JamiiForums
โœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Katibu Mkuu wake, John Mnyika kimetoa wito kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Camillus Wambura kuwajibika kutokana na tukio la Wanachama na Viongozi wa Chama hicho kudaiwa kukamatwa, kupigwa na kuumizwa na Polisi

Mnyika amesema "Tunamtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), kama haya matendo hayana baraka zake ajitokeze yeye mwenyewe atoe taarifa kwa Umma, juu ya matukio ya kupigwa, kuteswa na kuumizwa kwa Wanachama na Viongozi wa CHADEMA, akitaja idadi halisi, akitaja sababu ya hali hizo na kuwajibika kutokana na hayo"

Zaidi https://jamii.app/MnyikaPressApr30

#JamiiForums #Uwajibikaji #HumanRights #Governance #Democracy
โค1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, John Mnyika amewaonesha Waandishi wa Habari, video ya mtu aliyemtaja kwa jina la Noel akiwa amelala chini baada ya kudaiwa kupigwa rungu la kichwa, kung'atwa na mbwa na kuvunjwa Mguu na Polisi katika eneo la Mahakama ya Kisutu, Aprili 24

Zaidi https://jamii.app/UshahidiCHADEMA

#JamiiAfrica #JamiiForums #Governance #Accountability #Uwajibikaji
Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) imekumbusha Taasisi zote za Umma na binafsi Nchini zinazohusika na kuchakata taarifa binafsi za Watu, kuhakikisha zinajisajili kwenye Mfumo wa Usajili wa #RCMIS kabla ya tarehe ya mwisho, 30 Aprili 2025

Kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Mwaka 2022 (Sura ya 44), Taasisi yoyote inayokusanya au kuchakata taarifa binafsi, ikiwemo Mashirika ya Umma, Kampuni, Sekta ya 'hospitality', NGOs, Vyombo vya Habari, Shule, Vyuo, pamoja na watoa Huduma za Afya, inatakiwa kuwa imesajiliwa rasmi na PDPC ili kuzingatia matakwa ya Sheria

Imeelezwa, kushindwa kujisajili ni ukiukwaji wa Sheria ambapo mhusika anaweza kutozwa faini ya kati ya Tsh. 100,000 hadi Tsh. 5,000,000 au kifungo cha hadi Miaka Mitano, au vyote kwa pamoja

Soma https://jamii.app/SikuYaMwishoYaUsajili

#JamiiForums #DigitalRights #Governance #HakiYaFaragha #UlinziWaTaarifaBinafsi
๐Ÿ‘1
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Tawi lake la Bonyokwa kimemvua rasmi uanachama John Mrema aliyekuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa chama hicho kwa tuhuma za utovu wa nidhamu, dharau kwa mamlaka halali za chama na kukaidi misingi na maadili ya Chama

Kwa mujibu wa barua rasmi ya Aprili 30, 2025 iliyosainiwa na Katibu wa Tawi, Solomini Kagaruki ni kuwa Kamati Tendaji ya Tawi hilo ilikutana Aprili 29, 2025 na kufikia uamuzi huo kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006, toleo la 2019, ibara ya 5.4.3.

Miongoni mwa Tuhuma dhidi ya Mrema ni pamoja na kusambaza barua ya Wito ya Kamati ya Nidhamu kwenye mitandao ya kijamii badala ya kuitikia rasmi. Hata hivyo, Mrema amepewa haki ya kukata rufaa kwa ngazi ya juu endapo hataridhika na uamuzi huo

Zaidi https://jamii.app/JonMremaCDM

#JamiiForums #JamiiAfrica #Democracy #Accountability
#MAISHA: Unampa Ushauri gani Mdau huyu wa JamiiForums.com ili aweze kuyashinda Mawazo ya kuona anaelekea kufeli Maisha

Mjadala zaidi https://jamii.app/KutoboaMshaharaSerikali

#JamiiForums #LifeLessons #JFStories #JFChitChats #JamiiAfrica
๐Ÿ‘1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Baada ya kusambaa kwa taarifa za kushambuliwa kwa Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Charles Kitima na Watu wasiojulikana, usiku wa jana Aprili 30, 2025, Jeshi la Polisi limesema linamshikilia Rauli Mahabi โ€œHarajaโ€, Mkazi wa Kurasini kutokana na tukio hilo na uchunguzi unaendelea

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema tukio limetokea Saa Nne Usiku maeneo ya TEC - Kurasini, Temeke na kwamba alishambuliwa kichwani na kitu butu akiwa maliwatoni pembeni ya kantini

Muliro amesema Padre Kitima anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Aga Khan

Soma https://jamii.app/KitimaUpdates

#JFMatukio #JamiiForums #Governance #HumanRights
KENYA: Mbunge wa Chama cha ODM, Charles Were amepoteza maisha baada ya kupigwa risasi akiwa kwenye gari katika mzunguko wa Hifadhi ya City kwenye Barabara ya Ngong Jijini Nairobi kutoka kwa Watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki ambao bado hawajatambulika

Mbunge huyo wa Kasipul ambaye chama chake kinaongozwa na Raila Odinga amepigwa risasi Saa 1:30 Usiku, jana Aprili 30, 2025 ambapo mashuhuda wamesema mtu aliyempiga risasi alisogea karibu kabisa katika dirisha la gari na kufyatua risasi kisha kutokomea kusikojulikana

Alikimbizwa Hospitali lakini baadaye ikatangazwa amefariki, Jeshi la Polisi la Kenya bado halijatoa tamko kuhusu tukio hilo

Soma https://jamii.app/RIPCharlesWere

#JamiiForums #KenyanPolitics #HumanRights
๐Ÿ‘1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akizungumzia uamuzi wa baadhi ya kesi kufanyika kwa njia ya Mtandao, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ametolea mfano Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) walitoa tamko linaloashiria uvunjifu wa Amani na Usalama, hali iliyosababisha baadhi ya Wafungwa na Mahabusu kusikiliza mashauri yao kwa njia ya Mtandao

Amesema "Watanzania waelewe kuwa Jeshi linapokuwa na taarifa za Kiusalama linashirikiana na Mahakama kutoa Haki ile ile lakini kwa kutumia Teknologia ya Mahakama Mtandao ili kuzuia fujo Mtaani, naomba Watanzania watuelewe.โ€

Soma https://jamii.app/BashungwaAprili29

#JamiiForums #Accountability #Governance #HumanRights #CivilRights
โค1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, ameliagiza Jeshi la Magereza kusimamia Sheria na taratibu kwa wanaotaka kuwaona Wafungwa na Mahabusu, akieleza taratibu hizo lazima ziheshimiwe bila upendeleo na hakuna wanaotakiwa kupewa Huduma Maalum (V.I.P)

Soma https://jamii.app/BashungwaAprili29

#JamiiForums #Accountability #Governance #HumanRights #CivilRights
JamiiAfrica inawatakia Wafanyakazi wote Maadhimisho mema ya Siku ya Wafanyakazi Duniani

Tukumbuke, nyuma ya kila Huduma bora, Bidhaa nzuri na Maendeleo ya Taifa kuna jasho, Maarifa na Bidii ya Mfanyakazi

Tuendelee kusimamia Haki, Mazingira salama ya Kazi na Maslahi bora kwa Wafanyakazi wote. Bila Mfanyakazi, hakuna Mafanikio

#JamiiAfrica #JamiiForums #MeiMosi2025 #WorkersDay
โค2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amesema Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania litaendelea kuwawezesha Wafungwa na Mahabusu kusikiliza mashauri yao wakiwa Magerezani kupitia Mahakama Mtandao, hasa kunapokuwepo na viashiria vya matishio ya kiusalama

Ameyasema hayo Aprili 30, 2025 alipoambatana na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), kukagua Makasha ya kisasa ya Mahakama Mtandao yanayowezesha usikilizaji wa mashauri kwa njia ya Kiteknolojia katika Gereza la Isanga -Dodoma

Soma https://jamii.app/BashungwaAprili29

#JamiiForums #Accountability #Governance #HumanRights #CivilRights
๐Ÿ‘1
DAR: Akizungumzia tukio la Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima kujeruhiwa, Rais wa TEC, Askofu Wolfgang Pisa amesema eneo alikoshambuliwa hulitumia kufanyia kazi zake baada ya shughuli za pamoja na hakuwa anapata kinywaji, wala si sehemu kunakopatikana kinywaji chochote

Askofu Pisa amesema Padri Kitima alikuwa na Mapadri wenzake katika kikao, walipomaliza wenziwe waliondoka, akabaki eneo la mgahawa anakofanyia shughuli zake siku zote na kuwa hakuna baa wala vinywaji na kama kuna anayehitaji kupata vinywaji kwa kawaida angeenda nje ya eneo hilo

Ameongeza โ€œMaana ukisema Mtu alikuwa anakunywa kwa saa zote hizo maana yake alikuwa anakunywa pombe, si hivyo. Wakati anatoka kurejea ndani kuna uchochoro wenye giza, hapo ndipo akavamiwa na kujeruhiwa na kitu kizito kichwani na kidevuniโ€

Soma https://jamii.app/TECPadriKitima

#JFMatukio #JamiiForums
๐Ÿ‘3๐Ÿ”ฅ1
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kushambuliwa kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, tukio lililotokea usiku wa Aprili 30, 2025, katika eneo la Kurasini, Dar es Salaam

Padre Kitima alivamiwa na watu Wawili wasiojulikana na kushambuliwa kichwani na mwilini na kusababishiwa majeraha mbalimbali

CCM imesema inalaani vikali kitendo hicho cha kikatili na kisicho na utu dhidi ya kiongozi wa dini, ambaye kimesema amejitolea maisha yake kuhudumia jamii kwa upendo na uadilifu

CCM imetoa wito kwa vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa kina na wa haraka ili kuwabaini na kuwachukulia hatua kali wahusika wa tukio hilo

Soma https://jamii.app/CCMKitima

#JamiiForums #Governance #Accountability #HumanRights
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limelaani vikali tukio la kushambuliwa kwa Padre Charles Kitima, Katibu Mkuu wa baraza hilo lililotokea usiku wa Aprili 30, 2025 katika Makao Makuu ya TEC, Kurasini, Dar es Salaam

Kwa mujibu wa taarufa ya Baraza hilo, Padre Kitima kwa sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Aga Khan

Aidha, TEC imetoa wito kwa Jeshi la Polisi na Vyombo vya Usalama kuhakikisha wahusika wanakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria. Vilevile uchunguzi wa tukio hili ufanyike kwa haraka, kwa uwazi na bila upotoshaji ili kurejesha imani ya wananchi

Soma https://jamii.app/TamkoTECMei1

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #SocialJustice
Hatua ndogo ni hatua bado. Usijione mdogo kwa sababu hujafika kule unapotamani kufika

Acha kujilaumu kwa kile ambacho hujafanya jana, leo ni nafasi nyingine ya kujaribu tena, kujifunza tena na kusonga mbele

#Goodmorning #JamiiAfrica #JamiiForums #AmkaNaJF