JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
KATAVI: Familia ya marehemu Edga Mwaniwe, Wakazi wa Manispaa ya Mpanda imegoma kuuchukua mwili wa ndugu yao huyo kwa ajili ya maziko uliohifadhiwa Hospitali ya Manispaa Mpanda, leo Mei 4, 2025 ikiwa ni siku ya saba

Msemaji wa familia hiyo, Charles Mwaniwe amesema kifo cha ndugu yao kina utata na kwamba mshukiwa namba moja hajachukuliwa hatua na Jeshi la Polisi

Taarifa ya Polisi kuhusu tukio hilo imesema inawashikilia Watu Saba kwa kusababisha kifo cha Edga kwa kumshambulia wakimtuhumu kuuza madini feki kwa Tsh. 570,000 kwa Robert Benedict ambaye ndiye familia inamtuhumu

Kuhusu Robert, Polisi imesema alifika eneo la tukio na kukuta Edga akishambuliwa, akamchukua na kumpeleka Kituo cha Polisi baadaye hospitali ambapo alipoteza maisha

Soma https://jamii.app/KataviTukio

#JFMatukio #JamiiForums #Accountability #HumanRights
πŸ‘3
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Makamu wa Rais Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Eusebius Nzigilwa amesema tukio la kushambuliwa kwa Katibu wa Baraza hilo, Padre Charles Kitima lilitaka kupora haki ya uhai, uhuru wa haki yake ya kusema na kutenda kadiri ya wito wake aliojaaliwa na Mwenyezi Mungu, huku akiongeza kuwa ni shambulio dhidi ya heshima ya taifa kwani linajulikana kuwa kisiwa cha amani.

Askofu Nzigilwa amesema hayo leo Mei 04, 2025 katika Misa Takatifu iliyoadhimishwa na Askofu Mkuu Jude Thaddaeus Ruwa`ichi OFMCap, katika ibada ya kusimikwa kwa askofu Stephano Musomba wa Jimbo Katoliki la Bagamoyo

Soma https://jamii.app/Mei4TEC

#JamiiAfrica #JamiiForums #HumanRights #Accountability #SocialJustice
πŸ‘1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Jeshi la Polisi limesema linafuatilia kwa karibu tuhuma zilizotolewa na Mwananchi (ambaye jina lake linaendelea kufuatiliwa) kupitia Mitandao ya Kijamii, akiwatuhumu askari Wawili kuwa walimfuata kumtaka afanye nao kazi ya kijajusi huku wakitaka kufahamu alipo Mdude

Taarifa ya Jeshi la Polisi imesema kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, limeunda kikosi kazi ambacho tayari kimefika Mbeya kwaajili ya uchunguzi zaidi wa suala hilo, huku likitoa wito kwa yeyote mwenye taarifa zitakazosaidia kubaini ukweli wa suala hilo atoe ushirikiano

Soma https://jamii.app/UchunguziMei4

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #SocialJustice
πŸ‘1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
MBEYA: Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wamefika Ofisini kwa Mkuu wa Upelelezi Mkoani humo kwa lengo la kumpa ushahidi wa watu wanaodai ni askari ambao wanadaiwa kuhusika na tukio la kumjeruhi kisha kumteka Mpalukwa Nyagali, maarufu kama Mdude

Aidha, Wanachama hao wamedai kuwa wataendelea kuandamana kwenda Ofisini kwa RPC kila siku, mpaka watakapopata Majibu ya mwisho ya Mdude yupo wapi

Soma https://jamii.app/UshahidiMdude

#JamiiForums #HumanRights #SocialJustice #JamiiAfrica #Accountability
πŸ‘1
Kusoma kwa undani habari hizi na nyingine zilizojiri juma lililopita bofya https://jamii.app/YaliyojiriJumaLililopita

#JamiiForums #YaliyojiriJumaLililopita #JFToons
❀1
Haki za wachache ni za muhimu kama yalivyo Matamanio ya wengi; Viongozi wa Kidemokrasia huhakikisha pande zote zinazingatiwa kwa usawa.

#JamiiForums #JamiiAfrica #Democracy #GoodMorning #AmkaNaJF #Quotes
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anadai Barabara ya Kitunda - Banana imeendelea kuwa kero kubwa kwa Watumiaji kutokana na uwepo wa mashimo kiasi kwamba kuna Gari nyingi zikiwemo Daladala zimebadilishiwa β€˜ruti’ na kusababisha Watu wengi kukosa usafiri

Soma https://jamii.app/KitundaBananaRoad

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #JFMdau2025
Mdau wa JamiiForums.com anasema kumbukumbu za Binamu yake alivyokuwa akimnyanyasa Kingono Utotoni zinamtesa na anaumia akikumbuka ambavyo Mama yake hakulipa uzito suala hilo, kila alipomwambia kinachoendelea

Anasema changamoto anazozipitia sasa ni kukosa Imani na Ujasiri wa kukaa na Ndugu zake wa kiume sehemu moja, anashindwa kulala gizani kwa Miaka 29 sasa, anapenda Watoto ila hataki Kuzaa na kuna muda anatamani kufa sababu anaona Kifo kitakuwa zawadi kwake

Soma zaidi https://jamii.app/NduguKuharibuWatoto

#JamiiForums #Maisha #ChildAbuse #SexualViolence
#MICHEZO: Yanga imesema baada ya maelezo ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) kuitaka Klabu hiyo kurejea katika Mamlaka za Tanzania kuhusu suala lao la kutocheza dhidi ya Simba, msimamo wao ni kuwa hawana imani na hawako tayari kupeleka shauri hilo kwenye Mamlaka ambazo zinatenda dhuluma

Yanga imeeleza sababu za kufanya hivyo ni kutokana na uonevu, uvunjwaji mkubwa wa kanuni na upendeleo wa dhahiri kwa baadhi ya Timu unaoendelea kufanywa na Mamlaka za soka Tanzania

Taarifa ya Klabu hiyo imeeleza kuwa Wanayanga wote, watakuwa tayari kuipambania Haki yao kivyovyote vile ili kukomesha dhuluma na uvunjwaji mkubwa wa kikanuni unaoendelea kufanywa na Mamlaka za Soka kwa maslahi mapana ya Maendeleo ya Soka Nchini

Soma https://jamii.app/YangaTamko

#JFSports #JamiiForums
πŸ‘2
Mshiriki wa Shindano la Stories of Change 2024, anasema ifikapo Mwaka 2035 Usugu wa Vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa (UVIMADA), itakuwa janga kubwa zaidi kwani Tanzania imo kwenye orodha ya Nchi 14 za Kusini mwa Jangwa la Sahara zenye kiwango kikubwa cha UVIMADA

Anapendekeza uanzishwe Mfumo maalumu wa kukusanya taarifa (Kanzi Data) za Kimaabara za Wagonjwa wenye UVIMADA, utakaoratibiwa kwenye ngazi ya kanda ili kufuatilia ukubwa wa Janga, kupanga mipango Kisera na kibajeti, kuratibu tafiti pamoja na kutoa miongozo

Soma zaidi Andiko hili https://jamii.app/UVIMADASOC2024

#JamiiForums #JamiiAfrica #PublicHealth #Afya
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MANYARA: Suzana Samweli (13), Mwanafunzi wa Darasa la 6, Mkazi wa Kata ya Galapo, Wilaya ya Babati ameuawa kikatili na mwili wake kukutwa umetupwa shambani

Familia ya marehemu imesema Suzana hakurudi nyumbani Jioni ya Aprili 29, 2025, baada ya kutoka shuleni na mwili wake ukapatikana shambani Mei 1, 2025, ikielezwa alibakwa na kutobolewa macho

Akizungumza na Kituo cha Clouds FM, Kamanda wa Polisi Mkoa, SACP Ahamed Makarani amesema wanamshikilia Elias Daniel (26), Mkazi wa Kijiji cha Gedamar kwa mahojiano zaidi, pia yapo matukio mengine ya aina hiyo ambayo hayakuripotiwa Polisi

Soma https://jamii.app/MwanafunziAuawa

#JamiiForums #JFMatukio #HumanRights
πŸ‘1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro, amesema wanamshikilia Mtu mmoja aliyedaiwa kuchapisha taarifa kwenye Ukurasa wa X (Twitter) akiandika β€œSiku za Padre Kitima zinahesabika”

Muliro amesema "Amekamatwa na anahojiwa, anaitwa Frey Edward Cossey (51), Mkazi wa Dodoma na Mbezi Beach Makonde kufuatia chapisho lake la vitisho dhidi ya Padri Charles Kitima alilolitoa kwenye Mitandao ya Kijamii siku chache kabla ya tukio."

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima, alishambuliwa na kujeruhiwa Aprili 30, 2025 ikiwa ni siku mbili baada ya andiko hilo la Mtandaoni

Soma https://jamii.app/MuliroMei5

#JFMatukio #Accountability
πŸ‘2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Dorothy Jonas Semu, Kiongozi wa Chama cha #ACTWazalendo akizungungumza katika sherehe za kutimiza Miaka 11 ya Chama hicho amesema hawapo tayari kususia Uchaguzi Mkuu wa 2025 na kuwa watapambana wakati wakishiriki na watashiriki wakiwa wanapambana

Amesema β€œHuu ni Mwaka wa kuinusuru Zanzibar, Mwaka wa maamuzi. Ni Mwaka wa kukata kiu ya muda mrefu ya Wazanzibari ya kupata Zanzibar mpya, #Zanzibar moja na yenye Mamlaka kamili.”

Ameongeza kuwa ACT inapendekeza; Wakurugenzi wa Halmashauri wasisimamie Uchaguzi, Wajumbe wapya wa INEC wateuliwe, Kura haramu zidhibitiwe, Wagombea wasienguliwe ovyo, Mawakala wawe huru na Vyombo vya Dola visishiriki hujuma kwenye Uchaguzi.

Soma https://jamii.app/ACTMei5

#UchaguziMkuu2025 #Uchaguzi2025 #Democracy #Siasa
πŸ‘2
Bunge la Ulaya linatarajia kufanya mjadala Mei 7, 2025 kuhusu kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu ikiwemo ya Uhaini ambayo kama atakutwa na hatia moja ya adhabu yake ni kifo

Taarifa ya tovuti ya Bunge hilo imeeleza kuwa Mjadala huo utagusia masuala ya Haki za Binadamu, Demokrasia na Uhuru, ambapo mjadala utafanyika kuanzia Saa 8:00 Mchana hadi Saa 5:00 Usiku

Baada ya mjadala huo, Wabunge wa Bunge hilo watakuwa na ratiba ya kupiga Kura, kesho yake Mei 8, 2025

Soma https://jamii.app/BungeLaUlaya

#JamiiForums #Democracy
πŸ”₯1
Mdau wa JamiiForums.com ameanzisha Mjadala akishauri watu kupunguza matukio ya kimahaba mbele ya Wazazi siku ya harusi, kama kulishana keki mdomo kwa mdomo

Unadhani ni mambo gani hayapaswi kufanyika ukumbini siku ya harusi?

Mjadala https://jamii.app/ScenesZaHarusi

#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha #LifeStyle