JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Rais Samia Suluhu Hassan amewapongeza Wakenya kwa kufanya Uchaguzi wa Amani uliompa Ushindi Naibu Rais, William Ruto

Amesema #Tanzania itaendeleza undugu na Ushirikiano wa Kihistoria na Kenya uliodumu Miaka na Miaka

Soma > https://jamii.app/SamiaAmpongezaRuto

#KenyaDecides2022
πŸ‘10😁1πŸŽ‰1πŸ’©1
#MYANMAR: Mahakama imemhukumu tena Kiongozi wa Nchi hiyo aliyeondolewa Madarakani, Aung San Suu Kyi kifungo cha Miaka sita jela kwa Ufisadi

Mpinzani huyo ameshtakiwa kwa makosa yasiyopungua 18 yakiwemo ya Ufisadi na Ukiukwaji wa mchakato wa Uchaguzi. Anaweza kuhukumiwa Miaka 190 jela

Soma - https://jamii.app/SuuKyiCase

#HumanRights
πŸ‘2
#KENYA: Ubalozi wa Marekani umetoa wito kwa pande zote kufanya kazi pamoja na kutatua changamoto ambazo zilijitokeza kipindi cha Uchaguzi Mkuu

Pia, Vyama vya Siasa viendelee kuwasihi wafuasi wao kuwa watulivu na kujiepusha na vurugu

Soma - https://jamii.app/USEmbassyKenya

#KenyaDecides2022
πŸ‘5
Vijana hivi sasa wanakua katika ulimwengu wa kidigitali ambapo Ujuzi na Uzoefu katika Masuala ya Digitali ni muhimu hususan katika Ajira

Hata hivyo, Mafunzo katika Nchi mbalimbali za Uchumi wa Chini na Kati bado ni changamoto kwani idadi kubwa ya Shule bado hazina vifaa vya kufundishia Wanafunzi

Zaidi, soma - https://jamii.app/DSYouth

#DigitalRights #DigitalSkills
😁6πŸ‘1
China imewawekea vikwazo Maafisa wa #Taiwan ikiwemo marufuku ya kuingia China na maeneo ya #HongKong na Macau kwa madai ya kuunga mkono uhuru wa Kisiwa hicho

Miongoni mwao ni Bi-khim Hsiao, Mwakilishi wa Taiwan Nchini Marekani

Soma https://jamii.app/VikwazoTaiwan

#ChinaTaiwanCrisis
πŸ‘5πŸ‘Ž4
CHINA NA TAIWAN: China imeendelea na mazoezi ya kijeshi karibu zaidi na Taiwan wakati baadhi ya Wabunge wa Marekani wakitembelea Kisiwa hicho

> Kikosi cha China kimesema kimeweka doria na kipo tayari kwa mapigano

Soma https://jamii.app/ChinaTaiwan2022

#JamiiForums
πŸ‘4
UKATILI KWA WATOTO: Takwimu zinaonesha Watoto Bilioni 1 Duniani hupitia aina fulani ya Unyanyasaji wa Kihisia, Kimwili au Kingono kila mwaka

Aidha, zaidi ya Mwanafunzi 1 kati ya 3 (miaka 13 - 15) hupitia aina fulani ya uonevu

Aina zote za ukatili zinaweza kusababisha madhara kwa Watoto, kudhalilisha Utu wao na kuzuia Maendeleo yao

Fahamu zaidi > https://jamii.app/WatotoData

#JFData #HakiMtoto
πŸ‘5
FIFA YAIFUNGIA INDIA KUJIHUSISHA NA SOKA

FIFA imeifungia #India kutokana na Mahakama kuingilia masuala ya Shirikisho la Soka

Michuano ya Kombe la Dunia la Wanawake U-17 inayoandaliwa na India, Oktoba 2022 ipo shakani kufanyika Nchini humo

Soma https://jamii.app/FIFABanIndia

#JFSports
πŸ‘2
#AUSTRALIA: Waziri Mkuu wa zamani, Scott Morrison anadaiwa kushikilia majukumu ya Wizara za Afya, Fedha, Hazina, Mambo ya Ndani na Rasilimali kwa Miaka 2 kinyume na sheria

Amejitetea alifanya kwa nia njema kutokana na janga la #COVID19

Soma https://jamii.app/WaziriAustralia

#Democracy
πŸ‘6
#UHURUWAHABARI: RUTO AHIMIZA UTAWALA WAKE KUKOSOLEWA

Rais Mteule wa #Kenya, William Ruto ameruhusu Utawala wake kukosolewa, akiwahimiza Wanahabari kufanya hivyo watakapokosea

Amesisitizia Mizania ili kuwa na Vyombo vya Habari vilivyo na Usawa

Soma - https://jamii.app/FreePressRuto

#PressFreedom
πŸ‘12
ODINGA: MATOKEO YA TUME NI BATILI

Aliyekuwa Mgombea wa Kiti cha Urais kupitia Azimio la Umoja, Raila Odinga ameyakataa Matokeo ya Urais na kudai Takwimu zilizotangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ni batili na hakuna mshindi aliyetangazwa kihalali

Amemtuhumu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Wafula Chebukati kwa kuwazuia Makamishna wengine wa Tume kupata taarifa za uhesabu kura kinyume na Sheria ya Tume hiyo

#Democracy #KenyaDecides2022
πŸ‘8πŸ‘Ž4
KENYA: MAAFISA WA IEBC WALIOJITENGA WASEMA MATOKEO YA URAIS YAMEKIUKA KATIBA

Naibu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, Juliana Cherera pamoja na baadhi ya Maafisa wa Tume hiyo wamesema kuwa matokeo yaliyotangazwa hayakuonyesha idadi ya Wapiga Kura waliojiandikisha, kura zilizopigwa au idadi ya kura zilizokataliwa ambapo ni kinyume cha Katiba na Sheria ya Nchi hiyo

#KenyaDecides2022
πŸ‘13πŸ‘Ž3
SAMATTA AREJEA KRC GENK

Mtanzania Mbwana Ally Samatta amerejea KRC Genk ya Ubelgiji akitokea FenerbahΓ§e ya Uturuki

Amerejea kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu kukiwa na uwezekano wa kumnunua na tayari ametambulishwa Genk

Soma > https://jamii.app/SamattaGenk

#JFSports
πŸ‘13πŸ‘6😁1
UCHAGUZI KENYA: Mahakama ya Mjini Bungoma imeruhusu Polisi kumshikilia Didmus Barasa kwa siku 10 ili kusubiri Uchunguzi wa Kesi ya mauaji inayomkabili

> Anadaiwa kumuua Msaidizi wa Mpinzani wake wakati wa zoezi la kuhesabu Kura

Soma - https://jamii.app/AmriYaMahakama

#JFUwajibikaji
πŸ‘7
BOLT KUSITISHA HUDUMA YA MAGARI KWA WATEJA BINAFSI

Bolt imesema uamuzi huo ni kutokana na mazungumzo baina ya Bolt na LATRA kuhusu utaratibu wa utoaji huduma hiyo kuchukua muda mrefu

> Huduma inatarajiwa kusitishwa kuanzia kesho Agosti 17, 2022

Soma https://jamii.app/HudumaZaBolt

#JamiiForums
πŸ‘12πŸ‘Ž4
MDAU: CHANGAMOTO ZA MALEZI YA MTOTO WAKATI WA BALEHE

Miongoni mwa changamoto ni; Usununu usiokuwa na sababu. Mtoto ghalfa tu anakuwa mkali au mkimya na mkorofi asiyetaka kukusikiliza

Anaegemea zaidi kufuata ushawishi wa makundi-rika. Hapa Wataalamu wa Malezi wanashauri uweke bidii katika kuwafahamu Marafiki zake

Tembelea - https://jamii.app/MaleziBalehe
#Malezi
πŸ‘2πŸ”₯1
KENYA: MAAFISA USALAMA WAREJESHWA NYUMBANI KWA RAIS MTEULE RUTO

Hatua hiyo inakuja mwaka mmoja baada ya Maafisa hao kuondolewa kwenye makazi yake kipindi akiwa Naibu Rais

Aidha, Katiba inataka Vyombo vya Usalama ambavyo ni Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF), Idara ya Taifa ya Ujasusi (NIS) na Jeshi la Polisi (NPS) kuanza kumpa Rais Mteule taarifa fupi ya hali ya Usalama

Soma - https://jamii.app/UsalamaKE

#Governance
πŸ‘14
UMUHIMU WA MAZIWA YA NJANO KWA MTOTO MCHANGA (COLOSTRUM)

Maziwa ya Njano ni Maziwa ya Mwanzo, mazito yenye rangi ya njano ambayo hutoka siku chache za mwanzo baada ya kujifungua

Maziwa haya ni Chakula kamili chenye virutubisho vingi, na pia yanatoa Kinga maalum kwa Mtoto dhidi ya Maradhi

Aidha, Maziwa ya Njano humsaidia Mtoto kutoa kinyesi cha mwanzo chenye rangi ya Kijani au Nyeusi ambacho humfanya Mtoto aumwe Tumbo siku za mwanzo kama hatanyonya.

#JamiiForums #BreastfeedingMom #BreastFeeding #WBW2022
πŸ‘13
HOJA: KUKOSA AJIRA KUNACHANGIWA NA UCHAGUZI MBAYA WA MASOMO?

Mdau ndani ya JamiiForums.com anasema Watu wengi husoma fani rahisi ambazo haziwaachii Ujuzi utakaowasaidia kufanya kitu fulani Maishani

Anaeleza kuwa, idadi kubwa ya Wahitimu hukosa ajira kwasababu fani walizosoma ni tofauti na mahitaji

Unakubaliana na Hoja yake?

Mjadala > https://jamii.app/MdauFani
πŸ‘16πŸ€”6πŸ‘Ž2
MBEYA: AJALI YA INYALA, WALIOFARIKI WAFIKIA 19

Polisi wamethibitisha idadi ya vifo katika ajali ya magari matatu iliyotokea Kata ya Inyala Mkoani Mbeya imeongezeka kutoka 8 hadi 19

Ajali hiyo imetokea leo Agosti 16, 2022

Soma > https://jamii.app/AjaliInyala2022

#JamiiForums
😒5πŸ‘2πŸ‘Ž1