JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
14/2/2020 NI SIKU YA KUMKUMBUKA KONDOO DOLLY KAMA KIUMBE WA KWANZA KUUNDWA KWA NJIA YA REPRODUCTIVE CLONING

> Ametokea kwa Mama watatu, mmoja alitoa yai, wa pili alitoa DNA, wa tatu akabeba mimba hadi akazaliwa 5/7/1996. Alikufa 14/2/2003

> Alipewa jina la Dolly kwa heshima ya Mwanamuziki Dolly Parton

Soma https://jamii.app/KondooMaarufu
USHAURI: FANYA HAYA KAMA BREKI ZITAFELI UKIWA KWENYE MWENDO

> Usiwe na hofu. Washa ‘double hazard’ kuwajulisha madereva wenzio una tatizo. Kwa 'Automatic' weka gari kwenye gia ndogo (L), kwa 'Manual' shusha gia mpaka 1

> Washa kiyoyozi (AC) mpaka mwisho. Washa taa zote na kila kitu itafanya umeme mwingi utumike na kuipunguzia nguvu gari. Tafuta eneo salama kugongesha gari lako, unapogongesha lenga upande wa kushoto

Soma https://jamii.app/GariBreki
KENYA: MUUMINI AKAMATWA AKIIBA SADAKA KANISANI

> Peter Muiya Irungu anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuiba sadaka Kanisani

> Kanisa limeshangazwa na kitendo hicho kwakuwa Irungu ni Muumini ambaye hajawahi kukosa ibada hata siku moja

Soma - https://jamii.app/ChurchBurglaryKenya
MKURUGENZI WA WILAYA ANYIMWA MSHAHARA KWA KUSHINDWA KUJIBU MASWALI

> Mkurugenzi wilaya ya Mwanga, Zefrin Lubuva alishindwa kujibu kwanini Halmashauri hiyo imeshindwa kutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya Wanawake, Vijana na Walemavu

Soma https://jamii.app/MshaharaMkurugenzi
BURUNDI: MADUKA YOTE YA KUBADILISHIA FEDHA YAFUNGWA, BENKI KUHUSIKA KATIKA UBADILISHAJI

> Benki Kuu imetangaza kuyafunga maduka yote kwa madai kuwa wamiliki wamekuwa wakifanya shughuli zao kinyume na utaratibu uliowekwa na Serikali

> Kuanzia sasa Benki zote za kibiashara ndizo zitaruhusiwa kubadilisha fedha

Soma - https://jamii.app/BureauChangeClosed
PAKISTAN: APIGWA KWA KUONGEZA MKE BILA RUHUSA YA MKE WA KWANZA

> Asif Siddiqi, alipigwa kwa kutaka kufunga ndoa na mke wake wa tatu

> Ndoa za mitala zinakubalika lakini ni lazima apate idhini ya wake zake wa kwanza kabla ya kuoa tena

Soma https://jamii.app/KipigoHarusini
MAREKANI, TALIBAN ZAINGIA MAKUBALIANO YA KUPUNGUZA MACHAFUKO AFGHANISTAN

> Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Mark Esper, amesema wanaamini njia pekee ya kumaliza ghasia za Afghanistan ni kupitia maridhiano ya kisiasa

Soma - https://jamii.app/MarekaniTalibanMakubaliano
MTWARA: UBADHILIFU WA TSH. MILIONI 82 ZA VITAMBULISHO VYA WAFANYABIASHARA WABAINIKA

> Fedha hizo za mauzo ya vitambulisho hazijapelekwa Benki

> Waliendesha zoezi la ufuatiliaji wa fedha katika wilaya tatu za Masasi, Tandahimba na Mtwara

Soma https://jamii.app/TAKUKURURushwa
NIGERIA: SERIKALI YATUMIA MITANDAO YA SIMU KUWAKAMATA WANAHABARI

> Wanahabari, Samuel Ogundipe na Azeezat Adedigba wamekamatwa baada ya kufuatiliwa kupitia Mitandao ya Simu

> Hawakujua kuwa mawasiliano yao yanarekodiwa

Soma - https://jamii.app/NigeriaGvtSurveillance

#DataProtection #JamiiForums
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
ANDREW MSECHU (SPAC DAWG), KAMUSI YA MANENO YA ARUSHA

> Ni msanii anayefanya Kiswahili cha Arusha kiwe na maneno kama ‘Mafekeche’ ‘Fasi ya dwasi’, ‘Fyade’ ‘Yechu!Yechu!’

> Ana shahada ya Sheria. Anajulikana kama Kamusi ya Arusha

Soma https://jamii.app/SpacDawg
MPYA: Manchester City imefungiwa kushiriki mashindano yote yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) kwa misimu miwili ijayo na kutozwa faini ya Paundi Milioni 24.9

- Ni kutokana na kile kilichotajwa kuwa uvunjaji mkubwa wa kanuni za Financial Fair Play
MUATHIRIKA WA KWANZA WA VIRUSI VYA CORONA ATHIBITISHWA AFRIKA

> Misri imethibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza wa #CoronaVirus

> Ni Raia wa Kigeni. Mgonjwa huyo amelazwa na yupo katika uangalizi maalum

Zaidi, soma - https://jamii.app/CoronaVirusEgypt
MAMBO YA KUZINGATIA KWA WENYE MAGARI WANAPOTUMIA VIVUKO

> Unapoingia kwenye kivuko fuata sheria na maagizo kutoka kwa baharia. Shusha vioo na ufungue mkanda unapokuwa ndani ya kivuko

> Hakikisha watu wote wameshuka katika gari na umebaki dereva. Usizime gari unapokuwa ndani ya kivuko. Wakati wa kutoka subiri ruhusa ya baharia na tembea mwendo wa kawaida

Soma https://jamii.app/ZingatiaVivuko
HUENDA MAN. CITY IKAPUNGUZIWA ALAMA ZA LIGI NA KUSHUSHWA DARAJA

- Klabu lazima zitoe taarifa za kweli kupata leseni ya Ligi Kuu, na taarifa hizo huwa sawa na zile zitolewazo UEFA

- Jana, UEFA imeikuta klabu hiyo na uvunjivu wa Kanuni za Financial Fair Play katika taarifa zake

Zaidi, soma https://jamii.app/ManCityAdhabuLigi
HII NDIO HUSEMEKANA KUWA ASILI YA NENO ‘MSELA’

> Ilitokana na neno, ‘Sailor’ mfanyakazi wa meli wa kawaida. Waliokuwa wanazamia meli wanajiona ni Ma-sailor na wakaitana hivyo

> Kuzamia meli kunahitaji ujasiri, neno hilo likawa mtu aliyejitoa

Soma https://jamii.app/MselaBaharia
MAREKANI: MADHARA YA SHAMBULIZI LA IRAN KWA WANAJESHI WETU NI MAKUBWA

> Baraza la Congress limeonya kwamba matatizo ya ubongo waliyopata wanajeshi wa nchi hiyo katika shambulio la kulipiza kisasi lililofanywa na Iran kwenye kambi ya Ain al Assad ni makubwa na kuna hatari madhara hayo yakabakia kwa kipindi chote cha uhai wao

Soma - https://jamii.app/BrainDamageUS
CECIL MWAMBE ATANGAZA KUACHANA NA CHADEMA NA KUOMBA KUJIUNGA CCM

> Mbunge wa Ndanda (CHADEMA ), Cecil Mwambe leo Februari 15 amejiuzulu nafasi hiyo na kutangaza kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM)

> Amesema anatoka CHADEMA kwa hiyari yake na kama CCM itampokea basi apewe tena nafasi ya kugombea Ubunge

Soma - https://jamii.app/MwambeAtokaCDM
SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MAOMBI YA DAWA KUTOLEWA KWA NJIA YA KARATASI

> Naibu Waziri wa Afya amepiga marufuku kwa watumishi wa afya kutumia karatasi kama njia ya kuidhinisha maombi ya dawa baada ya kubaini mianya ya upotevu wa dawa za Serikali katika vituo vya afya

> Dawa zote ziwekwe kwenye fomu za maombi (requisition form) huku zikionyesha jina la aliyeomba, saini yake na saini ya mtu au idara ya famasi inayopokea maombi hayo

Soma - https://jamii.app/ZuioKaratasiDawa
WAHAMIAJI HARAMU WAKAMATWA DODOMA

> Raia wa Kenya wakamatwa kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria katika matukio mawili tofauti

> Sita walikamatwa Wilayani Chamwino wakitokea Arusha kwenda Mbeya, kwa basi la kampuni ya Capricon

Soma https://jamii.app/WahamiajiDodoma