JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Eti Mdau, Mtu akikukumbuka na Tsh. 100,000 ya ghafla ghafla Siku yako itakuwa safi eeh?

Mjadala https://jamii.app/WeekendVibes

#JamiiAfrica #LifeStyle #Maisha #JamiiForums
SONGWE: Mdau wa JamiiForums.com anasema Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi imefanikiwa kujenga Stendi mpya ya Mabasi eneo la Forest Mlowo, lakini imeanza kutumika huku Miundombinu mingi ikiwa hairidhishi

Anahoji, kulikuwa na ulazima gani wa kuharakisha Magari kuanza kupita kabla ya maboresho kukamilika? Akisisitiza Miundombinu Bora ni muhimu kwa Watumiaji wa Stendi hiyo

https://jamii.app/StendiMlowoMbovu

#JamiiForums #JamiiAfrica #ServiceDelivery #JFMdau2025 #HudumaZaKijamii
1
DURBAN: Kama ilivyofanya Mwaka 1993, Simba imefanikiwa kuandika historia ya kufika Fainali ya Michuano inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (#CAF), ni baada ya kuingia Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (Confederation Cup) kwa kuitoa Stellenbosch FC ya Afrika Kusini

Hiyo ni baada ya Nusu Fainali ya Pili kumalizika kwa 0-0 kwenye Uwanja wa Moses Mabhida, hivyo #Simba kusonga mbele kwa faida ya Goli 1-0 ililopata katika mchezo wa kwanza

Simba itacheza fainali na mshindi wa mchezo kati ya CS Constantine (Algeria) dhidi ya RS Berkane (Morocco), ambapo Fainali ya kwanza itachezwa Mei 17, 2025 na marudio ni Mei 25, 2025

Michuano hiyo ilianzishwa Mwaka 2004 baada ya CAF kuunganisha Mashindano ya African Cup Winners' Cup yaliyoanzishwa Mwaka 1975 pamoja na CAF Cup yaliyoanzishwa Mwaka 1992

Soma https://jamii.app/SimbaFainal

#JFSports #CAFCC #JamiiForums
👍2
Mdau waJamiiForums.com anasema kama Ada ya Mtoto wako ya Mwaka mzima ni kubwa kuliko kipato chako cha mwezi, basi hapo Unajifilisi na kiwango chako cha Maisha kitakuwa duni sana

Anasema ukifuata kanuni hii basi utajikuta Kipato chako cha Miezi 10 iliyobaki kinagharamia mahitaji mengine muhimu na utaishi bila madeni wala Msongo wa Mawazo

Umezielewa hesabu za Mdau au unaona haziwezekani?

Mjadala zaidi https://jamii.app/KipatoAdaKodi

#JamiiForums #Maisha #JFChitChats #JFStories #LifeLessons #JamiiAfrica
Picha zikionesha matukio tofauti ya Washiriki mbalimbali wa mbio (Fun Run) za Kilometa Tano zilizofanyika leo Aprili 27, 2025 ikiwa ni Siku ya kwanza ya Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ambayo yanafanyika kwa siku tatu Jijini Arusha

Mbio hizo zilizoshirikisha Wadau mbalimbali wanaoshiriki maadhimisho hayo zilianzia Uwanja wa Gymkhana/Mgambo na kuhitimishwa katika eneo hilo hilo

Soma https://jamii.app/WPFD2025Day1

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
👍1
Kusoma kwa undani habari hizi na nyingine zilizojiri juma lililopita bofya https://jamii.app/YaliyojiriJumaLililopita

#JamiiForums #YaliyojiriJumaLililopita #JFToons
👍1
ARUSHA: Leo Aprili 28, 2025 ni siku ya kwanza ya Maadhimisho ya Siku ya Vyombo vya Habari Duniani (#WorldPressFreedomDay2025). Maadhimisho haya yanafanyika kwenye Hoteli ya Gran Melia na yanatarajiwa kufanyika kwa siku tatu

Kwenye Maadhimisho haya Wadau watajadili mada mabalimbali ikiwemo mchango wa Akili Mnemba (AI) kwenye Tasnia ya Habari na Mikakati inayoweza kutumiwa na Watengeneza Maudhui kwenye wakati huu ambapo Teknolojia imekua

Maadhimisho ya WPFD 2025 yanaratibiwa na Taasisi ya JamiiAfrica, Serikali, Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) pamoja na Wadau wengine wa Habari ndani na nje ya Tanzania

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayOne

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia