JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kikao Kazi cha Taasisi Zinazounda Utatu, Agosti 18, 2025, Jaji Mkuu George Masaju ametaka Mahakama iondoe ucheleweshaji wa mashauri usio na sababu za msingi, akisema hali hiyo inadhoofisha utoaji wa haki, akisema “Kitu mnachoweza kumaliza kwa siku mbili, unasema mpaka umalize Miezi minne?”

Zaidi soma https://jamii.app/MasajuKesiMahakamani

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Governance #UtawalaBora
👍1
DAR: Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudai huduma ya Kampuni inayokamata Vyombo vya Moto vinavyoegeshwa kimakosa ndani ya Wilaya ya Ubungo na kueleza faini ya Tsh. 80,000 inayotozwa haiendani na kosa, ufafanuzi umetolewa na Mamlaka inayosimamia.

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imesema dereva anayekutwa na kosa hataruhusiwa kuondoka eneo la tukio hadi awe amelipa faini tofauti na utaratibu wa Polisi ambapo faini inaweza kulipwa baadaye hata baada ya kuondoka eneo la tukio.

Halmashauri hiyo pia imetoa maelekezo kwa Watendaji wa Boss Kazi Ltd kufanya kazi kwa kufuata masharti ya mkataba na Sheria za nchi, kuhudumia Wananchi kwa staha, heshima na weledi, kupiga picha kabla ya kutoa faini ili kuepusha sintofahamu na kutoa elimu ya kutosha kwa kila Mwananchi anayekamatwa kuhusu kosa lake na namna ya kulipa.

Zaidi https://jamii.app/WrongParkingUbungo

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFHuduma #ServiceDelivery #JFMdau2025 #Accountability
2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MBEYA: Kamanda wa Polisi Mkoa, Benjamin Kuzaga amesema wanawashikilia Watu Tisa kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia Mitandao ya Kijamii ikiwemo Facebook na WhatsApp, ambapo Watuhumiwa hao walikamatwa Agosti 18, 2025 katika maeneo ya Nsalala na Mapelele, Mbalizi.

Kamanda Kuzaga ameeleza kuwa Watuhumiwa hao walitumia mbinu mbalimbali ikiwemo kutangaza nafasi feki za ajira, kuwatapeli Watu kwa kutumia simu na mitandao kwa mtindo wa “Tuma kwenye namba hii,” na kuwarubuni wengine wachangie fedha kujiunga na Kampuni ya Q NET yenye asili ya Malaysia.

Amewataja waliokamatwa ni Nemia Njonga (23), Ombeni Ambilikile (22), Jacob Peter (23), Baraka Mgala (22), Lusajo Jeremiah (45), Adili Mbeyale (19), Shaban Yasin (23), Ester Kimaro (28) na Abdi Awadhi (21).

Zaidi soma https://jamii.app/WakamatwaUtapeli

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFDigitali #DigitalSafety #Accountability
1
Mdau wa JamiiForums.com kupitia Jukwaa la Siasa ameeleza katika kipindi hiki cha mchakato wa vyama kuwapata Wagombea, kumekuwa na usambazaji wa vifaa vyenye nembo ya chama. Anadai matukio hayo yanaweza kuibua mjadala kuhusu ushawishi, kwani bado haijathibitishwa kama vinaweza kuathiri maoni ya Wapiga Kura kwa makusudi.

Amehoji, Je, wahusika wanahakikisha hakuna uvunjifu wa Sheria za Uchaguzi wakati wa usambazaji wa vifaa hivyo?

Zaidi Soma https://jamii.app/KablaYaKampeni

#JamiiForums #Accountability #Misinformation #Disinformation #ElectionInformation2025 #MisDis2025 #TaarifaZaUchaguzi2025
2
GEITA: Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limesema linaendelea kuchunguza tukio la kutoweka kwa Elisha Juma, mkazi wa Mtaa wa Kadisi, Kata ya Katente, Wilaya ya Bukombe, ambaye pia ni mwimbaji wa nyimbo za injili.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 21, 2025, Polisi wameeleza walipokea malalamiko kwamba mnamo Agosti 19, 2025 saa 10:00 jioni, Elisha alichukuliwa na watu watatu wasiojulikana akiwa studio ya MAS J, Kilimahewa kata ya Bulangwa, waliokuwa na gari jeupe lisilojulikana usajili wake.

Aidha, Jeshi limetoa wito kwa yeyote mwenye taarifa ya kuweza kusaidia kupatikana kwa Elisha asisite kuziwasilisha ili zifanyiwe kazi.

Zaidi soma https://jamii.app/JumaElishaWasiojulikana

#JamiiAfrica #JamiiForums #Governance #Accountability #JFMatukio #UtawalaBora #HakiZaBinadamu
2
NJOMBE: Mdau wa JamiiForums.com ambaye ni Mkazi wa Njombe Mjini ametoa wito kwa Halmashauri hiyo kuweka wazi ikiwa imetoa maelekezo kwa Shule za Msingi kutoza Wanafunzi hadi Tsh. 10,000 kwa ajili ya mitihani ya kila wiki, na kuongeza kuwa gharama hizo zimekuwa mzigo kwa Wazazi na Walezi.

Zaidi soma https://jamii.app/ShuleNjombeHalmashauri

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFHuduma #Accountability #JFMdau2025 #JFUwajibikaji
1
SOMALIA: Marais watatu wastaafu Sharif Sheikh Ahmed, Abdiqasim Salad Hassan na Mohamed Abdullahi Farmaajo wameungana kutoa tamko dhidi ya Serikali ya Rais Hassan Sheikh Mohamud, wakiilaani kwa uporaji na uuzaji holela wa ardhi ya umma bila kuzingatia taratibu za Kisheria na usimamizi unaostahili.

Viongozi hao wamesema Serikali imekuwa ikihamisha umiliki wa ardhi bila kuhusisha Mamlaka ya Mikataba ya Taifa, na kutoingiza mapato kwenye Hazina ya Taifa. Hali inayosababisha Wananchi maskini wa Mogadishu kufukuzwa na kuondolewa katika makazi yao.

Wametaka Wananchi na Wafanyabiashara kuepuka kununua au kushiriki katika mali zilizopatikana kwa njia zisizo halali, wakisema ni mikataba hatarishi na isiyo na uhalali, hatua ambayo imepongezwa na makundi ya uharakati.

Soma zaidi https://jamii.app/Somalia

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Governance
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (#JAB), Wakili Patrick Kipangula ametoa angalizo kwa Waandishi wa Habari wasiokuwa na ithibati, kuwa hawataruhusiwa kuripoti Uchaguzi Mkuu 2025.

Amefafanua kuwa Mwandishi kufanya kazi bila kitambulisho cha Bodi ya Ithibati ni kosa linaloweza kusababisha faini ya hadi Tsh. Milioni 5 au kifungo cha miaka mitatu hadi mitano. Ameeleza hayo wakati wa Mkutano wa Wadau wa Habari na Utangazaji Kanda ya Mashariki, Agosti 21, 2025.

Zaidi soma https://jamii.app/JABWaandishiUchaguzi

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFUwajibikaji #Accountability #JFSiasa
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
JF KUMBUKIZI: Akizungumza siku ya Mei Mosi, 1995, katika hotuba yake Mwl. Julius Kambarage #Nyerere alisema kuwa mwenye akili akikupa mawazo ya kipumbavu, ukayakubali, anakudharau.

"Na wewe una akili, anajua unajua kwamba ni ya kipumbavu, ukayakubali, anakudharau."

Zaidi Soma https://jamii.app/MawazoKipumbavu

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Siasa #JFKumbukizi #AmkaNaJamiiAfrica #GoodMorning
5
ARUSHA: Jeshi la Polisi limetoa taarifa kuwa linafanya uchunguzi kuhusiana na tukio la Mtu mmoja aitwaye Bakari Halifa Daud (18) Mkazi wa Sombetini kujeruhiwa kwa kupigwa risasi mguuni na Abdulaziz Abubakari (Dogo Janja).

Kamanda wa Polisi Mkoa, SACP Justine Masejo amesema uchunguzi wa awali umebaini tukio hilo lilitokea Agosti 23, 2025 Saa 5:30 Usiku maeneo ya Sombetini na kwamba Jeshi linawashikilia Watu wawili kuhusiana na tukio hilo huku uchunguzi ukiendelea.

SACP Masejo ameongeza kuwa wakati Abdulaziz Abubakari (30), Mkazi wa Levolosi akiwa anashuka kwenye gari alidai kutaka kuvamiwa na Bakari akiwa na mwenzake kwa kutumia silaha ya jadi hali iliyosababisha kutumia silaha aliyokuwa nayo.

Zaidi https://jamii.app/DogoJanjaKumpigaRisasi

#JamiiAfrica #JamiiForums #HumanRights #Accountability #Uwajibikaji
Mdau wa JamiiForums.com kutoka Jukwaa la Siasa anasema katika kipindi hiki cha Uchaguzi na uteuzi wa Wagombea, Wananchi wameonekana kuwakataa wale Wagombea walioteuliwa na chama husika.

Shiriki Mjadala https://jamii.app/MtuBinafsi

#JamiiForums #Accountability #Misinformation #Disinformation #ElectionInformation2025 #MisDis2025 #TaarifaZaUchaguzi2025
KILIMANJARO: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa Serikali Kuu na Mamlaka za juu za Usalama kuingilia kati na kuchukua hatua juu ya matukio yanayoendelea kati ya Wakulima dhidi ya Wafugaji katika Kijiji cha Mbatakero, Wilaya ya Hai, akidai kuna uvamizi unaoathiri Watu, Mazao, mali na kutishia uhai wa Watu.

Mdau anadai mgogoro huo umesababisha kuwe na matumizi ya ndivyo sivyo ya silaha za jadi na kwamba walalamikaji wanapowasilisha hoja zao kwa Mamlaka mbalimbali hazifanyiwi kazi kwa usahihi.

Anadai baadhi ya Wananchi wameanza kuhamasishana kujilinda wao, mali zao na afya zao na kwamba wamefikisha malalamiko yao katika Vyombo vya Habari vya Mkoani hapo navyo vimekuwa na uzito wa kuwasikiliza hali ambayo inaweza kusababisha machafuko kama hakutakuwa na muongozo wa Serikali.

Zaidi soma https://jamii.app/KijijiChaMbatakero

#JamiiAfrica #JamiiForums #HumanRights #Accountability #JFMdau2025
2
Mdau wa JamiiForums.com anasema wakati wa Uchaguzi taarifa za Wagombea husambaa kwa kasi Mitandaoni, zingine zikiwa sahihi na zingine si sahihi, hali inayoweza kuwachanganya Wananchi kimaamuzi.

Anahoji, Je, taarifa za Wagombea unazoziona Mtandaoni huwa unaziamini au unazihakiki kwanza kabla ya kufanya maamuzi?

Shiriki Mjadala https://jamii.app/WagombeaMtandaoni

#JamiiForums #Accountability #Misinformation #Disinformation #ElectionInformation2025 #MisDis2025 #TaarifaZaUchaguzi2025
KAGERA: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Mamlaka kufuatilia uanzishwaji wa kambi ya maandalizi Shuleni kwa madarasa yenye mitihani (Kidato cha 2 & 4) akidai kuna michango ambayo inafanywa kuwa ya lazima ambapo wale wasiotoa wanawekwa pembeni hali inayofanya baadhi ya Wanafunzi kuikimbia shule kwa kukosa michango hiyo.

Zaidi https://jamii.app/WanafunziKambiKujisomea

#JamiiAfrica #JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #JFMdau2025
1
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anadai maeneo mengi ya #Kariakoo ikiwemo Mataa ya Uhuru kuna kundi la Watu linafanya uonevu wa kukamata Bodaboda na kuwalazimisha watoe Tsh. 10,000 hadi Tsh. 20,000 nje ya utaratibu wa Faini za Kiserikali pindi wanapowakamata wakiwatuhumu kuwa na makosa mbalimbali.

Anaeleza kama hakutakuwa na utaratibu wa kudhibiti tabia hiyo, itafika hatua Wanaoonewa watachoka na kunaweza kutokea madhara makubwa, kwani wanaokamatwa wengine hawana makosa lakini wanaingia katika mtego huo, hivyo ameshauri Serikali ichukue hatua kudhibiti usimamizi ili Haki itendeke.

Zaidi soma https://jamii.app/UsalamaBodaboda

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #JFHuduma #JFMdau2025
1