JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Taarifa huru huwezesha #Uwajibikaji wa Viongozi, kupambana na ufisadi, kuhamasisha ushiriki wa raia, na kuchochea ubunifu. Bila taarifa huru, maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi hulemazwa.

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
πŸ‘1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SHINYANGA: Mkuu wa Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Viktoria, Baba Askofu Dkt. Yohana Nzelu akizungumza na Waumini wa Kanisa hilo katika Ibada iliyofanyika Usharika wa Agape Kahama

Soma https://jamii.app/AskofuNzelu

#JamiiForums #Accountability #Governance
πŸ‘1
VATICAN: Papa Francis, Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani amefariki Dunia akiwa na umri wa Miaka 88

Vatican imetangaza kifo cha Papa Francis, leo Aprili 21, 2025 kupitia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii

Alikuwa Papa wa kwanza kuzaliwa au kukulia nje ya Ulaya katika kipindi cha karne 12, wa kwanza kutoka Amerika, na wa kwanza kutoka shirika la Kijesuiti kushika wadhifa huo.

Soma https://jamii.app/PopeFrancisDies

#JamiiForums #JFMatukio #RIPPopeFrancis
πŸ‘3
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Mkuu wa Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Viktoria, Askofu Dkt. Yohana Nzelu, akizungumza na Waumini katika Ibada iliyofanyika Usharika wa Agape Kahama, amegusia umuhimu wa Serikali kuwaondolea Wananchi hofu ya kuzungumza, kwa kuwa hali hiyo ikiendelea itasababisha visasi

Soma https://jamii.app/AskofuNzelu

#JamiiForums #Accountability #Governance
πŸ‘2
Maudhui potofu yanaweza kupotosha Umma, Kudhalilisha Watu, au hata kuchochea machafuko ya kijamii. Ni muhimu Jamii ifahamu na iwe na uwezo wa kutambua Maudhui ya aina hii.

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
MWANZA: Mdau wa JamiiForums.com anasema licha ya uwepo wa Magugumaji maeneo mengi ya Kando ya Ziwa Victoria, mbona haoni jitihada za Mamlaka husika kuyaondoa wakati yamekuwa kero kwa Watu na Vyombo vya usafiri?

Soma https://jamii.app/Magugumaji

#JamiiForums #Accountability #JFMdau2025 #Uwajibikaji
MANYARA: Timu ya #Yanga imefanikiwa kufikisha alama 70 katika Michezo 26 iliyocheza ya Ligi Kuu Bara baada ya kuichapa Fountain Gate Magoli 4-0 kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwara, leo Aprili 21, 2025

Wafungaji wa Mchezo huo ni; Clement Mzize (mawili), Ki Aziz na Clatous Chama. Matokeo hayo yanaifanya Yanga kuendelea kubaki nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Simba yenye alama 57, Michezo 22 huku Fountain Gate ikisalia nafasi ya 11 ikiwa na pointi 29

Soma https://jamii.app/GateYanga

#Sports #JamiiForums #JFLigiKuu25
SINGIDA: Wakati akilalamikia ubora wa Barabara ya Singida – Babati – Arusha, Mdau mwingine wa JamiiForums anasema eneo la Endasak Wilaya ya Hanang Barabara ina Mashimo mengi pia

Anaongeza kuwa hali hiyo inaanzia Kata ya Masakta hadi Endasak na changamoto hiyo ni ya muda mrefu licha ya kuwa ni Barabara Kuu

Soma https://jamii.app/BarabaraSingidaBabati

#JamiiForums #ServiceDelivery #Accountability #Governance
πŸ‘2
Ukaguzi wa taratibu za ununuzi wa vifaa vya ujenzi vilivyotumiwa katika OR-TAMISEMI chini ya Mpango wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kwaajili ya ujenzi wa shule Mkoani Mara, ulibaini ununuzi wa vifaa vyenye thamani ya Tsh. 3,100,824,370 ulifanyika kinyume na masharti ya ununuzi wa Mwongozo wa Mamlaka ya Uthibiti wa Ununuzi wa Umma wa Utekelezaji wa Kazi za Ujenzi

Vifaa hivyo vilinunuliwa kutoka kwa Wazabuni ambao hawakuwa wameidhinishwa, au katika maduka yasiyokuwa na idhini ndani ya jamii husika au bila kuwa na makubaliano yoyote ya kimkataba kutoka kwa Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA)

Hayo yamebainika katika Ripoti ya CAG 2023/24 na kuelezwa kuwa hilo linadhoofisha Kanuni za uwazi, uwajibikaji na matumizi sahihi ya fedha za umma

Soma https://jamii.app/CAGMiradiMaendeleo

#RipotiYaCAG25 #RipotiCAG2025 #Uwajibikaji #CAGMiradiMaendeleo #Accountability #JamiiForums #Transparency
πŸ‘2
MWANZA: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa Mamlaka kushughulikia changamoto za miundombinu ndani ya Stendi ya Mabasi ya Nyegezi, akidai kuna Maji taka yanayotoka Chooni na kutiririka sehemu Watu wanapopita hali ambayo inaweza kusababisha Magonjwa ikiwemo Kipindupindu

Mdau anasema β€œNdani ya Stendi kuna Vyakula vinauzwa, kuna Maduka ya bidhaa mbalimbali ikiwemo vinywaji, kwa hali hiyo Kipindupindu kinaepukwaje?

Soma https://jamii.app/NyegeziMajiTaka

#JamiiForums #PublicHealth #Accountability #JFMdau2025
πŸ‘1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Abiria wamelazimika kuzuia basi la Mwendokasi kupita katika Kituo cha Kimara Mwisho baada ya kusubiri usafiri huo kwa saa kadhaa bila mafanikio, asubuhi ya leo Aprili 22, 2025

Ikumbukwe mara kadhaa Wadau wa JamiiForums.com wamekuwa wakilalamikia changamoto ya usafiri wa Mwendokasi ikiwemo kukaa muda mrefu kituoni

Soma https://jamii.app/MwendokasiMgomo

#JamiiForums #JFHuduma #ServiceDelivery


Video: Kagaba_GR
πŸ‘2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
JFKUMBUKIZI: Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akizungumzia maendeleo ya Demokrasia, ikiwemo suala la #Uwazi na matumizi ya #Teknolojia katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya, wakati alipokuwa Kiongozi ya Timu ya Uangalizi ya Uchaguzi huo, Agosti 2022

Soma https://jamii.app/JKKenya2022

#JamiiForums #JFKumbukizi #Democracy #KenyaPolitics #Transparency