JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MDAU: KWANINI BEI YA MAFUTA INAZIDI KUPANDA NCHINI?

Anasema gharama za maisha zinazidi kupanda kutokana na ongezeko la bei ya mafuta japokuwa Takwimu za Soko la Dunia zinaonesha mafuta yamekuwa yakishuka miezi ya karibuni

Anahoji: Mamlaka inatumia kigezo gani kupandisha bei?

Mjadala > https://jamii.app/KupandaKwaMafuta
👍13😢1
DR-CONGO: Serikali imemtaka Msemaji wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa, Mathias Gillmann kuondoka Nchini humo haraka iwezekanavyo

> Ameshutumiwa kwa kutoa "taarifa zisizoeleweka na zisizofaa" kuhusiana na Nchi hiyo

Soma: https://jamii.app/MsemajiUN

#Diplomacy
👏8👍4😱1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
BONDIA MTANZANIA AINGIA NUSU FAINALI JUMUIYA YA MADOLA

Yusuf Changalawe amemtoa kwa TKO Arthur Lingelier na kutinga Nusu Fainali katika michezo ya Jumuiya ya Madola

Kwa matokeo hayo, Tanzania imepata uhakika wa medali

Soma - https://jamii.app/BondiaMadola2022

#JFSports
👍16👏5
57% YA WATOTO WACHANGA NCHINI WANANYONYESHWA INAVYOTAKIWA

Watoto hao ni wenye umri chini ya miezi sita

Vilevile, Tafiti zinaonesha asilimia 43 tu ya Watoto hunyonyeshwa hadi kipindi cha miaka miwili na kuendelea

Soma - https://jamii.app/Unyonyeshaji

#WorldBreastfeedingWeek
👍8
- Mdau wa JamiiForums.com anaomba msaada wa mbinu anazoweza kuzitumia ili kumfanya Mtoto wake mwenye Miaka 8 aache kukojoa Kitandani na kunyonya kidole

- Licha ya kumwamsha Mtoto usiku hata mara mbili ila bado atakojoa. Mtoto anaweza kulala hata nusu saa na akakojoa. Alianza tabia hizi akiwa na Miaka mitatu

Tembelea - https://jamii.app/MtotoKukojoa
#JFMalezi #Malezi
👍6
RWANDA: MISHAHARA YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI KUONGEZWA KWA 88%

Nyongeza hiyo ni sehemu ya Mikakati inayolenga kuboresha Maslahi ya Walimu na kukuza ubora wa Elimu

Waziri wa Elimu amesema Mishahara ya Walimu wa Shule za Sekondari nayo itaongezeka kwa 40%

Soma - https://jamii.app/WalimuRW

#Governance
👍28🥰3
BURKINA FASO: Jeshi limekiri kuua raia wa kawaida kimakosa katika mashambulizi yake ya anga Kusini Mashariki mwa Nchi hiyo

> Burkina Faso imekuwa ikipambana na Waasi wanaohusishwa na Makundi ya Al-Qaeda na ISIL (ISIS)

Soma https://jamii.app/MapiganoBurkinaFaso

#JamiiForums
👍5👎1
#COVID19: Shirika la Madawa la Ulaya linapendekeza Chanjo ya Novavax kubeba onyo la uwezekano wa Mtumiaji kupata madhara Moyo ya aina mbili ambayo ni 'Myocarditis' na 'Pericarditis'

> Hadi sasa chanjo hiyo imetolewa kwa Watu 250,000 Barani Ulaya

Soma https://jamii.app/NovavaxEffects
#JFAfya
👍5
Ibara ya 8 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa Mwananchi nafasi ya kushiriki katika shughuli za Maendeleo ya Nchi

Ushirikishwaji Wananchi katika mchakato wa Bajeti ni muhimu kwasababu husaidia kuifanya izingatie vipaumbele vyao

Pia, huongeza ufanisi katika usimamizi wa Mapato na Matumizi ya Fedha za Umma katika ngazi ya Vitongoji, Vijiji/Mitaa na Kata

#JamiiForums #WAJIBU #JFUwajibikaji
👍9
CHELSEA YAWAWINDA AUBAMEYANG NA DE JONG

Frenkie de Jong na Pierre-Emerick Aubameyang wote ni Wachezaji wa Barcelona

> Barcelona inataka kuwauza Wachezaji hao ili kuweka sawa vitabu vya mahesabu ya klabu

Soma https://jamii.app/TransferBarca

#JFSports
👍6
KENYA: Mahakama ya Juu imebatilisha uamuzi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) wa uandikishaji wa Wapiga kura kwa Mfumo wa Kielektroniki pekee kwa kigezo cha kuepuka Uchakachuaji wa Kura katika Uchaguzi wa Agosti 9

Soma https://jamii.app/Kenya2022Uchaguzi

#KenyaDecides
🥰1
MAREKANI: Wanahabari wa #Reuters wamepanga kugoma kupinga ongezeko la Mishahara la 1% ambalo haliendani na Mfumuko wa Bei wa 9%

> Hivi karibuni Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari nchini humo wamelalamika kutotendewa haki na Waajiri wao

Soma https://jamii.app/MgomoReuters
👍4👏1😁1
MAREKANI: Rais Joe Biden amesaini amri inayolenga kulinda Haki ya kutoa Mimba

Amri hiyo inawataka Maafisa wa #Afya kuruhusu Fedha za Umma kutumika kuwasaidia Wanawake kusafiri kwenda kwenye Majimbo wanakoweza kutoa Mimba

Soma - https://jamii.app/BidenMimba

#HumanRights
👎6👍5🤯3
INDIA: Bunge limetupilia Mbali Muswada wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi na Faragha unaotajwa kuipa Serikali Mamlaka ya kudai taarifa za Wateja kutoka kwa Kampuni za Teknolojia

Wadau wamesema hatua hiyo italinda faragha za Raia

Soma https://jamii.app/DataProtectionAndPrivacy

#DigitalRights
👍3
Kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Mawasiliano (ITU) Mataifa ambayo gharama za Intaneti zipo juu yana idadi kubwa zaidi ya watu wasiotumia Mtandao

Intaneti ni Huduma ambayo inategemewa na wengi katika shughuli zetu. Ni muhimu kila mmoja kuweza kuifikia ili kunufaika nayo kikamilifu

#DigitalRights
👍9
Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu (CRPD) ulipitishwa mwaka 2006 kukabiliana na ukiukwaji mkubwa wa #HakiZaBinadamu unaofanywa dhidi ya Watu wenye Ulemavu duniani kote

Ni muhimu kwa Watu wenye Ulemavu kuwa washiriki hai katika Jamii zao na kuishi Maisha yenye kuridhisha

Fahamu zaidi - https://jamii.app/CRPD15

#HumanRights
👍21
IRINGA: KINYOZI AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 KWA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI

Batista Ngwale (27) amekutwa na hatia katika Mahakama ya Wilaya ya Iringa, ikielezwa alisababisha Binti kusitisha masomo

Binti huyo alikuwa anasoma Kidato cha Nne

Soma > https://jamii.app/HukumuIringa

#JFMatukio
👍6
UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Eric Hamissi kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL). Amewahi kuhudumu kama Mkurugenzi Mkuu wa TPA

Vilevile, Stephen Kagaigai ameteuliwa na Rais kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TBC

#Governance
👍5👎3
FAIDA ZA MTOTO KUNYONYESHWA NDANI YA SAA MOJA BAADA YA KUZALIWA

1) Kusaidia Maziwa ya Mama kutoka mapema

2) Kusaidia kumpa Mtoto joto

3) Kujenga uhusiano wa kihisia na upendo kati ya Mama na Mtoto

Fahamu zaidi > https://jamii.app/KunyonyeshaMtoto

#WorldBreastfeedingWeek
👍12😁21
SOMALIA: Umoja wa Mataifa umesema takriban 90% ya Raia wanakabiliwa na ukame Nchini humo, hali iliyopelekea watu 918,000 kuhama makazi yao

Pia Utapiamlo pamoja na milipuko ya magonjwa inaripotiwa kuongezeka

Soma - https://jamii.app/SomaliaDrought
👍9