JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KENYA: Polisi wa kupambana na ghasia wamepelekwa katika Jimbo la Rongai baada Uchaguzi wa Wabunge kuahirishwa

> Waandamanaji wenye hasira wamechoma matairi ya gari nje ya Kituo cha Kupiga kura cha Mercy Njeri

Soma - https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022 #Democracy
👍6😁1
#JFDATA: Uchaguzi Mkuu wa Kenya unafanyika leo Agosti 9, 2022 ambapo Wapiga Kura 22,120,458 wamesajiliwa huku Vituo vya Kupigia Kura vikiwa 46,229

Wagombea wapatao 16,108 wanawania katika Nafasi mbalimbali. Miongoni mwa Nafasi 6 zinazowaniwa ni Urais, Ugavana, Useneta na Ubunge

#KenyaDecides2022 #Democracy
👍9
KENYA: Wanamgambo wa Al-Shabaab wameripotiwa kuvamia lori lililokuwa na Raia waliokuwa wanaelekea kupiga kura, kuwaamuru kushuka na kisha kulichoma moto

> Wanadaiwa kuwaonya Wenyeji kutoshiriki zoezi la Upigaji wa Kura

Soma - https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022
👍11👎5
UCHAGUZI KENYA: Raia 6,567,869 wamepiga Kura kufikia saa 6 mchana, ikiwa ni 30% tu ya Wapiga Kura wote Nchini humo

Aidha, Wakenya wanaoishi katika Nchi 12 ikiwemo #Tanzania wanaruhusiwa Kupiga Kura katika Vituo vilivyoidhinishwa

Soma - https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022
👍15
KENYA: Tume ya Uchaguzi imeidhinisha Vituo 238 kutumia Sajili za Mikono kupiga kura, ikiwa Mfumo wa Biometriki utasumbua

> Vituo 84 ni katika Jimbo la Makueni na 154 kutoka Matungu, Mumias-Mashariki na Magharibi

Soma - https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022
👍2
KENYA: Mbunge wa Nakuru, David Gikaria anayetetea nafasi yake ktk Uchaguzi wa 2022, anashikiliwa na Polisi baada ya kutokea mabishano kati yake na Askari katika Kituo cha Kupiga Kura

> Gikaria anawania Ubunge kupitia UDA

Soma https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022
👍4
KENYA: Tume ya Uchaguzi imetangaza kuwa katika Jimbo la Dadaab huko Garissa, hadi saa 6 mchana vituo 4 vya kupiga kura vilikuwa havijafunguliwa

> Tume hiyo imesema iwapo ufumbuzi hautapatikana mapema leo zoezi la kura litafanyika kesho

Soma https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022
👍4👎1
Uwepo wa Kamati za Ukaguzi husaidia kuleta #Uwajibikaji katika Usimamizi wa Mapato na Matumizi ya Fedha za Umma katika Taasisi husika

Japokuwa Kamati hizi zipo Kisheria, bado CAG alibaini mapungufu makubwa katika Kamati za Ukaguzi za Taasisi 18 ikiwemo kutohakiki Taarifa za Fedha na Vikao vya Robo Mwaka kutofanyika

#JFUwajibikaji
👍4
UCHAGUZI KENYA: WALIOPIGA KURA NI 56%

Idadi ya waliopiga kura katika Uchaguzi Mkuu leo Agosti 9, 2022 ni Watu 12,065,803 kati ya 22,120,458 waliojiandikisha

> Hiyo ni sawa na 56.17% huku ikikadiriwa idadi ya mwisho inaweza kufikia 60%

Soma https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022 #Democracy
👍6
MAREKANI: Donald Trump amelaani uvamizi wa FBI nyumbani kwake huko Florida, ikiwa ni Sehemu ya uchunguzi unaomkabili tangu kutoka Madarakani

Uvamizi huo unadaiwa kulenga hati za siri zinazodaiwa kutumwa hapo baada ya kuondoka Ikulu 2021

Soma https://jamii.app/TrumpKuchunguzwa

#Democracy
4😁4👍3🤔2
KENYA: MBUNGE ASAKWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI

Polisi wamemtaka Mbunge wa Kimilili, Didmus Barasa ambaye pia ni mgombea Ubunge wa eneo hilo, ajisalimishe

Anatuhumiwa kumuua mlinzi wa mpinzani wake kwa kumshambulia kwa risasi

Soma > https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides #Democracy
👍3
KENYA: RUTO AONGOZA MATOKEO YA AWALI

Hadi kufikia majira ya saa tatu asubuhi, Agosti 10, 2022;

- William Ruto (UDA) anaongoza kwa kura 1,377,854 (49.74%)

- Raila Odinga (AZIMIO) anafuatia akiwa na kura 1,356,726 (48.98%)

Soma https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides #Democracy
🔥11
#KENYA: MALORI MAWILI YANAYODAIWA KUBEBA WAPIGA KURA KUTOKA UGANDA YAKAMATWA

Malori yalinaswa eneo Bunge la #Endebess Kaunti ya Trans Nzoia yakidaiwa kubeba Watu 91

Watu 65 walifanikiwa kutoroka kwa msaada wa Mbunge Robert Pukose

Soma https://jamii.app/KuraEndebess

#KenyaDecides2022
😁8👍6
UCHAGUZI #KENYA: POLISI 2 NA RAIA 1 WAKAMATWA NA KARATASI ZA KURA ZENYE TIKI

Miongoni mwa vifaa vilivyopatikana ni sahili moja ya wapiga kura, Madaftari 2 ya matokeo ya Uchaguzi, pakiti mbili za karatasi za kupigia kura za Urais

Soma - https://jamii.app/KuraKilgoris
#KenyaDecides2022
Mapendekezo yanayotolewa na CAG yanalenga kuboresha mifumo ya Usimamizi, Uwajibikaji na Utendaji wa Serikali

Kutotekelezwa kwa mapendekezo kwa wakati kunafanya madhaifu yaliyobainishwa kuendelea kuwepo, na wakati mwingine kusababisha Serikali kuingia hasara

#JamiiForums #WAJIBU #JFUwajibikaji #Accountability
👍2👎1
KENYA: ZOEZI LA KUHESABU KURA LABADILI MUDA WA KUFUNGUA SHULE

Serikali imesogeza mbele muda wa kufungua Shule hadi Agosti 15, 2022 badala ya Agosti 11, 2022 kwasababu mchakato wa kuhesabu kura za Uchaguzi Mkuu bado unaendelea

Soma > https://jamii.app/ShuleZaKenya

#KenyaDecides2022
👍7
MAHAKAMA YAAGIZA DEREVA "NDUGU ABIRIA" KULIPWA TSH. MILIONI 150

Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni imeamuru Waubani Linyama maarufu 'Ndugu Abiria' kulipwa Tsh. Milioni 150 kutokana na picha yake kutumika katika matangazo ya Biashara bila ridhaa yake

Soma - https://jamii.app/NduguAbiria
👍20🔥5
WAKENYA WALIOPO RWANDA WAMPA KURA NYINGI ODINGA

Raila Odinga amepata Kura 150 huku Mpinzani wake, William akipata Kura 81. George Wajackoyah na Waihiga David Mwaure wamepata Kura 4 kila mmoja

Waliopiga Kura ni watu 239 kati ya 545 waliojiandikisha Rwanda

Fuatilia Yanayojiri > https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022
👍6
UCHAGUZI KENYA: MATOKEO YA AWALI

Kufikia saa 8:55 Mchana

Raila Odinga amepata Kura 1,954,940 sawa na 50.05%

William Ruto amepata Kura 1,895,704 (48.55%)

Kura za George Wajackoyah ni 17,625 (0.45%) na David Waihiga 7,761 (0.19%)

Zaidi > https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022
👍13🎉1
MDAU: MATATIZO MAKUBWA HUZALIWA KWA UTATUZI MBAYA WA TATIZO DOGO

Anasema Wazazi wamekuwa wakitumia nguvu kubwa kurekebisha Watoto wao kuliko Maarifa jambo ambalo linapelekea Watoto wengi kuathirika Kisaikolojia kutokana na vipigo na kufokewa

Udhalilishaji wa Watoto sio njia sahihi ya kutatua tatizo bali ni njia sahihi ya kumuongezea uoga na upweke unaoweza kupelekea maamuzi mabaya mbeleni

Soma zaidi - https://jamii.app/UtatuziMbaya

#Malezi
👍1