JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: Mahakama ya Tanzania imesema Shauri la Jinai Namba 8606/2025 na Namba 8607/2025 kati ya Jamhuri na Tundu Lissu, ambayo yamepangwa kutajwa na kusikilizwa Juni 2, 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mwenendo wote utarushwa mubashara (live) na pia Mshtakiwa atafikishwa Mahakamani

Taarifa ya Mahakama imeeleza, lengo ni kuwawezesha Wananchi kufuatilia bila kuwa na ulazima wa kufika Mahakamani, pia ni Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania kuimarisha uwazi, uwajibikaji na matumizi ya teknolojia katika huduma ya utoaji haki

Taarifa imeeleza Mahakama ya Wazi Kisutu ni ndogo, inachukua Watu 80, hivyo imekubalika watakaoingia ni Mawakili wa Serikali na Watu wengine (10), Mawakili Utetezi na Watu wengine (60) na Waandishi wa Habari (10)

Soma https://jamii.app/LissuJune2

#JFMatukio #JamiiForums #Governance #Democracy
3
Kusoma kwa undani habari hizi na mengine yaliyojiri juma lililopita bofya https://jamii.app/YaliyojiriJumaLililopita

#JamiiForums #YaliyojiriJumaLililopita #JFToons #AmkaNaJF
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, #TunduLissu alivyowasili ndani ya Mahakama ya Kisutu kwaajili ya kuanzia kusikiliza kesi zinazomkabili, leo Juni 2, 2025

Mahakama ya Tanzania ilitoa taarifa kuwa mwenendo wote wa kesi hiyo utarushwa mubashara (live) ili kuwawezesha Wananchi kufuatilia, bila kuwa na ulazima wa kufika Mahakamani kutokana na udogo wa Mahakama ya Kisutu

Zaidi https://jamii.app/KesiLissuJuni

#JamiiForums #Siasa #Democracy #Governance #HumanRights #Kuelekea2025
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#DEMOKRASIA: Viongozi mbalimbali na baadhi ya Wanachama wa CHADEMA wamejitokeza Mahakamani Kisutu kusikiliza kesi ya Lissu leo Juni 2, 2025

Soma https://jamii.app/KesiLissuJuni

#JamiiForums #Siasa #Democracy #Governance #HumanRights #Kuelekea2025
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamezuiliwa kuingia ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia kesi ya Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, Tundu Antiphas Lissu

Soma https://jamii.app/PolisiVirunguCHADEMA

#JamiiForums #Siasa #JamiiAfrica #Democracy #Governance #HumanRights #UchaguziMkuu2025
😢1
DAR: Imeelezwa Mawakili 30 kati ya 120 wanaomtetea Tundu Lissu wapo Mahakama уа Hakimu Mkazi Kisutu kwaajili ya kusikiza kesi zinazomkabili Mteja wao leo Juni 2, 2025, wakiwemo Dkt. Rugemeleza Nshala na Wakili Peter Kibatala

Zaidi https://jamii.app/KesiLissuJuni

#JamiiForums #Siasa #Democracy #Governance #HumanRights #Kuelekea2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SIMIYU: Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina, akizungumza na Wananchi wa Mwandu Itinje, Juni 1, 2025, alisema “Hatuwezi kuwa Viongozi wa kuongea mapambio tu wakati Fedha za Wananchi zinaliwa”

Video Credit: Habari Digital

Soma https://jamii.app/MpinaVigelegeleWezi

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #UchaguziMkuu2025
KAGERA: Mdau wa JamiiForums.com anadai baadhi ya Walimu wa Shule za Msingi zilizopo Wilayani Missenyi, wamekuwa na utaratibu Mwanafunzi akifeli somo au kufanya kosa, anapewa adhabu ya kuleta Vyuma chakavu

Anadai hali hiyo imechangia baadhi ya Wanafunzi kuchukua Vifaa vya ndani na kuvifanya Vyuma chakavu, ambapo pia wanakuwa katika Mazingira hatarishi, wanapotafuta Vyuma hivyo Mtaani

Anaeleza tabia hiyo imeanza kujitokeza katika Shule ya Msingi Mugana A, Katarabuga n.k, akitoa wito kwa Mkurugenzi wa Missenyi kufuatilia kwa ukaribu suala hilo na kuchukua hatua stahiki

Soma https://jamii.app/ShuleMissenyi

#JamiiForums #Accountability #Elimu #Governance #JamiiAfrica
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Shauri la uhaini linalomkabili Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, #TunduLissu limeendelea, leo Juni 2, 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo limeahirishwa hadi Juni 16, 2025 baada ya upande wa Jamhuri kueleza upelelezi haujakamilika

Hakimu Mkazi Mfawidhi Franko Kiswaga ameagiza Jamhuri kuharakisha na kutoa taarifa za mwenendo wa upelelezi wa kesi hiyo ili shauri lianze kusikilizwa mapema

Akizungumza baada ya kuahirishwa kwa shauri hilo, Wakili anayemtetea Lissu, Dkt. Rugemeleza Nshala amesema Hakimu ametoa onyo kwa Lissu kwa kitendo cha kuzungungumza “No Reforms No Election” wakati tayari Mahakama imeanza

Soma https://jamii.app/KesiLissuJuni

#JamiiForums #Siasa #Democracy #Governance #HumanRights #Kuelekea2025
Ripoti ya CAG ya Mwaka 2023/2024 ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo imeonesha Mapitio ya nyaraka na ziara za Ukaguzi wa miradi zilibaini Shule mpya 35 za msingi zenye thamani ya Tsh. 15,819,500,000 na shule mpya 148 za Sekondari zenye thamani ya Tsh. 109,327,133,843 zilijengwa katika maeneo ambayo hayakupimwa

Ufuatiliaji hafifu wa Maafisa masuuli katika kupata maeneo kwa ajili ya ujenzi wa Shule ulisababisha hali hii, hivyo kuziweka Shule hizo katika hatari ya Migogoro ya Ardhi, kama vile Migogoro ya Umiliki na Mipaka

Machi 2023, Katibu Mkuu wa OR-TAMISEMI aliagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha Shule hizo zinajengwa katika maeneo yaliyopimwa na hati miliki za Viwanja husika zinapatikana ndani ya Miezi Mitatu tangu tarehe ya agizo

Soma zaidi https://jamii.app/ViwanjaShuleVisivyopimwa

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #ServiceDelivery #HudumaZaKijamii #CAGReport25
1
DAR: Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART) umeingia mkataba wa Miaka 12 na Kampuni binafsi ya usafirishaji ya Emirates National Group (ENG) kutoka Abu Dhabi kuendesha Mradi wa BRT Jijini Dar

Mkataba huo ulisainiwa Mei 30, 2025 ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa DART, Dkt. Athumani Kihamia amesema Emirates National Group itachukua uendeshaji wa awamu ya kwanza ya mradi wa BRT na kuleta mabasi mapya 177

Imeelezwa Mchakato huo ulianza Mwaka 2017 kupitia mfumo wa ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), lakini ulipata changamoto za kimajadiliano kuhusu viwango vya nauli na mifumo ya usuluhishi

Ikumbukwe Mwaka 2020, Serikali ilitangaza zabuni upya ambapo kampuni 40 ziliwasilisha maombi, ambapo Emirates National Group iliibuka mshindi.

Soma https://jamii.app/EmiratesKusimamiaMwendokasi

#JamiiForums #JamiiAfrica #ServiceDelivery #Transparency
👎1
DODOMA: Barua inayodaiwa kutoka kwa Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Emmanuel Kihampa, imeeleza kufungwa kwa shughuli za Kanisa la Ufunuo na Uzima, linalongozwa na Askofu Josephat Gwajima, kwa madai ya kutoa mahubiri yenye mwelekeo wa Kisiasa na nia ya kuichonganisha Serikali na Wananchi, kwa kuwa vitendo hivyo vinaathari ya kuhatarisha amani na utulivu nchini

Pia, barua hiyo imeliamuru kanisa hilo kusitisha shughuli zake mara moja na imefutiwa usajili wake, ila lina haki ya kukata rufaa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ndani ya siku 21

Jitihada za kumpata Msajili wa Jumuiya za Kiraia kuzungumzia barua hiyo hazijafanikiwa

Soma https://jamii.app/GwajimaKanisaKufungwa

#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance #Utawala
3👍1👎1