JamiiForums
βœ”
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Rushwa ni tatizo kubwa kwa Nchi nyingi. Athari zake ni kubwa zaidi katika Nchi zinazoendelea

Fedha zilizokusudiwa kwa Maendeleo zinapopotea kutokana na Rushwa, utoaji wa Huduma za Msingi kwa Wananchi ikiwemo Maji, Afya na #Elimu hukwama. Hali hii inapelekea ukosefu wa Usawa na #Haki

#KemeaRushwa
πŸ‘3
HALI YA RUSHWA AFRIKA: Kwa mujibu wa Toleo la 10 la Global Corruption Barometer (GCB) – Africa, watu wengi barani humo wanaona Rushwa imeongezeka katika Nchi zao, na jitihada za kupambana na tatizo haziridhishi

Ili kukabiliana na changamoto hii, ni muhimu kwa Mamlaka kuimarisha Uwazi na Uwajibikaji hususan katika Masuala yanayohusisha Fedha za Umma

Zaidi, soma - https://jamii.app/WananchiRushwa

#KemeaRushwa
πŸ‘4
#JFSPORTS: Rais wa Shirikisho la Soka Afrika, Patrice Motsepe ametangaza kuanza kwa #AfricanSuperLeague ambayo itakuwa na zawadi ya Tsh. Bilioni 233.2

Michuano hiyo itakuwa na Timu 24 kutoka Mataifa 16 na #Michezo itaanza Agosti 23, 2022 hadi Mei 24, 2023.

#JamiiForums #Sports
πŸ‘12πŸ‘4
UCHAGUZI KENYA: MBARONI KWA KUKATAA KUHESABU KURA

Jeshi la Polisi limewakamata wasimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kisauni, Kaunti ya #Mombasa baada ya kukataa kuhesabu kura walipobaini Mgombea (hajatajwa) amepata kura nyingi zaidi

Soma - https://jamii.app/KuraKenya
#KenyaDecides2022
πŸ‘3πŸ€”3
MSUMBIJI: Serikali imepiga marufuku Watu kurekodi matukio ya Ajali au majanga, kabla ya kupiga Simu kwa Mamlaka ya Dharura ya kutoa msaada

Hatua hiyo ni katika utekelezaji wa Sheria mpya ya Huduma ya Kitaifa ya Usalama wa Umma

Soma https://jamii.app/MarufukuKurekodi

#DigitalRights
πŸ‘9
UCHAGUZI KENYA: TWITTER KUONESHA MATOKEO YASIYO RASMI

Twitter imeanzisha kipengele cha kuripoti matokeo ya Uchaguzi Mkuu yasiyo rasmi ambapo kuanzia sasa tahadhari itawekwa chini ya matokeo ya kura yaliyowekwa na watu binafsi

Zaidi - https://jamii.app/TwitterKE

#KenyaDecides2022
πŸ‘7
SAKATA LA JENEZA: Klabu ya Simba imewaomba Radhi waumini wa Dini ya Kikristo, Serikali na Jamii baada ya msanii Tundaman kutumia vifaa vya Dini ya Kikristo #SimbaDay

Simba imesema haikufahamu kama atatumia aina hiyo ya maudhui

Soma - https://jamii.app/SimbaRadhi

#JFSports
πŸ‘21πŸ‘Ž3
CHICHARITO YUPO TAYARI KURUDI MAN UNITED

Straika wa zamani wa #ManUnited, Javier Hernandez β€œChicharito” amesema yupo tayari kuichezea timu hiyo bila malipo

Kwa sasa Chicharito (34) anaichezea LA Galaxy ya Marekani

Soma > https://jamii.app/Chicharito

#JFSports
πŸ‘19πŸ‘Ž2😁1
UCHAGUZI KENYA: AJALI YAUA 7 WAKISHEREHEKEA USHINDI WA MBUNGE

Watu saba wamefariki na wengine kujeruhiwa kwenye ajali iliyotokea eneo la Longeld, Samburu Mashariki

Walikuwa wanakwenda kukutana na Mbunge Mteule wa Leerata kabla ya gari kupoteza mwelekeo na kupinduka
πŸ€”9😒8πŸ‘7
KENYA: Tume Huru ya Uchaguzi (IEBC) imetoa ruhusa kwa vyombo vya habari kutoa takwimu za kura kulingana na vyanzo vyao lakini matokeo rasmi yatatangazwa na IEBC baada ya zoezi la kuhesabu kura kukamilika

Soma: https://jamii.app/KenyaVotesResults

#KenyaDecides2022 #Democracy #Kenya2022
πŸ‘18πŸ‘Ž1😱1
UCHAGUZI KENYA: ANAYEDAIWA KUUA KWA RISASI ASHINDA UBUNGE

Didmus Barasa amechaguliwa tena kuwa Mbunge wa Kimilili baada ya kupata kura 26,000 dhidi ya kura 9000 za DAP-K Brian Khaemba

> Barasa anadaiwa kumpiga risasi na kumuua Msaidizi wa Khaemba

Soma - https://jamii.app/BarasaMP

#KenyaDecides2022
πŸ‘8😱1
#SOC2022: BADO SIKU 35. ANDIKA, USHINDE!

Andiko linatakiwa kuchochea mabadiliko chanya katika jamii

Linaweza kujikita kwenye nyanja mbalimbali zikiwemo Elimu, Uchumi, Kilimo n.k

Mwisho wa kuwasilisha ni Septemba 14, 2022

Taarifa zaidi > jamii.app/Shindano2

#StoriesOfChange
πŸ‘2
STORIES OF CHANGE 2022: Mtanzania yeyote kuanzia miaka 18 anaruhusiwa kushiriki

Zawadi zitatolewa kwa Washindi 20

Kwa Maelezo zaidi > jamii.app/Shindano2

#StoriesOfChange #SOC2022
πŸ‘7
#SIERRALEONE: Serikali imetangaza amri ya kutotoka nje kwa Nchi nzima huku kukiwa na maandamano makubwa dhidi ya Serikali

Waandamanaji wanashinikiza Rais Julius Maada Bio ajiuzulu kutokana na kuongezeka kwa mfumuko wa bei

Zaidi - https://jamii.app/SierraLeoneCurfew

#SierraLeoneProtests
πŸ‘11
Kuhusu suala la kutosha au kutokutosha kwa Maziwa ya Mama, Wataalamu wa #Afya wanasema Tafiti zinaonesha asilimia kubwa ya wakina Mama Maziwa yao yanatosha kwa Watoto

Wengi hufikiri hawana Maziwa ya kutosha kwasababu utengenezaji wake pia unahusisha Saikolojia ya Mama mwenyewe. Mawazo mengi, Msongo wa Mawazo au kuchoka hupelekea utoaji wa Maziwa kupungua

#JamiiForums #BreastfeedingMom #WorldBreastfeedingWeek
πŸ‘7
Uchambuzi wa Hoja za CAG unaonesha pamoja na kupata Hati Safi, Taasisi nyingi za Umma bado zina kasoro za Kiutendaji na zinahitaji kufuatiliwa ili kudhibiti uwezekano wa kuwepo kwa vitendo vya Rushwa na Ubadhirifu wa Rasilimali za Umma

Badala ya kuridhika na Hati Safi zilizotolewa na CAG, ni muhimu Bunge na Kamati zake kufuatilia utendaji wa Serikali na Taasisi zake na kuzingatia uzito wa Hoja pamoja na athari zake kwa Jamii

#JFUwajibikaji
πŸ‘7😁1
KENYA: ODINGA AMPITA RUTO KWA IDADI YA KURA

Kwa Mujibu wa Citizen, kufikia saa 6:30 mchana Raila Odinga alikuwa na Kura 6,431,752 (49.46%), William Ruto 6,389,957 (49.14%) Prof. Wajackoyah 56,430 (0.43%) na Waihiga 28,973 (0.22%)

Soma https://jamii.app/OdingaRuto

#KenyaDecides2022
πŸ‘11
UCHAGUZI KENYA: Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Huru na Mipaka (IEBC), Wafula Chebukati amevionya Vyombo vya Habari kutotangaza Mshindi wa Kura ya Urais kabla ya Mamlaka hiyo

Amesema atakayeshinda atatangazwa na Tume

Soma - https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022
πŸ‘8
WAANGALIZI WAPONGEZA MCHAKATO WA UCHAGUZI KENYA

Kiongozi wa Wasimamizi hao kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jakaya Kikwete amesema Wasimamizi wamefuatilia Vituo vyote kuanzia wakati wa Kampeni, Upigaji Kura hadi sasa

Soma - https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022
πŸ‘10😁2
KATAVI: Machia Mbasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kupanga njama za kumuua Mabula Ntemange, anayedaiwa kuwa na Uhusiano na Mkewe yeye akiwa jela

Pia, amemtuhumu Mabula kwa kuchukua kodi katika Vibanda vyake vya Biashara

Soma https://jamii.app/NjamaMauaji

#JFMatukio
πŸ‘7