JamiiForums
βœ”
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RIPOTI MAUAJI WATU 33 MALI: UN wameeleza Wanajeshi wa #Mali na Wanamgambo wa Kundi la Wagner la Urusi ndio waliua raia 33 (29 wa Mauritania, 4 wa Mali)

Tukio hilo la Machi 5, 2022 lilisababisha mvutano kati ya Nchi ya Mali na #Mauritania

Soma > https://jamii.app/RipotiYaUN

#JFLeo
πŸ‘6πŸ€”1
KUNYONYESHA KUNAPUNGUZA HATARI YA MAGONJWA KWA MAMA NA MTOTO

Mtoto anaponyonya anapunguza hatari ya kupata Pumu, Unene kupita kiasi, Aina 1 ya kisukari, Ugonjwa mkali wa kupumua kwa chini, Maambukizi ya sikio na Maambukizi ktk Utumbo

Mama anaponyonyesha anapunguza hatari ya kupata Shinikizo la Damu , Aina ya 2 ya Kisukari, Saratani ya Ovari na Saratani ya Matiti

Soma - https://jamii.app/KunyonyeshaMtoto

#WBW2022
πŸ‘12πŸ₯°1
UWANJA WA MKAPA: YANGA 0-2 VIPERS

Yanga imepoteza mchezo dhidi ya Vipers SC ya Uganda katika kilele cha kukamilisha Wiki ya Mwananchi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, leo Jumamosi Agosti 6, 2022

Soma > https://jamii.app/Yanga0Vipers2

#JFSports #Yanga #JamiiForums
😁33πŸ‘9😒4πŸ‘Ž1
MANARA, HERSI KIKAANGONI TFF

Sekretarieti ya TFF imewafungulia mashtaka ya kimaadili Rais wa Yanga, Mhandisi Hersi Said na Haji Manara

Sababu ni Manara kushindwa kutekeleza adhabu ya kutojihusisha na Mpira kwa Miaka 2

Soma > https://jamii.app/MashtakaYanga

#JFSports
πŸ‘31πŸ€”11❀1
TETESI: MAN. UNITED YAGEUKA KWA LEROY SANE

Manchester United inataka kumsajili Winga wa Bayern Munich, Leroy Sane na imeanza mazungumzo na Bayern

Sane ambaye amewahi kuichezea Man. City ana mkataba wa miaka mitatu kutumikia Bayern

Soma https://jamii.app/UsajiliWaSane

#JFSports
😁4πŸ€”2
USHAURI: UNAMSAIDIAJE MTOTO MWENYE URAIBU WA MICHEZO KWENYE SIMU?

Mdau wa JF anasema Mtoto wake wa miaka 5 amekuwa na uraibu wa 'Games' za kwenye simu janja, na akiona Smartphone anachanganyikiwa

Afanye nini ili Mtoto asizidi kuwa na uraibu huu?

Mjadala > https://jamii.app/MtotoGameSimu
πŸ‘2
Mdau anashauri kujiongezea ujuzi na maarifa ya Kiuchumi, #Afya, Kilimo, #Biashara na Kijamii kwa kusoma kozi fupi ambazo hutolewa bure Mtandaoni

Pia amesisitiza kufanya β€˜Google’ na β€˜YouTube’ marafiki ktk Maisha ya kila siku

Soma - https://jamii.app/TeknolojiaElimu

#DigitalWorld
πŸ‘17
IVORY COAST: Rais Alassane Ouattara ametoa Msamaha kwa Mtangulizi wake, Laurent Gbagbo aliyehukumiwa kifungo cha Miaka 20 jela

Mwaka 2018 Gbagbo alikutwa na hatia ya kuhusika katika machafuko ya Kisiasa baada ya Uchaguzi wa Mwaka 2011

Soma https://jamii.app/MsamahaWaRais

#Governance
πŸ‘12πŸ‘Ž1
EPL: MAN UNITED 1-2 BRIGHTON

Manchester United ikiwa nyumbani Uwanja wa Old Trafford imefungwa goli 2-1 ktk mchezo wake wa kwanza wa Premier League 2022/23, leo Agosti 7, 2022

Cristiano Ronaldo alianzia benchi katika mchezo huo

Soma > https://jamii.app/ManUYafungwa

#EPL #MUNBHA #mufc
😁12πŸ‘11πŸ‘Ž3πŸ”₯1
LEO KATIKA HISTORIA: Miaka 24 iliyopita leo (Agosti 07, 1998) Balozi za Marekani Dar es Salaam (Tanzania) na Nairobi (Kenya) zilishambuliwa na Magaidi

#JFHistoria
πŸ‘14πŸ‘Ž3😒2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Tunawatakia Wiki njema. Usiache kuwa WEWE siku zote!

#JamiiForums
πŸ‘16πŸ‘Ž2
Sikukuu ya Maonesho ya Wakulima 'Nane Nane' iliadhimishwa kwa mara ya kwanza Mwaka 1977 ili kuongezea nguvu Sera ya Serikali ya wakati huo ya 'Siasa ni Kilimo'

Jamii Forums inakutakia maadhimisho mema ya Siku hii. Asante kwa kuendelea kuwa sehemu ya Familia yetu

#JamiiForums
πŸ‘13
UCHAGUZI KENYA: Benedict Manzin, Mchambuzi wa Siasa za Afrika-Kusini mwa Jangwa la Sahara amesema Wafuasi wa William Ruto na Raila Odinga wanasambaza taarifa zinazodai Wapinzani wao wana njama za kuiba kura

Mashirika ya Kiraia Nchini #Kenya na Shirika la Uangalizi yameonya kwamba Taarifa hizo potofu zinahatarisha #Demokrasia na yametaka Mitandao ya Kijamii kuchukua hatua

Soma - https://jamii.app/SMUchaguziKE

#KenyaDecides
πŸ‘12
Ukaguzi wa CAG umeonesha kumekuwa na utolewaji wa Fedha zaidi ya kiasi kilichoidhinishwa na Bunge kwa baadhi ya Halmashauri

Hii inaweza kusababisha Fedha za Umma kutumika vibaya na Watumishi wa Halmashauri hizo kwasababu Fedha iliyopelekwa ni kubwa kulinganisha na mahitaji halisi

#JFUwajibikaji
πŸ‘5
Wakiongozwa na Misri, #Israel na #Palestina wamekubaliana kusitisha mapigano katika Ukanda wa #Gaza yaliyofanyika kwa Siku tatu mfululizo

Watu 44 wameuawa ambapo kati yao Watoto ni 15, huku Wapalestina 350 wakijeruhiwa

Soma > https://jamii.app/IsraelGazaChaos

#JFLeo #GazaUnderAttack
πŸ‘6
Rushwa inakwamisha Maendeleo ya Kiuchumi, Kijamii pamoja na Kisiasa. Pia ni kikwazo kikubwa kwa #UtawalaBora kwa Mataifa mengi Barani Afrika na Duniani kwa ujumla

Rushwa huathiri Ustawi wa watu binafsi, Familia na Jamii kwa ujumla. Hata hivyo, Wahanga wakubwa wa tatizo hili ni Watu wa Hali ya Chini Kiuchumi

Unashauri nini kifanyike kuimarisha Mapambano dhidi ya Rushwa?

#KemeaRushwa #JamiiForums
πŸ‘3
ETHIOPIA: WAASI WA #TIGRAY WAGOMEA MAZUNGUMZO YA AMANI

Wamesema hawawezi kuzungumza ikiwa Watu wao bado hawana huduma za Mawasiliano, Benki na Umeme

> Mnamo Mwezi Julai Waasi hao walikubali mazungumzo iwapo huduma hizo zingerejeshwa

Soma https://jamii.app/TigrayPeaceTalks

#TigrayCrisis
πŸ‘4πŸ‘1
RB LEIPZIG YAAFIKIANA NA CHELSEA KUMSAJILI TIMO WERNER

RB Leipzig imekubaliana na Chelsea kumnunua Mshambuliaji Timo Werner kwa Paundi Milioni 25.3 (Tsh. 70,840,000,000)

Werner anataka kurejea katika klabu yake ya zamani ili kujiweka sawa kwa ajili ya Kombe la Dunia

#JFSports
πŸ‘8
SOMALIA: Maeneo ya karibu na Ikulu ya Rais wa #Somalia Mjini #Mogadishu yameshambuliwa kwa mabomu muda mfupi baada ya Bunge kuidhinisha Baraza la Mawaziri lenye Wajumbe 75

Somalia, taifa lililopo katika pembe ya Afrika linakabiliwa na Umasikini na janga la njaa

Soma - https://jamii.app/BomuIkuluSom
πŸ‘7
NIGERIA: Jeshi limetangaza kumuua Kiongozi wa Kundi la Boko Haram, Alhaji Modu β€˜Bem Bem’ katika mashambulizi ya anga yaliyofanyika Agosti 3, 2022 kwenye Jimbo la Borno

> Pia, Wanamgambo 27 wa kundi hilo wameua katika mashambulizi

Soma https://jamii.app/28KilledInNigeria

#JamiiForums
πŸ‘11