JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Majukwaa ya Kidigitali yanaweza kuwa na mchango mkubwa katika kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kupitia;

- Fursa za Ubunifu na #Ujasiriamali ambazo husaidia kuinua Uchumi

- Utoaji Elimu/Maarifa ya Kidigitali yanayohitajika katika Soko la #Ajira

Zaidi, soma > https://jamii.app/DigitalSDGs
👍5
DAR: Msanii wa Nigeria, Kizz Daniel anashikiliwa Kituo cha Polisi Oysterbay baada ya kupokea malipo ya kuburudisha katika Ukumbi wa Next Door Arena na kushindwa kutokea eneo husika

> Aidha, 'Passport' yake inashikiliwa na Polisi

Soma - https://jamii.app/KizzDanielArrested

#Arts #JFSanaa
👍19
DR-CONGO: Waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) waliopo Mashariki mwa Nchi hiyo wamewaua takriban Watu 16 akiwemo Kapteni wa Jeshi katika mashambulizi mapya dhidi ya Vijiji

> Waasi hao wanadaiwa kulenga maeneo ya Kandoyi na Bandiboli

Soma https://jamii.app/DRCRebelsAttack

#HumanRights
👍3
MANCHESTER UNITED YATAKA KUMNUNUA RABIOT

- Man. Utd imekubaliana na Juventus kumnunua Kiungo Adrien Rabiot (27) kwa ada ambayo bado haijafahamika

- Hata hivyo, Man. Utd bado inajadiliana na Wakala wa Kiungo huyo ambaye pia ni mama yake ili kuafikiana matakwa binafsi

#JFSports
👍5
UCHAGUZI KENYA: Wasimamizi 4 wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) wamefukuzwa kwa madai ya kukutana na Mgombea nyumbani kwake kinyume na maadili ya Uchaguzi

Watuhumiwa wanashikiliwa na Polisi wakisubiri kufikishwa Mahakamani

Soma https://jamii.app/MaafisaWafukuzwa

#KenyaDecides
👍12👏4
SIMBA DAY: SIMBA 2-0 SAINT GEORGE

Simba imeshinda magoli 2-0 dhidi ya Timu ya Saint George ya Ethiopia katika Tamasha la #SimbaDay, Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam leo Agosti 8, 2022

Magoli yamefungwa na Kibu Denis na Nelson Okwa

Soma > https://jamii.app/Simba2George0

#JFSports
👍17👏1
KENYA: Tume ya Uchaguzi imesitisha Uchaguzi wa Ugavana katika Kaunti za Kakamega na Mombasa, kutokana na makosa ya uchapishaji kwenye karatasi za kupigia kura

Tarehe nyingine ya Kupiga kura itatangazwa hapo baadaye

Soma https://jamii.app/UchaguziUgavana

#KenyaDecides
👍13🔥2
WAKENYA KUAMUA RAIS AJAYE

Taifa hilo litamchagua Rais wake wa Tano leo Agosti 9, 2022

Wapiga Kura wanaotarajiwa kushiriki zoezi ni 22,120,458

Wagombea Urais ni pamoja na George Wajackoyah, David Mwaure, William Ruto na Raila Odinga

Fuatilia Yanayojiri > https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides
👍12🔥3
PICHA: Mgombea Urais wa Kenya, William Ruto amepiga Kura katika Shule ya Msingi Kosachei huko Sugoi. Mgombea Mwenza wake, Rigathi Gachagua naye amepiga Kura eneo la Mathira, Kaunti ya Nyeri

Mgombea Mwenza wa Raila Odinga kupitia Azimio la Umoja, Martha Karua amepiga Kura huko Gichugu, Kaunti ya Kirinyaga na Mgombea David Waihiga Mwaure amepiga Kura yake Jijini Nairobi

#KenyaDecides2022
👍12🎉2
KENYATTA APIGA KURA: Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amepiga kura eneo Gatundu Kusini, Kaunti ya Kiambu huku akiwataka Wakenya kuipa Tume Huru ya Uchaguzi (IEBC) muda na nafasi ya kujumlisha na kutangaza matokeo kwa uhuru

Amesema "Matumaini ya Wakenya wengi kuwa uchaguzi huu utakuwa Huru na Haki, Watu wapige kura na kurudi nyumbani kwa amani"

#Democracy #KenyaDecides2022
👍9👏1
KENYA: Mgombea Ubunge wa Kenya Kwanza, Hamisi Butichi anashikiliwa na Polisi baada ya kukutwa na mapanga na silaha nyingine katika Kituo cha Kupigia Kura

Soma https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022 #Democracy
🤔7👍4
KENYA: Raia 11 wamewasilisha ombi ktk Mahakama ya Juu kuzuia kuapishwa kwa William Ruto na Rigathi Gachagua ikiwa watashinda, wakisema kuapishwa kwao kutakuwa ni ukiukwaji wa Katiba

> Wawili hao wametajwa kuwa na kashfa za Ufisadi na Uhujumu Uchumi

Soma - https://jamii.app/KuapishwaRuto

#Democracy #KenyaDecides2022
👍18
UCHAGUZI KENYA: Mwanaume mmoja amejeruhiwa kwa risasi katika eneo la Eldoret nje ya ofisi ya mmoja wa Wagombea Ugavana wa Uasin Gishu

> Jeshi la Polisi limesema uchunguzi wa kilichotokea unaendelea

Soma https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides #Democracy #Kenya2022
👍6🤔1
KENYA: Mgombea wa Urais wa UDA, William Ruto amesema yupo tayari kukubali matokeo ya mchakato wa Uchaguzi Huru na wa Haki

> Ruto amesema kwa kawaida matatizo ya Uchaguzi huja pale ambapo Wagombea hukataa matokeo

Soma https://jamii.app/KenyaElect2022

#Democracy #KenyaDecides2022
👍8🤔1
UCHAGUZI KENYA: Mgombea Mwenza wa Urais wa UDA, Rigathi Gachagua alilazimika kusubiri kwa muda mrefu baada ya Mfumo wa Kibiomertiki kushindwa kumtambua

> Hata hivyo alipiga kura kupitia Orodha ya Wapiga Kura iliyochapishwa

Soma https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022
👍81
KENYA: Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imesimamisha Uchaguzi wa Wabunge wa Jimbo la Rongai, Kaunti ya Nakuru baada majina ya Wagombea, Masanduku ya Kura na Karatasi za Kupigia Kura kukosekana kwenye Vituo vya Kupigia Kura

Soma - https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022
👍6
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
NAIROBI, KENYA: Mgombea Urais kupitia Azimio la Umoja, Raila Odinga amesindikizwa na kundi kubwa la Wafuasi wake katika Kituo cha Kura kilichopo Shule ya Msingi Old Kibera alipokwenda kupiga kura

> Odinga anagombea nafasi hiyo kwa mara ya 5

Soma - https://jamii.app/KenyaElect2022

#Democracy #KenyaDecides2022
👍12
UCHAGUZI KENYA: Mgombea Urais wa Chama cha Roots, Prof. George Wajackoyah ameshindwa kupiga kura katika Kituo cha Matungu baada ya mfumo wa biometriki kutomtambua

Taratibu za kuwezesha Upigaji kura zinaendelea

Soma - https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022
👍7