JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KENYA: Serikali imetangaza kufungwa ghafla kwa shule zote kuanzia Agosti 2, 2022 kabla ya Uchaguzi Mkuu na kufunguliwa Agosti 11, 2022

> Wanafunzi ambao tayari wameanza mitihani ya katikati ya Muhula wamebaki na sintofahamu

Soma - https://jamii.app/ShuleKenya

#Kenya2022
πŸ‘13πŸ€”3
RAIS WA ZAMBIA AWASILI TANZANIA

- Rais Hakainde Hichilema amewasili Nchini kwa ziara ya Kiserikali ya siku 1 na kupokelewa na Rais Samia Suluhu

- Ziara inakusudia kuimarisha zaidi mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Zambia na Tanzania

Fuatilia https://jamii.app/Hichilema-TZ

#JFSiasa
πŸ‘13
MDAU: WATANZANIA WANASTAHILI UFAFANUZI WA GHARAMA ZA INTANETI KUPANDA

Anasema Watu wengi hawaelewi na bado hawajapata ufafanuzi wa sababu zinazopelekea Vifurushi vya Intaneti kupanda mara kwa mara

Anaeleza, kupanda kwa gharama za Intaneti kuna athari mbalimbali kwa Wananchi ikiwemo kupunguza motisha ya kutafuta maarifa Mtandaoni

Soma - https://jamii.app/Vifurushi05

#DigitalRights
πŸ‘27πŸ‘Ž1
Ushiriki wa Umma katika masuala ya Kisiasa na Kidemokrasia ni sehemu muhimu ya Utawala wa Demokrasia

Wahusika wa mchakato wa Kusikiliza, Kuhoji, Kutafakari na Kufanya maamuzi yoyote katika Nchi ni Wananchi wenyewe

Zaidi, soma > https://jamii.app/UshirikiHuru

#Democracy #Governance
πŸ‘2
SERIKALI YAENDELEZA MARUFUKU YA β€˜LUMBESA’

Makamu wa Rais, Dkt. Mpango amezuia vipimo visivyo rasmi ktk ununuzi wa mazao ikiwemo β€˜lumbesa’

Hii si mara ya kwanza β€˜lumbesa’ kuzuiwa. Waziri Mkuu Majaliwa aliizuia akisema inatumika kuwaibia Wakulima

Soma https://jamii.app/Mpango-lumbesa

#JFLeo
πŸ‘10
FEDHA ZA UMMA: USIMAMIZI DHAIFU HUPELEKEA MATUMIZI YASIYO NA TIJA

Ripoti ya CAG 2020/21 inaonesha udhaifu katika usimamizi wa matumizi ya Fedha za Umma

Hii imepelekea kuwepo matumizi nje ya Bajeti, matumizi yasiyo na tija na kufanyika malipo bila kudai risiti

#JFUwajibikaji
πŸ‘4
#JFDATA: Kwa mujibu wa Shirika la UNICEF, ushahidi katika baadhi ya Nchi unaonesha Watoto wenye Ulemavu wana uwezekano mkubwa wa kutengwa Shuleni kuliko wenzao wasio na Ulemavu

Ili kuwajumuisha Watoto wenye Ulemavu, ni muhimu kuwa na Mikakati ya kupambana na vikwazo vinavyowakwamisha

Fahamu zaidi > https://jamii.app/DataUlemavu

#HakiMtoto
πŸ‘8
KENYA: Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limesema Serikali kutowawajibisha Polisi kwa tuhuma za mauaji baada ya uchaguzi wa mwaka 2017, kunaongeza hatari ya kutumia Mamlaka yao vibaya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa wiki ijayo

Soma https://jamii.app/KenyaPolisi
πŸ‘6
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Mashirika (isipokuwa machache) yamekuwa hayafanyi vizuri, na kupelekea mengi kukopa ili kutoa Gawio katika kipindi maalum kwa miaka iliyopita

Katika Ripoti ya 2020/21, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alisema Mashirika 16 yana Madeni zaidi ya Mtaji. Alieleza, yalikuwa na uwiano usioridhisha wa Madeni kwa Mtaji kwa zaidi ya 100%

#JFUwajibikaji
πŸ‘8
SOMALIA: Waziri Mkuu ametangaza kuteuliwa kwa Mukhtar Robow (Mwanzilishi Mwenza wa Kundi la Al-Shabaab) kuwa Waziri wa Dini

> Hatua hiyo inatajwa inaweza kusaidia kuimarisha vita dhidi ya Waasi na kuzuia vita vya wenyewe kwa wenyewe

Soma https://jamii.app/WaziriSomalia
πŸ‘14πŸ‘4πŸ€”1
MADHARA YA KUTUMIA SHISHA

Baadhi yanayoweza kujitokeza kwa mtumiaji; Saratani, Matatizo ya Moyo, Kuharibika Fizi, Fangasi na Kifua kikuu

Kuzaa Njiti (wanaotumia wakiwa wajawazito), Kupoteza Uwezo za Kujamiiana, Kuchakaa kwa ngozi

Soka > https://jamii.app/MadharaYaShisha

#JFAfya
πŸ‘9
UTAFITI: KUKOSA USINGIZI HUPUNGUZA NGUVU ZA KIUME

Utafiti huo wa kwenye jarida la habari za #Afya, LiveScience unasema Wanaume ambao hulala chini ya Saa sita wanaweza kutungisha Mimba kwa 31% huku wanaolala kwa Saa tisa wakiwa na asilimia 49

Soma - https://jamii.app/UsingiziKiume
#Afya
πŸ‘15πŸ€”3πŸ’©3πŸ‘1
MDAU: JINSI YA KUJIANDAA MWENZA WAKO ANAPOPATA UJAUZITO

- Mnapogundua ana Mimba anzeni kuweka akiba kulingana na uwezo wenu. Kama mnaishi pamoja, Mimba ikifikisha Miezi Minne anzeni kuomba na Mtoto aliye Tumboni

- Mjamzito azingatie vyakula vyote vyenye virutubisho. Kama una kipato kidogo anza kununua vitu vya Mtoto taratibu usisubiri mpaka Mama ajifungue

Zaidi, soma - https://jamii.app/MimbaMaandalizi

#JFMaisha
πŸ‘14
UCHAGUZI KENYA: Watu wa Jamii ya Washona watapiga kura kwa mara ya kwanza ktk Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9, 2022

Kundi la kwanza la Washona liliwasili Kenya likitokea #Zimbabwe takriban Miaka 60 iliyopita na kupewa uraia Mwaka 2020

Soma - https://jamii.app/WashonaElectKE

#KenyaDecides2022
πŸ‘6
HUDUMA YA INTANETI: GHARAMA ZINAKUATHIRI KWA KIWANGO GANI?

Kutumia Intaneti bado ni gharama kubwa kwa Wananchi katika Nchi nyingi zenye Uchumi wa Chini na Kati

Gharama kubwa za kujiunga zinakwamisha Mamilioni ya Watu kutumia Huduma ya Intaneti kikamilifu

Unatumia kiasi gani kugharamia Huduma hii ili kufanikisha shughuli zako za kila siku?

Zaidi, soma > https://jamii.app/Internet001

#DigitalRights
πŸ‘10
KIFO CHA MWENYEKITI: FAMILIA YADAI KAUAWA, POLISI YAKANUSHA

Mwili wa Mwenyekiti wa Kijiji cha Byamtemba Mkoani Kagera, Jonathan Bunyaga uliokotwa kando ya barabara ya Bukoba - Mtukula

Ndugu wamedai kubaini majeraha yaliyoonesha alichomwa na kitu chenye ncha kali. Kamanda wa Polisi, William Mwampaghale amesema chanzo cha kifo ni ajali ya pikipiki kugongana

Soma - https://jamii.app/UtataKifoKagera
πŸ‘5🀯3
Kwa mwaka 2020/21, Serikali ilishindwa kukusanya 10% ya Bajeti iliyoidhinishwa, ikiwa ni ongezeko la 5% ukilinganisha na mwaka 2019/20. Hii inafanya utekelezaji wa Bajeti kutofikia Malengo yaliyopangwa

Kushindwa kukusanya Mapato kulingana na Bajeti iliyoidhinishwa inadhihirisha Bajeti Iliyopangwa haikuwa na uhalisia, hivyo matarajio ya Wananchi kutofikiwa

#JFUwajibikaji
πŸ‘7
#JFSPORTS: Kocha wa #ManUnited, Erik ten Hag amekasirishwa na Cristiano Ronaldo kuondoka uwanjani wakati mchezo dhidi ya Rayo Vallecano ukiendelea

> Kocha huyo amesema "Sikubaliani na alichofanya, sisi ni timu unatakiwa kukaa hadi mwisho"

Soma https://jamii.app/CR7AmkeraKocha
πŸ‘14πŸ‘1
UINGEREZA: Upigaji kura kwa njia ya Mtandao ili kumpata Mrithi wa #BorisJohnson umesogezwa hadi Agosti 11, 2022 kutokana na hofu ya kudukuliwa

Wataalamu wa Mtandao wa Serikali wameibua wasiwasi juu ya uwezekano wa kubadilishwa kwa kura

Soma: https://jamii.app/HofuUdukuzi

#Democracy
πŸ‘7πŸ‘Ž3
SERIKALI YASITISHA MABADILIKO HUDUMA ZA NHIF

Imesitisha mabadiliko ya utaratibu mpya ulioanza kutumika Agosti 1, 2022 baada ya malalamiko ya Wateja

Mabadiliko yaliweka idadi ya mahudhurio hospitalini na utoaji kibali kwa huduma kama MRI, CT SCAN

Soma https://jamii.app/TamkoLaBima
#JFAfya
πŸ‘8πŸ‘Ž1