This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza Jeshi la Polisi kupinga vitendo vya #Rushwa kwa maelezo kuwa hayo yalikuwa maradhi makubwa kwa jeshi hilo na kwamba anapotumiwa video zikionesha matukio ya Rushwa za Barabarani naye anamtumia Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Camillus Wambura
Rais Samia ameeleza hayo katika sherehe ya Kufunga Kozi ya Maafisa na Wakaguzi wa Jeshi la Polisi Chuo cha Taaluma ya Polisi, leo Juni 9, 2025.
Soma https://jamii.app/RaisAkemeaRushwa
#JFMatukio #Governance #JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability

Kila mtu ana hadithi yake, sauti yake na mchango wake wa kipekee kwa dunia. Kuwa tofauti ni zawadi ni ishara ya ubunifu, uthubutu na utambulisho wa kweli.
Usiogope kuwa tofauti, ogopa zaidi kupotea kwenye kundi la watu wanaoishi kwa kujificha, bila kuishi maisha yao ya kweli. Kuwa wewe Dunia inakuhitaji jinsi ulivyo halisi na wa kipekee
#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha #GoodMorning #AmkaNaJF

DAR: Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudai Wakazi wa Mtaa wa Makamba, Mbezi Msakuzi hawana Huduma ya Maji kwa madai kuwa Mhandisi amesitisha uchimbaji mtaro "kwa sababu binafsi", Mamlaka inayohusika imetoa ufafanuzi
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar (DAWASA), Everlasting Lyaro amesema walifanya vikao Machi 2025 na Ofisi ya Serikali za Mtaa wa Msakuzi Kusini na kuwaeleza hakuna fedha taslimu inayotakiwa kutolewa na Mwananchi kwa DAWASA, hivyo maunganisho mapya (Water connections fee) yatalipiwa baada ya kukamisha hatua za upimaji (Survey)
Amesema “Mtumishi wa DAWASA haruhusiwi kupita na kuchangisha fedha kwa Wananchi ili atoe huduma kwa upendeleo, Mamlaka imeweka utaratibu wa kutambulisha Watumishi wanaotekeleza miradi na wanaohudumia Wananchi.”
Soma https://jamii.app/MbeziMsakuziMaji
#Accountability #ServiceDelivery #JamiiForums

Kupitia Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ndani ya JamiiForums.com, Mwanachama anasema baadhi ya Wafanyakazi wenzake ambao ni 'wakongwe' hapo Ofisini wamemchukia na hata hawamsalimii baada ya kugundua analipwa Mshahara mkubwa zaidi yao wakati yeye ni Mfanyakazi mpya
Je, nawe umeshawahi kupitia changamoto hii, ulifanyaje?
Tembelea mjadala huu zaidi https://jamii.app/MshaharaKuchukiwaKazini
#JamiiForums #Maisha #JFChitChats #JFStories #LifeLessons

#HAKIZABINADAMU: Huduma ya Taifa ya Polisi Kenya (NPS) imethibitisha Maafisa Watano kuondolewa kazini kwa muda, ili kuruhusu uchunguzi huru, wa kina na wa haraka unaoendeshwa na Mamlaka Huru ya Kusimamia Utendaji wa Polisi (IPOA), kuhusu Mazingira ya kifo cha Albert Ojwang
Ojwang alifariki Juni 8, 2025, Siku moja baada ya kukamatwa Nyumbani kwake Kakot, Homa Bay, akiwa chini ya uchunguzi kuhusu chapisho alilodaiwa kumdhalilisha Naibu Mkuu wa Polisi kwenye Mtandao wa Kijamii wa X, na kusafirishwa hadi Nairobi alipofia
Taarifa ya awali ya Polisi ilidai kuwa Ojwang alifariki kwa majeraha baada ya kujigonga ukutani akiwa rumande, lakini ripoti za awali na malalamiko ya Wanaharakati wa Haki za Binadamu zilionesha Mwili wake ulikuwa na majeraha ya wazi ya kupigwa, ikiwemo Kichwani, Usoni na Mikononi
Kufuatia malalamiko hayo, Polisi walitoa taarifa ya Pili ikieleza kuna ‘masuala tata’ kuhusu kifo cha Ojwang yanayohitaji uchunguzi zaidi
Soma https://jamii.app/IGPKenya
#JamiiForums

RUVUMA: Baadhi ya majengo ya Shule ya Sekondari ya Jenista Mhagama iliyopo Halmashauri ya Songea yameungua kwa Moto ikiwemo Mabweni ya Wanafunzi wa kike na Stoo ambapo awali Mdau wa JamiiForums.com alidai moto huo umetokana na hujuma
Mkuu wa Wilaya, Wilman Ndile, alipoulizwa kuhusu tukio hilo amesema “Moto umesababisha hasara kubwa, umeharibu majengo, Chakula cha Wanafunzi cha thamani ya Tsh. Milioni 1, vingine vilivyoungua ni Magodoro na Vifaa ya Umeme
DC amesema Mwanafunzi alichoma Moto Dhule mara tatu tofauti, Mei 31, Juni 1 na Juni 3, 2025, kwa sasa anashikiliwa anatarajiwa kupelekwa Mahakamani, tumezungumza na Wazazi wake nao pia wamekiri kuwa Mtoto wao ni mkorofi.
Soma https://jamii.app/ShuleYaMhagama
#JamiiForums #JFMatukio #JamiiAfrica
Mkuu wa Wilaya, Wilman Ndile, alipoulizwa kuhusu tukio hilo amesema “Moto umesababisha hasara kubwa, umeharibu majengo, Chakula cha Wanafunzi cha thamani ya Tsh. Milioni 1, vingine vilivyoungua ni Magodoro na Vifaa ya Umeme
DC amesema Mwanafunzi alichoma Moto Dhule mara tatu tofauti, Mei 31, Juni 1 na Juni 3, 2025, kwa sasa anashikiliwa anatarajiwa kupelekwa Mahakamani, tumezungumza na Wazazi wake nao pia wamekiri kuwa Mtoto wao ni mkorofi.
Soma https://jamii.app/ShuleYaMhagama
#JamiiForums #JFMatukio #JamiiAfrica
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
TABORA: Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia ukurasa wake wa X (Twitter) leo Juni 6, 2025 kimeandika kuwa Watu waliokuwa na mapanga na visu wamevamia mkutano wao maeneo ya Igunga na kufanya vurugu, ikielezwa walianza kwa kurushia mawe msafara wa Makamu Mwenyekiti wa #CHADEMA, John Heche
Taarifa hiyo imeongeza “Jeshi la Polisi halikuwepo eneo la mkutano licha ya kuwa na taarifa ya kuwepo kwa mkutano, Polisi walifika baada ya tukio hilo kutokea. Watu hao wamedhibitiwa na Wananchi.”
Jitihada za kupata taarifa rasmi ya Jeshi la Polisi kutoka Mkoani Tabora zinaendelea
Soma https://jamii.app/MkutanoCHADEMAIgunga
#JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imeagiza Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kusitisha shughuli zozote za kiutendaji na oparesheni hadi hapo Kesi ya Msingi iliyofunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wake Zanzibar, Said Issa Mohamed na wenzake wawili, dhidi ya Baraza la Wadhamini na Katibu Mkuu wa chama hicho, itakaposikilizwa Juni 24, 2025
Uamuzi huu umetolewa bila uwepo wa Wawakilishi wa Upande wa Utetezi (CHADEMA), baada ya Wakili wao, Jebra Kambole kujiondoa kwenye shauri hilo na kusababisha Mahakama kuendesha kesi kwa upande mmoja. Shughuli zilizositishwa kwa muda ni shughuli za Kisiasa za Ndani na Oparesheni kama vile Mikutano ya Hadhara na vikao vya CHADEMA.
Kuhusu madai kuwa CHADEMA imekuwa ikiitenga Zanzibar katika masuala mbalimbali, ikiwemo mgawanyo wa rasilimali fedha, Jaji Mwanga amesema ni suala la kisheria na limefafanuliwa vyema kwenye Sheria ya Vyama vya Siasa
Soma https://jamii.app/CHADEMAStop
#JamiiAfrica #JamiiForums

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imesema imebaini uwepo wa vitendo vya Ukiukwaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa Sura 258 katika Mikutano ya Siasa, kwa baadhi ya Vyama kuruhusu Wanachama na mashabiki wake kutumia maneno ya Uongo, kashfa na uchochezi dhidi ya Chama kingine, Mtu binafsi, Taasisi au Serikali
Msajili amekiasa kila Chama cha Siasa chenye Usajili kamili, kuwaelimisha na kuwadhibiti Wanachama na Mashabiki wake, kuhakikisha hawakiuki Sheria za Nchi, hususani Sheria ya Vyama vya Siasa na Kanuni zake na inafuatilia mienendo ya Viongozi, Wanachama na Mashabiki wa Vyama vya Siasa
Soma https://jamii.app/MsajiliMaelekezo
#JamiiForums #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025 #Siasa

DAR: Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema linaidai Klabu ya Yanga (kiasi cha Fedha hakijawekwa wazi) na si kweli kuwa Klabu hiyo inadai Fedha za ubingwa wa Kombe la Shirikisho la TFF ilizostahili kupata msimu uliopita
TFF imesema Yanga iliomba kwa barua Fedha zao za zawadi katika mashindano mbalimbali zikatwe kulipia malipo wanayotakiwa kulipa kwa TFF ikiwemo ada za wachezaji wa kigeni
TFF imesema imeandika barua kwenda #Yanga ikiitaka Klabu hiyo kumtuma Mtaalamu wao wa Fedha Juni 11, 2025 kuhakiki deni la Klabu hiyo akiwa na vielelezo vyote katika Ofisi za TFF
Wakati Yanga ikisema haitacheza fainali ya Michuano hiyo hadi ilipwe, TFF imeeleza Mdhamini Mkuu wa mashindano hayo, Benki ya CRDB ililipa Fedha zote za Kimkataba Tsh. 255,000,000
Soma https://jamii.app/TFFVsYanga
#JamiiForums #JamiiAfrica #JFSports #Michezo

Yanga imesema haijawahi kulipwa fedha yoyote ya Ubingwa wa Kombe la Shirikisho la TFF kwa Misimu mitatu mfululizo (2021/2022, 2022/2023 na 2023/24) na kwamba TFF imekuwa ikishikilia fedha hizo kwenye akaunti zao huku wakifahamu ni makosa na ni kinyume cha utaratibu
Yanga imeeleza “Hakuna uthibitisho wowote wa kimaandishi kuonyesha TFF wamewahi kulipa fedha hizo. Ni aibu, fedheha na kumtia dosari mdhamini kuendesha mashindano bila kumlipa Bingwa. Tunaelekeza, dawa ya deni ni kulipa kwa wakati ikiwa ni haki ya mshindi na inampa heshima mdhamini wa mashindano.”
Taarifa “leleweke, ada za malipo ya Wachezaji wa kigeni walizozisema kwenye taarifa yao hulipwa mwanzo wa msimu mpya na hela hizi za Ubingwa hutolewa Mwisho wa msimu. Yanga haijawahi kupokea taarifa yoyote rasmi kutoka TFF kuhusu Klabu yetu kuwa na deni kwao.”
Soma https://jamii.app/YangaMajibuJuni10
#JamiiForums #JFSports #JamiiAfrica

Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Kada wa Chama cha ACT Wazalendo, Selemani Said Bungara (Bwege) amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) kiko sahihi kudai Mabadiliko ya Mfumo wa Uchaguzi lakini ameonesha wasiwasi kama wataweza kushikilia msimamo wao huo kwa bila ruzuku kwa Miaka mitano ijayo
Akihojiwa na EATV, Bwege aliyewahi kuwa Mbunge wa Kilwa Kusini kwa Miaka 10 (2010- 2020) kupitia Chama cha Wananchi (CUF) kabla ya kuhamia #ACTWazalendo ameongoza kuwa #CHADEMA wakishikilia msimamo huo hadi Mwaka 2030 watakuwa Chama imara zaidi huku akidai ACT inasubiri huruma ya #CCM katika Uchaguzi
Soma https://jamii.app/BwegeKuhusuUchaguzi
#JamiiForums #Kuelekea2025 #Democracy #UchaguziMkuu2025