JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Shule za Msingi 35 na Shule za Sekondari 148 zilijengwa kwenye Ardhi isiyopimwa kwa Tsh. Bilioni 125.14, hali inayoweza kusababisha migogoro ya Ardhi na changamoto za uendelevu wa Miradi

Ripoti ya CAG ya Miradi ya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 inasema pia Mikataba yenye thamani ya Tsh. Bilioni 13.45 ilisainiwa bila kupitia uhakiki wa kisheria, hali inayoongeza hatari za Kisheria na Kifedha. Pia, kulikuwa na riba ya Tsh. Bilioni 1.29 iliyotokana na ucheleweshaji wa malipo kwa Wakandarasi

Aidha, malipo ya awali ya Tsh. Bilioni 13.79 yalifanyika bila dhamana, jambo linaloongeza hatari za Kifedha kwa Serikali ikiwemo upotevu wa Fedha hizo iwapo Mkandarasi atashindwa kutekeleza wajibu wake

Soma https://jamii.app/CAGMiradiMaendeleo

#RipotiYaCAG25 #RipotiCAG2025 #CAGMiradiMaendeleo #Accountability #JamiiForums #Transparency
Vipi Mdau, una maoni gani kuhusu Mtazamo huu?

Mjadala zaidi https://jamii.app/MkateWaMwingineUchunge

#JamiiForums #Lifestyle #JFChitChats
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetoa onyo kwa Wananchi kutofika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Aprili 24, 2025 wakati Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, atakapofikishwa kwaajili ya kusikiliza kesi ya #Uhaini inayomkabili

Kamanda Muliro amesema Jeshi limefuatilia mipango ya Viongozi wa Chama hicho na kubaini siku hiyo kutafanyika vurugu, hivyo kusisitiza yeyote atakayejitokeza Mahakamani Siku hiyo atachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria

Onyo hilo ni kufuatia wito uliotolewa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, Aprili 16, 2025 aliyehamasisha Wanachama na Wananchi kufika kwa wingi Mahakamani kumtia moyo Kiongozi wao

Soma https://jamii.app/KesiYaLissu

#JamiiForums #Accountability #Governance
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya Miradi ya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 inaeleza jumla ya Tsh. Trilioni 8.44 zilikuwepo kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ikijumuisha bakaa ya Miaka iliyopita na Fedha zilizopokelewa ndani ya Mwaka

Kati ya Fedha hizo, Tsh. Trilioni 5.93 zilitumika huku Tsh. Trilioni 2.50 hazikutumika hadi kufikia Juni 30, 2024 na kwamba tathmini ya Utendaji wa Kifedha ilibaini changamoto kadhaa, ikiwa ni pamoja na Fedha za Mradi kiasi cha Tsh. Milioni 635.44 zilizokopwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kutorejeshwa

Pia, malipo ya Tsh. Milioni 892.92 yalifanywa bila ya kazi iliyokamilika kuthibitishwa na Mhandisi Mshauri.

Soma https://jamii.app/CAGMiradiMaendeleo

#RipotiYaCAG25 #RipotiCAG2025 #CAGMiradiMaendeleo #Accountability #JamiiForums #Transparency
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Familia ya Raphael Majembe ikizungumza na Wanahabari Aprili 11, 2025 ilidai ndugu yao, Nestory Raphael Majembe (29) amefariki akiwa chini ya ulinzi katika Kituo cha Tabata Shule na kudai kabla ya mauti kumkuta alishambuliwa kwa kipigo akituhumiwa kuiba Simu

Familia hiyo imedai Nestory alikamatwa Usiku wa Aprili 6, 2025, akawekwa mahabusu ambapo baadaye Polisi waliwajulisha amefariki kwa kujiua jambo ambalo wanapinga na kuomba Mamlaka za juu ziagize uchunguzi

JamiiForums imezungumza na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Jumanne Muliro, kuhusu tuhuma hizo na amesema “Ndugu wa karibu wa Marehemu walikuja, tukachunguza na wakaelewa vizuri. Mashahidi ambao ni Ndugu zao walikuwepo, walieleza jambo lilivyokuwa mpaka huyo Mtu akapoteza Maisha.”

Soma https://jamii.app/PolisiTabata

#JFMatukio #JamiiForums #HumanRights #CivilRights #Accountability
👍1
Mdau wa JamiiForums.com, Wakili Bashir Yakub, anakumbushia kesi ya Uhaini iliyopata umaarufu ambayo wahusika walituhumiwa kupanga, kuratibu mipango ya kuiondoa Madarakani isivyo halali Serikali ya Mwalimu Julius Nyerere Miaka ya 1970

Watuhumiwa walipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha Maisha jela isipokuwa Oscar Kambona ambaye hakuwepo ndani ya Nchi.

Soma https://jamii.app/KosaLaUhaini

#JFSheria #JamiiForums #CivilRights #JFKumbukizi
Mdau ni kitu gani umewahi kusikia kuhusu popo lakini ukaja kugundua sio kweli?

Mjadala zaidi https://jamii.app/MamboKuhusuPopo

#JamiiForums #InternationalBatDay
DAR: CHADEMA imeomba siku 21 kujibu hoja zilizowasilishwa na Saidi Issa Mohammed na wenzake watatu waliofungua kesi Mahakama Kuu wakiiomba Mahakama kutoa amri ya kusimamisha shughuli zote za Kisiasa za Chama hicho hadi shauri lao la msingi litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi

Jambo TV imeripoti kuwa m Mawakili wamesema "CHADEMA wameambiwa wawasilishe majibu yao kabla au Mei 9, 2025, na kesi itakuja kutajwa Mei 12, 2025.”

Wapeleka maombi Saidi (aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa #CHADEMA Zanzibar) na wenzake Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu (Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini kutoka Zanzibar), wànadai wanatengwa, mgao wa mali hauzingatiwi na hata mishahara ni shida

Soma https://jamii.app/CHADEMAKesiUpdates

#JamiiForums #Kuelekea2025 #Democracy #Siasa
Vyombo huru vya Habari ni Sauti ya Jamii — tukivilinda, tunalinda Sauti zetu wenyewe.

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DEMOKRASIA: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesema kuna wengine wamesema wao hawashiriki uchaguzi na sio kazi yake kuwataka washiriki uchaguzi, kwa sababu ni haki ya kikatiba. Lakini msingi na jambo la maana ni je, mawazo yao yanatekelezeka kwa kipindi hiki?

Ameyasema hayo Aprili 17, 2025 Jijini Dodoma

Soma https://jamii.app/ReformsVsElections

#JamiiForums #Demokrasia #Accountability #Governance
👎1
MAISHA: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Jamii kuzingatia kuwa Watoto hawachagui Wazazi wao, lakini Wazazi wana nafasi ya kuchagua aina ya Upendo na Maadili wanayowaachia Watoto wao

Mdau, Unadhani kuna sababu gani ya Mwanaume kutelekeza Mtoto anayejua ni wake?

Mjadala https://jamii.app/Kutelekeza_Mtoto

#JamiiForums #Maisha #Malezi
1
Ripoti ya CAG ya Miradi ya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 imeeleza ukaguzi wa kiufundi wa Mradi wa Umeme wa Maji wa Julius Nyerere (JNHPP) haukuwa na Mpango wa dharura wa kuzuia na kukabiliana na maafa kwa jamii zilizo kando ya bwawa, hali ambayo inafanya wakazi wa maeneo hayo kuwa katika mazingira hatarishi

Vilevile, katika usimamizi wa Mikataba #TANESCO iliajiri kampuni ya kisheria bila kupata idhini ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, jambo ambalo lilisababisha uwakilishi dhaifu wa kisheria katika kesi ya Bodi ya Usuluhishi wa Migogoro ya Mikataba

Aidha, jumla ya Tsh. Milioni 752.87 zililipwa kwa kampuni hiyo bila kukata kodi ya zuio ya Tsh. Milioni 143.94, pia fidia ya ucheleweshaji ya Tsh. Bilioni 327.93 haikukatwa kutoka kwa Mkandarasi, jambo lililopunguza uwajibikaji wa kimkataba

Soma https://jamii.app/CAGMiradiMaendeleo

#RipotiYaCAG25 #RipotiCAG2025 #Uwajibikaji #CAGMiradiMaendeleo #Accountability #JamiiForums #Transparency
👍21