JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UTEUZI: Rais Samia amemteua Gilead John Teri kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (Tanzania Investment and Special Economic Zones Authority - TISEZA) leo Julai 1, 2025

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusilika, Teri ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo kufuatia kutungwa kwa Sheria ya Uwekezaji na Maeneo maalum ya mwaka 2025

Aidha, Sheria hiyo imeunganisha majukumu ya kilichokuwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na iliyokuwa Mamlaka ya Maneno maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA)

Zaidi Bofya https://jamii.app/UteuziGileadTeri

#JamiiAfrica #Utawala #JamiiForums #Uteuzi
DAR: Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, #TunduLissu, imeahirishwa hadi Julai 15, 2025 ikiwa bado inasubiri hatua atayoichukua DPP akimaliza kupitia faili, ambalo imeelezwa na Mawakili wa Jamhuri kuwa bado lipo mezani kwake

Akizungumza kabla ya maamuzi hayo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Lissu aliiomba Mahakama iwaamuru Mawakili wa Jamhuri kueleza hatua ya uchunguzi ilipofikia, kwa kuwa hadi kufikia Wiki inayofuata atakuwa amekaa gerezani kwa Siku 90

Soma https://jamii.app/LissuJulai1

#JamiiForums #JamiiAfrica #CivilRights
Mdau, wewe ni Mzazi/Mlezi anayeamini katika Mfumo upi wa Malezi?

1. Kumchapa Mtoto humfanya awe na Nidhamu
2. Kumchapa Mtoto huweza kumfanya awe mkaidi zaidi
3. Mtoto anapaswa kulelewa pasipo kuchapwa

Mjadala zaidi https://jamii.app/MaleziKumchapaMtoto

#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha #JFStories #JFChitChats #Malezi
Mdau wa Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ndani ya JamiiForums.com ameomba ushauri wa hatua za kuchukua kutokana na kuchukiwa na Watu bila sababu kiasi kwamba hali hiyo imeanza kuathiri Maisha yake ya kawaida

Unamshauri nini Mdau?

Mjadala zaidi https://jamii.app/NachukiwaBilaSababu

#JamiiAfrica #JamiiForums #Lifestyle #Maisha
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akizungumza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kutajwa kwa shauri la kesi ya uhaini, Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, #TunduLissu, amesema akifanikiwa kutoka atarejea Barabarani na kuendelea na mchakamchaka ambao hakuufafanua zaidi

Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi Julai 15, 2025.

Soma https://jamii.app/LissuMahakamaniJulai1

#JamiiForums #JamiiAfrica #CivilRights
2
KAGERA: Waziri wa Mambo ya Ndani, Innocent Bashungwa amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kutetea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Karagwe, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), leo Julai 1, 2025

Bashungwa ambaye amekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kwa Vipindi Viwili kuanzia Mwaka 2015, aliwasili katika Ofisi hiyo akiwa katika gari ndogo aina ya Toyota Carina na kuchukua fomu kisha kurejesha kwa Katibu wa CCM Karagwe, Anatory Nshange ambapo pia aliondoka akiwa katika usafiri huo

Soma https://jamii.app/BashungwaFomu

#Siasa #Democracy #Kuelekea2025 @UchaguziMkuu2025
1
DAR: Baadhi ya Wakazi wanaoishi karibu na eneo linalodaiwa kujengwa Kanisa la Arise and Shine (Kawe), linaloongozwa na Boniface Mwamposa wamedai ujenzi huo umekuwa kikwazo kwa baadhi ya huduma ikiwemo Barabara kufungwa na maji kukatika

Wakizungumza leo Julai 1, 2025 Asubuhi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule hali hiyo inatokana na uharibifu wa miundombinu unaodaiwa kufanywa na Wakandarasi wa mradi huo wa ujenzi.

Baada ya kusikia malalamiko hayo, DC Mtambule aliamuru kusitishwa kwa ujenzi huo kwa muda, ili kutoa nafasi ya kufanya tathmini ya kina

Soma https://jamii.app/UjenziKanisa

#JamiiForums #Accountability #JFMatukio #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anasema "Mimi ni Mkazi wa Mtaa wa Mabomu, Mvuleni - Msongola, tuliuziwa kiwanja na kujenga, Miaka kadhaa baadaye akaja Mtu aliyejitambulisha ni Baba wa “Muuza Kiwanja”, akatutaka kuondoka hapo akidai tupo katika eneo lake

Anaeleza "Tulienda Mahakamani, tukashinda na kukabidhiwa nyaraka. Huyo Mzee amerejea na kuanza kuvunja Nyumbani yetu akidai naye alienda Mahakamani akashinda, hajatuonesha nyaraka za hukumu wala hakukuwa na Mwakilishi wa Serikali za Mtaa

Anatumia nguvu ya Kiuchumi kutunyanyasa, tumeenda Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wa Ilala, Maafisa wa hapo nao wanatukandamiza, wanatutaka tumlipe “Mzee” Tsh. Milioni 3, kama hatuna atamalizia kubomoa nyumba yote

Tunaomba msaada Mamlaka za juu, hatuna uwezo wa kujibizana Kisheria kwani ameonesha dharau kwa Mahakama, kwa sasa hatuna pa kuishi

Soma https://jamii.app/NyumbaBomolewa

#JamiiForums #JFMatukio #CivilRights #Accountability
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimesema kimetoa msaada wa dhamana kwa Waumini 52 wa Kanisa la Ufufuo na Uzima waliokamatwa na Polisi Juni 29, 2025 katika eneo la Ubungo, jijini Dar es Salaam

Soma https://jamii.app/LHRCWaumini52Gwajima

#JamiiAfrica #JamiiForums #HumanRights #JFMatukio
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Changamoto ni sehemu ya safari ya Maisha. Kama vile Mashine ya kufulia Nguo inavyopindua na kuzungusha nguo kwa nguvu ili kuzisafisha, ndivyo Matatizo huwa pale yanapotufikia

Tunapojikuta katikati ya matatizo, mara nyingi huwa hatuoni faida yake, bali maumivu tu lakini mwisho wa yote, tunatoka tuking'aa zaidi.

#JamiiForums #GoodMorning #JamiiAfrica #Maisha #AmkaNaJF
🔥1