JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MYANMAR: Kiongozi wa Kijeshi, Min Aung Hlaing ameongeza muda wa hali ya hatari kwa Miezi 6 huku akisema ni juhudi za kutekeleza mpango wa amani

Jeshi lilitangaza hali ya hatari Februari 2021 baada ya mapinduzi ya Kijeshi

Soma https://jamii.app/HatariMyanmar

#JFDemokrasia
🤔4
KENYA: Siku 10 baada ya Serikali kushusha bei ya Unga wa Mahindi kuwa Ksh. 100 (Tsh. 1,960) toka Ksh. 200 (Tsh. 3,920) kwa Kilogramu 2, uhaba wa bidhaa hiyo umekuwa mkubwa Madukani

- Serikali imewaonya wanaoficha na kutangaza msako kuanzia Agosti Mosi

Soma - https://jamii.app/UngaWaUgaliKE
👍5
MDAU: WATOTO WANAHITAJI ULINZI KIPINDI HIKI CHA LIKIZO YA SENSA

- Anasema Mitaani pamefurika kila aina ya Makundi na Watu wa rika tofauti. Huu ni muda wa Wazazi/Walezi kuchukua tahadhari ya kulinda Watoto wanapocheza

- Anashauri Wazazi kupangilia muda wao vizuri kwaajili ya usalama wa Watoto, ama kuwakabidhi sehemu salama pindi wasipokuwepo

Soma - https://jamii.app/WatotoSensa

#Malezi #Parenting
👍15
FAIDA ZA 'KIWIFRUIT' KIAFYA

1. Huimarisha Kinga na kuzuia Magonjwa: Kiwifruit moja huzalisha karibu 80% ya Vitamini C inayohitajiwa na Mwili kwa siku

2. Husaidia kuondoa Shinikizo la Damu na kuboresha Afya ya Moyo: Linaweza kupunguza hatari ya Kiharusi na Ugonjwa wa Moyo

Soma - https://jamii.app/BenefitsKiwi

#JFAfya #Health
👍12
Mdau wa JamiiForums.com anasema Watu wengi wenye #Biashara na Kampuni hawaajiri Vijana kwa kuhofia kuhujumiwa na huishia kuajiri Watu wa makamo wakiamini hawana Tamaa kama Vijana

Unakubaliana kwa kiasi gani na hoja hii?

Mjadala zaidi - https://jamii.app/VijanaSokoAjira

#JFMaisha
👍19👎4
MDAU: FANYA YAFUATAYO KUWAEPUSHA WATOTO WAKO NA JANGA LA AJIRA

1. Tutambue Vipaji na Vipawa vya Watoto mapema na kuviendeleza. Wafundishe Wanao kile ulichonacho. Ikiwa ni Mfanyabiashara anza kumzoesha kusimamia na kuijua #Biashara yako

2. Wakati wa likizo jaribu kumshikiza Mwanao katika maeneo yatakayomsaidia kuwa na ujuzi na Maarifa mbalimbali. Usikomae na 'tuition' tu ikiwa maendeleo yake sio mabaya.

Soma zaidi - https://jamii.app/UjuziWatoto

#Ajira #JFMdau #Maisha
👍15
Ripoti ya CAG 2020/21 imeonesha kumekuwepo na mianya ya uvujaji wa Mapato ambayo kama yangesimamiwa kwa umakini, yangeweza kuleta tija kwa Jamii

Mawakala kukusanya Mapato na kutoyawasilisha kwenye Halmashauri, ama Halmashauri kutokusanya Mapato kutoka vyanzo mbalimbali ni kiashiria cha Rushwa na Ubadhirifu wa Fedha za Umma

#JamiiForums #WAJIBU #JFUwajibikaji #KemeaRushwa
😁4👍2
Machache ambayo Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezungumza katika Uapisho wa Wakuu wa Mikoa leo Agosti 01, 2022

Soma - https://jamii.app/UteuziWateule

#Governance
👍6👎1😁1
Nukuu za Rais Samia Suluhu Hassan leo baada ya Uapisho wa Viongozi Ikulu, Dar es Salaam

#JamiiForums #Governance
👍6
MALI YAISHUTUMU UFARANSA KWA UKOLONI MAMBOLEO

Rais Emmanuel Macron alikaririwa akisema Mataifa ya Kanda yalikuwa na jukumu la kuhakikisha Raia wa #Mali wanaweza kuonesha Nguvu ya Umma

Kauli yake ilitafsiriwa kuwa ya kichochezi na Jeshi la Mali

Soma https://jamii.app/ShutumaMali

#JFDiplomasia
👍10
AFRIKA KUSINI: Wanaume 82 wanashikiliwa kwa madai ya kubaka kundi la Wanawake waliokuwa wanarekodi video ya Muziki ktk eneo la Mgodi, Johannesburg

Raia wametoa wito wa kuhasiwa kwa kemikali watuhumiwa watakaopatikana na hatia

Soma - https://jamii.app/UbakajiWaMakundi

#UkatiliKijinsia
🤔11👍4👎1🥰1
MAMA ADAIWA KUMUUA MWANAYE WA MIAKA MITATU KWA FIMBO

Mtuhumiwa (27) alimchapa mwanaye sehemu mbalimbali za mwili, chanzo kikidaiwa ni mtoto kufungua bomba na kuchezea maji ya baridi

Jeshi la Polisi limesema Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea

Soma https://jamii.app/AmuuaMwanaye

#HakiMtoto
😢15👎3👍2🤔1
VIELELEZO VYA WIZI VYAIBWA KITUO CHA POLISI

Mali zilizokuwa Kituo Kidogo cha Polisi Uchira, Wilaya ya Moshi, Kilimanjaro kama vielelezo zimeibwa

Anayedaiwa kuiba ni mtuhumiwa wa kesi hiyo, alitaka kuharibu ushahidi wa kesi yake

Soma > https://jamii.app/TukioLaWizi

#JFMatukio
😁41👍5👏1
MAREKANI YAMUUA KIONGOZI WA AL QAEDA

Rais Biden amesema Ayman al-Zawahiri ameuawa kwa shambulio la 'Drone' Jijini Kabul Nchini Afghanistan. Inaelezwa, alihusika katika mashambulizi ya Septemba 11, 2001 yaliyoua takriban watu 3,000

Kifo chake kimetajwa kuwa pigo kubwa zaidi kwa Kundi hilo tangu kuuawa kwa Osama bin Laden mwaka 2011

Soma https://jamii.app/ZawahiriKilled
👍18😁2👎1🎉1
MDAU: MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA JAMII YENYE MTAZAMO HASI

- Jithamini ujue thamani yako

- Kipaumbele chako kiwe kutenda mema pasipo kujali mtazamo wa wengine

- Ishi kwa tahadhari hususan kwa watu wanaokuzunguka

- Fahamu aina ya watu wanaokuzunguka pamoja na mtazamo wao

- Kuwa mwepesi kusamehe

Msome > https://jamii.app/MaishaYaJamii

#JFMaisha
👍11