JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amependekeza kutoza ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha 30% kwenye vifaa vya Sigara za Kielektroniki na vimiminika vya Sigara za Kielektroniki, ili kupunguza athari zinazotokana na matumizi ya bidhaa hizo na kuongeza wigo wa Kodi

Amesema hatua hiyo inatarajia kuongeza Mapato ya Serikali kwa kiasi cha Tsh. Milioni 3,322.2

Soma https://jamii.app/BajetuKuu2025

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025 #Governance #Uwajibikaji #Transparency
1
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amependekeza kupunguza ada ya usajili wa pikipiki za biashara kutoka Tsh. 340,000 hadi Tsh. 170,000 kwa miaka mitatu, huku akisema ada hiyo husika italipwa wakati wa usajili wa awali pekee

Vile vile amependekeza kupunguza ada ya leseni ya uendeshaji wa pikipiki, bajaji na guta kutoka Tsh. 70,000 hadi Tsh. 30,000

Soma https://jamii.app/BajetuKuu2025

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025 #Governance #Uwajibikaji #Transparency
3
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema “Ni kweli Kituo cha Kupoza Umeme cha llamilo (Simiyu) kimechelewa Utekelezaji wake kutokana na sababu za Kiutendaji na kwamba Mkandarasi wa Ujenzi ameshapatikana, na Utekelezaji utaendelea ili kuimarisha hali ya upatikanaji wa Umeme.”

Ufafanuzi huo umetolewa baada ya Mdau kueleza licha ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, kuweka jiwe la msingi la Mradi Machi 2021 na kuahidi Unenzi kukamilika baada ya Mwaka mmoja lakini sasa inaelekea Miaka mitano hakuna kilichofanyika, changamoto ya kukatika umeme mara kwa mara ipo vilevile, akahoji, kama Wananchi walidanganywa?

Taarifa ya #TANESCO imeongeza kuwa “Serikali kupitia Wizara ya Nishati na TANESCO tutahakikisha tunakamilisha kwa awamu ujenzi wa Miradi yote ya Gridi Imara iliyopangwa kama ilivyokusudiwa katika maeneo yote nchini.”

Soma https://jamii.app/UmemeSimiyuMradi

#Governance #Accountability #Transparency #JamiiAfrica #Uwajibikaji  #ServiceDelivery #JamiiForums #JFMdau2025
2
KENYA: Inaelezwa Askari James Mukhwana ambaye kwa sasa anashikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya Mwanaharakati Albert Ojwang’, amesema (OCS), Samson Talaam alitoa amri ya “kumuadhibu” Ojwang, amri ambayo Mukhwana anadai ilitoka kwa Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Eliud Lagat

Maelezo hayo, ambayo Citizen TV imeyapata yanadai Mukhwana amesimulia jinsi alivyoitwa Ofisini kwa OCS usiku huo akiwa kazini, na kuelezwa “Kuna agizo kutoka kwa DIG Lagat. Unamfahamu? Kuna Maafisa kutoka Makao Makuu ya DCI wanamleta mtuhumiwa hapa saa mbili Usiku. Waambie wale wafungwa wamuonyeshe adabu kidogo.”

Ojwang alifungiwa ndani Saa tatu na dakika 20 Usiku, muda mfupi baada ya hapo mateso yakaanza kwenye selo ya mwisho karibu na Vyoo. Mukhwana anasema wafungwa wanne, Collins Ireri, Gil Ammiton, Brian Mwaniki na Erick Ndambuki waliagizwa kumshambulia.

Soma zaidi Ushahidi huu https://jamii.app/KonsteboMukhwanaTalks

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #HumanRights #HakiZaBinadamu #Transparency
2🤔1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SIMIYU: Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ametoa onyo kwa Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina pamoja na Wanasiasa wengine wa Mkoa wa Simiyu, kuacha kutumia zao la Pamba kama mtaji wa Kisiasa

Bashe amesema Mpina aliwahi kumdanganya Hayati Rais Magufuli kuhusu Bei ya Zao la Pamba Duniani na kusababisha Wakulima kupata hasara, kwa kuuza Pamba kwa Tsh. 500

Soma https://jamii.app/BasheMpinaKuuaKitalu

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #JamiiAfrica #Siasa #Transparency
2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
JFKUMBUKIZI: Machi 04, 2019 Hayati John Pombe Magufuli alizungumzia matukio ya Utekaji Nchini na kusema "Watanzania wanajua kuchambua mambo, na lilipotokea tukio la kutekwa kwa Mo Dewji zilikuja habari nyingi kwamba waliohusika na Utekaji ni Wazungu wa aina fulani lakini suala hilo lilipomalizika, liliacha maswali mengi zaidi."

Aliongeza kwa kusema wahusika walijaribu kulichoma Moto Gari lakini baadae aliyetekwa akaonekana anakunywa Chai na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam (wakati huo), Lazaro Mambosasa.

Soma https://jamii.app/MagufuliMatukioUtekaji

#JamiiForums #JFKumbukizi #JamiiAfrica #HumanRights #Transparency #Siasa
2
Ujumbe huu uliandikwa na Isaac Asimov, ambaye alikuwa raia wa Marekani, Mwandishi na Profesa aliyefundisha katika Chuo Kikuu cha Boston

Alizaliwa Mwaka 1920 na kufariki Mwaka 1992 akiwa na umri wa Miaka 72

#Governance #JamiiForums #Accountability #Transparency #JFNukuu #JFQuote #Quotes #JamiiAfrica
3🔥2👍1
Luhaga Joelson Mpina alianza safari yake ya #Siasa Mwaka 2003 akiwa Kamanda wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hadi kushika nafasi mbalimbali katika chama hicho na sasa amechaguliwa kugombea nafasi ya Urais kupitia chama cha #ACTWazalendo.

Uamuzi wa kuhamia ACT Wazalendo unakuja mwezi huu Agosti 2025 baada ya jina lake kuondolewa kwenye orodha ya Wagombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika mchakato wa ndani ya chama uliofanyika Julai 2025.

Kufahamu zaidi bofya https://jamii.app/LuhagaMpinaWasifu

#JamiiAfrica #JamiiForums #Transparency #UchaguziMkuu2025 #PresidentialCandidates
Salum Mwalimu alianza safari yake ya #Siasa kikamilifu Mwaka 2014 ambapo aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa #CHADEMA upande wa Zanzibar, alishika nafasi mbalimbali katika chama hicho na sasa amechaguliwa kugombea nafasi ya Urais kupitia Chama cha #CHAUMMA.

Uamuzi wa kuhamia CHAUMMA alitangaza rasmi Mei 19, 2025 baada ya maamuzi ya Salum na Wanachama wengine wa CHADEMA kujitoa katika chama hicho kutokana na kutoridhishwa na maamuzi ya Uongozi mpya ikiwemo kutoshiriki Uchaguzi Mkuu 2025 pamoja na madai ya chama kupoteza dira.

Zaidi https://jamii.app/SalumMwalimuWasifu

#JamiiAfrica #JamiiForums #Transparency #UchaguziMkuu2025 #PresidentialCandidates #Siasa