Ukaguzi wa taratibu za ununuzi wa vifaa vya ujenzi vilivyotumiwa katika OR-TAMISEMI chini ya Mpango wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kwaajili ya ujenzi wa shule Mkoani Mara, ulibaini ununuzi wa vifaa vyenye thamani ya Tsh. 3,100,824,370 ulifanyika kinyume na masharti ya ununuzi wa Mwongozo wa Mamlaka ya Uthibiti wa Ununuzi wa Umma wa Utekelezaji wa Kazi za Ujenzi
Vifaa hivyo vilinunuliwa kutoka kwa Wazabuni ambao hawakuwa wameidhinishwa, au katika maduka yasiyokuwa na idhini ndani ya jamii husika au bila kuwa na makubaliano yoyote ya kimkataba kutoka kwa Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA)
Hayo yamebainika katika Ripoti ya CAG 2023/24 na kuelezwa kuwa hilo linadhoofisha Kanuni za uwazi, uwajibikaji na matumizi sahihi ya fedha za umma
Soma https://jamii.app/CAGMiradiMaendeleo
#RipotiYaCAG25 #RipotiCAG2025 #Uwajibikaji #CAGMiradiMaendeleo #Accountability #JamiiForums #Transparency

๐2
MWANZA: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa Mamlaka kushughulikia changamoto za miundombinu ndani ya Stendi ya Mabasi ya Nyegezi, akidai kuna Maji taka yanayotoka Chooni na kutiririka sehemu Watu wanapopita hali ambayo inaweza kusababisha Magonjwa ikiwemo Kipindupindu
Mdau anasema โNdani ya Stendi kuna Vyakula vinauzwa, kuna Maduka ya bidhaa mbalimbali ikiwemo vinywaji, kwa hali hiyo Kipindupindu kinaepukwaje?
Soma https://jamii.app/NyegeziMajiTaka
#JamiiForums #PublicHealth #Accountability #JFMdau2025

๐1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Abiria wamelazimika kuzuia basi la Mwendokasi kupita katika Kituo cha Kimara Mwisho baada ya kusubiri usafiri huo kwa saa kadhaa bila mafanikio, asubuhi ya leo Aprili 22, 2025
Ikumbukwe mara kadhaa Wadau wa JamiiForums.com wamekuwa wakilalamikia changamoto ya usafiri wa Mwendokasi ikiwemo kukaa muda mrefu kituoni
Soma https://jamii.app/MwendokasiMgomo
#JamiiForums #JFHuduma #ServiceDelivery
Video: Kagaba_GR
Ikumbukwe mara kadhaa Wadau wa JamiiForums.com wamekuwa wakilalamikia changamoto ya usafiri wa Mwendokasi ikiwemo kukaa muda mrefu kituoni
Soma https://jamii.app/MwendokasiMgomo
#JamiiForums #JFHuduma #ServiceDelivery
Video: Kagaba_GR
๐2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
JFKUMBUKIZI: Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akizungumzia maendeleo ya Demokrasia, ikiwemo suala la #Uwazi na matumizi ya #Teknolojia katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya, wakati alipokuwa Kiongozi ya Timu ya Uangalizi ya Uchaguzi huo, Agosti 2022
Soma https://jamii.app/JKKenya2022
#JamiiForums #JFKumbukizi #Democracy #KenyaPolitics #Transparency
Soma https://jamii.app/JKKenya2022
#JamiiForums #JFKumbukizi #Democracy #KenyaPolitics #Transparency
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Ally Mkii amefungua shtaka la Madai Mahakama Kuu, akiitaka Hospitali ya Aga Khan imlipe fidia ya Tsh. Bilioni 1.2, akidai uzembe wa kimatibabu umesababisha Mtoto wake akatwe mguu alipofika hapo kutibiwa
Wakili wa Ally, Pasensa Kurubone, amesema Washtakiwa ni Hospitali hiyo na Daktari aliyehusika, ambapo Mahakama imetupilia mbali pingamizi la Hospitali lililotaka shauri lisikilizwe na Mabaraza ya Waganga
Upande wa Ally Mkii amesema โTulimpeleka Aga Khan Tawi la Mbagala, Mwaka 2022, baada ya vipimo tukapelekwa Aga Khan ya Mjini, wakasema ana mvunjiko mdogo, akafungwa POP. Ikatakiwa turudi baada ya Wiki 3, hali ikawa mbaya tukarudi baada ya Wiki, ikabainika POP imebana na kushindwa kupitisha Damuโ
JamiiForums imewasiliana na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Aga Khan, Olayce Lotha aliyesema โSuala lipo chini ya Mkurugenzi wa Tiba na Afya pamoja na Wanasheria wetu, nalielekeza kwao kwa taarifa na ufafanuzi zaidi.โ
Soma https://jamii.app/MadaiYaFidia
#JamiiForums #Accountability

Kitu gani Mpenzi/Mwenza wako amewahi kukufundisha?
Mjadala https://jamii.app/MafunzoMpenzi
#JamiiForums #Maisha #LifeLessons #JFChitChats #JFStories
Mjadala https://jamii.app/MafunzoMpenzi
#JamiiForums #Maisha #LifeLessons #JFChitChats #JFStories
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeripoti kuwa Jeshi la Polisi limemkamata Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, John Heche, leo Aprili 22, 2025 eneo la Kariakoo na kwamba baada ya kumshikilia alipelekwa Kituo cha Polisi Msimbazi, kisha kumtoa kituoni hapo na kumpeleka kusikojulikana
Katibu Mkuu wa #CHADEMA, John Mnyika ameiambia JamiiForums kuwa โNi kweli Heche anashikiliwa na Polisi, tunaelekea Kituoni kujua kinachondelea, tutatoa taarifa zaidi baadaye.โ
Soma https://jamii.app/HecheKukamatwa
#JamiiForums #Democracy #JFMatukio

๐1๐1
Mdau wa JamiiForums.com anasema Iwe Mvua au Jua, Giza au Nuru ila anachokijua ipo Siku ataendesha Gari aina ya 'Hilux'
Na wewe una kitu gani ambacho unapambana lazima uje kukimiliki kwenye Maisha yako?
Shiriki mjadala huu zaidi https://jamii.app/NiniUtamiliki
#JamiiForums #Maisha #LifeLessons #JFChitChats #JFStories
Na wewe una kitu gani ambacho unapambana lazima uje kukimiliki kwenye Maisha yako?
Shiriki mjadala huu zaidi https://jamii.app/NiniUtamiliki
#JamiiForums #Maisha #LifeLessons #JFChitChats #JFStories
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Waziri wa OR-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa ameeleza tuhuma zilizotolewa na Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo, hazina ukweli wala uthibitisho na kwamba hakuna upotevu wa fedha katika ujenzi wa jengo la Utawala la Halmashauri ya Arusha Jiji
Mchengerwa amesema uchunguzi wa tuhuma hizo zilizotolewa na Gambo Bungeni umekamilika kama alivyoelekezwa kufanya na Spika Tulia Ackson, ambapo amedai kuna cheche za Siasa ambazo hazifai ndani ya taasisi zenye misingi ya Kisheria
Soma https://jamii.app/BungeniAprili22
#JamiiForums #Governance #Kulekea2025 #Siasa

KATAVI: Mdau wa JamiiForums.com anaeleza Daraja la Milala Shongo lililopo Kijiji cha Milala, Manispaa ya Mpanda limekuwa tatizo la muda mrefu kwa Wananchi wanaopita hapo, hivyo kuwa kikwazo cha mawasiliano na kusababisha shughuli za kiuchumi kusimama
Anaeleza asilimia kubwa wanaopata changamoto ni Wanawake na Watoto ambao wanashindwa kuvuka, hasa wakati wanapoenda katika matibabu kwa kuwa wakati wa mvua maji hujaa na kukata mawasiliano
Anadai siku za nyuma kulikuwa na mchakato wa kujenga Daraja hilo lakini ghafla mpango ukasimama na hawajui nini kilitokea, anatoa wito kwa mamlaka husika kujenga Daraja hilo kwa kuwa hali ni mbaya wakati huu wa mvua
Soma https://jamii.app/MilalaShongo
#JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery

This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Aprili 14, 2025 Mdau wa JamiiForums.com aliandika kuwa kuna changamoto ya chemba kutiririsha Majitaka katika Mitaa ya Nyamwezi na Mhonda, mlango wa kuingilia Soko Kuu (Shimoni) na kueleza kwamba, hali hiyo imekuwa hivyo tangu Machi 2025
Aprili 22, 2025, Mdau mwingine amepita katika eneo husika na kueleza kuwa Miundombinu imerekebishwa na majitaka hayatiririki Mitaani kama ilivyokuwa awali
Soma https://jamii.app/UsafiKariakoo
#Accountability #Uwajibikaji #PublicHealth #JamiiForums
Aprili 22, 2025, Mdau mwingine amepita katika eneo husika na kueleza kuwa Miundombinu imerekebishwa na majitaka hayatiririki Mitaani kama ilivyokuwa awali
Soma https://jamii.app/UsafiKariakoo
#Accountability #Uwajibikaji #PublicHealth #JamiiForums
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewaonya Watu ambao wameanza kuwasili kwaajili ya kuhudhuria kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, Mahakamani Aprili 24, 2025, akisema moto wa kisheria utashuka kwa nguvu zote kwa watakaodhamiria kuharibu Amani iliyopo
Soma https://jamii.app/ChalamilaKesiLissu
#JamiiForums #Governance #UchaguziMkuu2025 #Kuelekea2025
Soma https://jamii.app/ChalamilaKesiLissu
#JamiiForums #Governance #UchaguziMkuu2025 #Kuelekea2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anasema Wananchi wanaoishi Mbagala - Sabasaba, wanapata changamoto ya Mazingira kuchafuliwa na kuwa hatari kwa #Afya kutokana na Machinjio ya Ngโombe ambayo yapo kwenye Makazi ya Watu
Anaeleza Maji machafu ambayo yanatoka kwenye Machinjio hayo tanatiririka kwenye Makazi ya Watu na hakuna jitihada zinazofanywa na Mamlaka kudhibiti hali hii, akidai hali imekuwa mbaya zaidi msimu huu wa Mvua
Soma https://jamii.app/MajiMachinjioMBG
#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #PublicHealth