uchumi wa nchi

> Asilimia 72 ya mashamba Afrika Kusini yanamilikiwa na Wazungu

Zaidi, soma https://jamii.app/PompeoSouthAfrica
FAHAMU HAYA KUHUSU FIMBO YA MZEE DANIEL ARAP MOI

> Ilitengenezwa kwa pembe za ndovu na dhahabu na kuitwa 'Fimbo ya Nyayo'

> Ilikuwa ishara ya nguvu, uongozi na mshikamano wa Kitaifa

> Moi hakuwahi kutokea katika kazi yoyote bila fimbo hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/FimboYaNyayo
UPDATE: Tume ya Afya ya China imeripoti kuwa maambukizi ya #coronavirus yamepungua kutoka maambukizi 1,749 kwa jana hadi maambukizi 394 kwa siku ya leo

- Idadi ya vifo kwa sasa imefikia 2,126 huku vifo 10 vikiwa vimetokea nje ya ardhi Kuu ya China (Mainland China). Idadi ya Waathirika wa virusi hivyo imefikia 75,600 Ulimwenguni

- Maambukizi makubwa nje ya China yapo Nchini Korea Kusini (82), Singapore (84) na Japan (68) bila kuehesabu Waathirika 624 waliothibitika katika Meli ya Diamond Princess
RAIS MAGUFULI AKUTANA NA MADAKTARI WA TANZANIA

- Rais anakutana na Chama cha Madaktari Nchini katika Mkutano unaoendelea kwenye Ukumbi wa JNICC

- Mkutano huo unafanyika kuelekea maadhimisho ya miaka 55 ya Chama cha Madaktari Tanzania

Fuatilia https://jamii.app/RaisMadaktariTanzania
ETHIOPIA: WANAWAKE ZAIDI YA 50 HUSHAMBULIWA NA TINDIKALI KILA MWAKA

> Tafiti zimebainisha zaidi ya theluthi moja ya Wanawake walio kwenye mahusiano hunyanyaswa

> Moja ya unyanyasaji uliomkuta Atsede Nguse, ni kumwagiwa tindikali na mumewe

Soma https://jamii.app/TindikaliEthiopia
JACKSON MAKWETA: KIONGOZI WA KWANZA KUSHAURI MATUMIZI YA KISWAHILI KATIKA NGAZI ZOTE ZA ELIMU

> Mwaka 1982, Tume ya Makweta ilitoa mapendekezo hayo ili kuboresha mfumo wa elimu

> Alikuwa Waziri wa Elimu wa Serikali ya Awamu ya Kwanza

Soma https://jamii.app/JacksonMakweta
UJERUMANI: WATU 9 WAUAWA KATIKA SHAMBULIO LA RISASI

- Limetokea jana usiku katika baa 2 za kuvutia shisha ndani ya Mji wa Hanau

- Katika baa ya kwanza watu 3 waliuawa na katika baa ya pili watu 5 waliuawa. Mmoja amefariki akiwa hospitalini

Soma https://jamii.app/ShambulioRisasiWatu9Wafariki
KENYA: DADA WATANO WAMPIGA KAKA YAO HADI KIFO KISA MBUZI WA MAHARI

> Paul Njeri (51) alipigwa na dada zake baada ya kudai apewe mbuzi wa mahari

> Dada zake walimpiga na walipokuja kumuangalia asubuhi yake walikuta ameshafariki

Soma - https://jamii.app/SistersKillBrotherOverDowry
KENYA: BINTI WA MIAKA 13 AHUSISHWA NA MAUAJI YA MTOTO WA MIAKA 5

> Siku ya Ijumaa wawili hao walienda katika mto ulio karibu na kwao, baadaye binti huyo alirejea nyumbani peke yake

> Lakini pia, alitoroka nyumbani kwao usiku wa tukio hilo

Soma https://jamii.app/Binti13Atafutwa
ALIYEGUNDUA MFUMO WA 'CUT-COPY-PASTE' AFARIKI DUNIA

> Mtaalamu wa Kompyuta, Lawrence 'Larry' Tesler (74) amefariki dunia. Chanzo cha kifo chake hakijawekwa wazi

> Mwanasayansi huyo amewahi kufanya kazi na Makampuni ya Apple, Amazon na Yahoo

Zaidi, soma - https://jamii.app/LawrenceTeslerDead
WADHAMINI WA TUNDU LISSU WAWASILISHA MAOMBI YA KIBALI CHA KUMKAMATA

> Awali Mahakama ilitaka kuwakamata wadhamini hao baada ya kushindwa kumpeleka Lissu Mahakamani hapo

> Lissu anakabiliwa na Kesi ya Uchochezi na yuko Ubelgiji alikokwenda kwa matibabu

Zaidi, soma https://jamii.app/WadhaminiKibaliMbowe